YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday 22 December 2013

JAMAA AKIMBIA GESTI AKIWA MTUPU BAADA YA KUFUMANIWA NA MKEWE AKIWA NA KIMADA WAKIVUNJA AMRI YA SITA...!!




DUNIA ina mambo jamani! Mfanyabiashara wa madini aliyefahamika kwa jina moja la Jimmy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na kimada gesti.
Tukio hilo lililofunga mtaa kwa kujaza wambea kibao, lilitokea hivi karibuni ndani ya gesti hiyo (jina tunalo) Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mke wa mfanyabiashara huyo (jina halikupatikana mara moja), alimnasa mumewe  akijiandaa kuvunja amri ya sita ya Muumba.
Mke wa mfanyaiashara (kulia) baada ya kumfumania kimada akiwa na mumewe gesti maeneo ya Kinondoni, jijini Dar.
Wadakuzi waliokuwa eneo la balaa walitonya kuwa, siku hiyo ya tukio, Jimmy ambaye ni mkazi wa jijini Arusha, alifika Dar kibiashara na baadaye alimsaka kimada huyo wa siku nyingi na kwenda kujirusha naye bila kujua mkewe alishatonywa juu ya usaliti wake.
Awali chanzo makini kinachojua nini maana ya habari kiliwatonya mapaparazi wetu mara baada ya kupata mchongo wa fumanizi kutokea Sinza ya Kumekucha lililoandaliwa na mke wa Jimmy.

“Nyie njooni tu hapa Sinza-Kumekucha ndipo mkewe alipotonywa na dereva wa mumewe kuwa anaibiwa na kimada. Kuna gesti moja ipo ndani kidogo upande wa kushoto kama unaelekea Shekilango,” kilisema chanzo.
Timu ya mapaparazi ilifika katika gesti hiyo lakini bahati mbaya waliambiwa kuwa, Jimmy na kimada huyo walihamisha kiwanja cha starehe na kwenda Kinondoni.
                                               Kimada aliyefumaniwa na mume wa mtu.
Mapaparazi walipofika katika gesti hiyo ya Kinondoni, walimkuta mke wa Jimmy hivyo wakaambatana naye pamoja na askari polisi wawili kwa ajili ya kwenda kufumania.
Jimmy kabla ya kuingia gesti inadaiwa alijipumzisha katika grosari iliyo karibu na Mango Garden Bar, baadaye akaenda kwenye gesti hiyo ya jirani bila kujua mkewe alikuwa akitua mguu kila pale yeye aliponyanyua, akazama ndani ya gesti hiyo na kuanza kujiandaa kwa zinaa.
Mke wa Jimmy hakuwa mbali, baada ya kujiridhisha mumewe amezama chumbani, dakika kadhaa na yeye alitokea na kugonga mlango wa chumba hicho kufuatia kutonywa na mhudumu mmoja wa gesti hiyo.
Jimmy alikutwa tayari ameshavua nguo zote na kubakiwa na ‘boksa’ huku kimada naye akiwa na ‘kufuli’ pekee.
Kilichofuata hapo ni kipigo, mke wa Jimmy alianza kumtembezea kipigo yule kimada. Mapaparazi walivamia na kutandika picha za timbwili ambapo Jimmy alifanikiwa kupenya mlangoni na kukimbia bila kujali nguo nyingine.
Kutokana na kelele za timbwili hilo, majirani wa eneo hilo walifika kuhoji kulikoni ambapo mfumaniaji huyo alitoboa siri kwamba amekuwa akimfuatilia mumewe kwa siku nyingi baada ya kuambiwa ana kimada Dar.
“Huyo malaya akome kutembea na waume za watu. Nimekuwa nikimfuatilia mume wangu kwa muda mrefu. Nimetoka Arusha mpaka Dar kwa ajili yake. Kweli za mwizi ni arobaini, leo nimewanasa,” alisema mwanamke huyo huku akiondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.
Wakati pakichimbika, kimada huyo alisikika akimlaumu Jimmy kwamba amemuingiza kwenye mkenge akijua mkewe ni mdodosaji wa mambo na anaweza kufika Dar madai ambayo hayakuwa na wa kuyajibu.
Taarifa zaidi zilidai kuwa ndugu mmoja wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa na mchoro mzima 

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg