YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 16 September 2014

NEWS # MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA BUNGE MAALUMU LA KATIBA


MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam jana imetupilia mbali maombi ya pingamizi la awali la kusimamisha  Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma, iliyofunguliwa na  Mwandishi wa Habari Said Kubenea, kwa kuwa wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi.

Kadhalika, mahakama hiyo imetupilia mbali pingamizi hilo la awali, kwa kuwa mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.

Uamuzi huo ulitolewa chini ya jopo lililoketi la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Mh.Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi.

Jopo hilo lilisema mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo la awali kwa sababu halina mashiko ya kisheria.
Upande wa mlalamikiwa uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata na mlalamikaji Peter Kibatala.

Awali,  Mwanasehria Mkuu (AG) kupitia Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa maombi yake ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.

Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.
Mapema mahakamani hapo, Kubenea aliwasilisha maombi ya pingamizi la awali ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.

Katika kesi ya msingi iliyopewa usajili  namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011.

Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg