YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday 10 October 2014

BASI LA DAR EXPRESS LAPATA AJALI KILIMANJARO SIKU YA JANA


Muonekano wa basi la Dar Express lenye namba za usajili T640 AXL linalofanya safari zake Kati ya Dar na Rombo baada ya kupata ajali jana jioni eneo la Marangu, Mamba mkoani Kilimanjaro.
Wananchi wakiwa eneo la tukio muda mfupi baada ya basi la Dar Express kupata ajali.
(PICHA NA MTANDAO)

Saturday 4 October 2014

RAIS KIKWETE AKAGUA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA BINADAMU CHA UDOM


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianze kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha (mbele) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (kulia) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianze kazi rasmi hivi karibuni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (tai nyekundu) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianze kazi rasmi hivi karibuni.
Jengo kuu la  Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha Chuo Kikuu cha Dodoma  mjini Dodoma 
 Sehemu ya majengo ya Chuo  cha Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu ya UDOM mjini Dodoma
 Sehemu ya barabara ya lami ya kutoka na kuelekea vyuo mbalimbali vya UDOM
 Mhe. Baraka Konisaga, ambaye ni Mjumbe wa Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini akitoa rais binafsi muda mfupi kabla Rais Jakaya Mrisho Kikwete hajafunga rasmi kikao hicho cha siku tatu kilichojumuisha wajumbe zaidi ya 900 kuzungumzia sekta ya elimu ili  kupanga mikakati na kutatua changamoto zinazoikabili
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunga rasmi Kikao cha kazi cha viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri nchini katuika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma

TAMASHA LA FIESTA LAITEKA SINGIDA,KESHO JUMAPILI KURINDIMA MJINI DODOMA


 Baadhi ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Lina Sanga ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika jukwaani.
 Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.
 Mmoja wa mashabiki akishangilia huku akiwa amebebwa
 Msanii wa muziki wa bongofleva,Mr Blue a.k.a Kabyssal akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Sehemu ya umati wa watu ndani ya tamasha la Fiesta mjini Singida hapo jana katika uwanja wa Namfua
 Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
 Msaniii mwingine anaefanya vyema katika anga ya muziki wa bongofleva,kupitia kundi la WEUSI,Niki wa Pili akiwaimbisha mashabiki wake
 Shabiki kapagawa na yaliyokuwa yakijiri jukwaani.
 Badala ya kuwa watazamaji tu,nao pia walikuwa wakijimwaya mwaya taratiibu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kizazi kipya atambulikae kwa jina kisanii Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Msanii Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja jukwaani,huku miluzi na makelele ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la Fiesta likiendelea.
 Mashabiki wakishangilia
 Wasanii mahiri wa muziki wa Bongofleva,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Singida wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la Fiesta.PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.

HII NI FURAHA YA MATOKEO YA RASIMU YA KATIBA AU KUNA MENGINE?


Member of the CA,Deo Sanga could not hide his joy and walked at the centre of the debating chamber to celebrate vote results that endorsed final Draft Constitution in Dodoma on Thursday. 

TAZAMA PICHA ZA PALIPOFANYIKA BIRTHDAY PARTY YA CHIBU DANGETO DIAMOND



D 2Party ilifanyika Golden Jubilee Towers Dar es salaam ambapo kama hujaona pichaz za kilivyohappen unaweza kuchek post iliyotangulia kabla ya hii kwenye hii siku kubwa ya Diamond aliyotimiza miaka 25 ya kuzaliwa.
D 3

D 4


d 5

KAMA HUJUI BASI HUU NDIO UTAJIRI MCHAFU WA MSANII JOSE CHAMELEONE HAPA!SHUKA NAYO





Joseph Mayanja going by the Stage name Jose Chameleone is a Ugandan Born Singer 35 of age. Jose is an Afrobeat and Reggae musician based in Uganda and currently ranked as the wealthiest musician across East Africa. He is married to Daniella Atim who happens to be a Socialite both blessed with a daughter.Chameleon lives in a palatial home worth Sh17 million in the outskirts of Kampala. He also owns Coco Beach, a top entertainment spot on the shores of Lake Victoria, estimated at Sh27 million, a Cadillac Escalade, a convertible BMW, a Premio, aToyota Ipsum, a Landcruiser VX, Mercedes ML270 among other whips. The Bayuda star is also said to own an apartment in Arizona, USA and a posh house in Kigali, Rwanda. Chameleone recently unveiled what could be his latest investment-the Daniela Villas (named after his wife) in one of the uptown suburbs of Kampala, Namboole. 




Here are Photos of Chameleone's Expensive Lifestyle; 

















SAMUEL SITTA, NISINGESHIRIKI KARAMU YA WENYE DHAMBI


Mheshimiwa Samuel Sitta.
Kwako mheshimiwa Samuel Sitta.
Ni matumaini yangu kwamba sasa unajipongeza kwa kufanikisha kazi uliyopewa ya kuliongoza Bunge Maalum la Katiba ya kuhakikisha akidi inatimia ili kupitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa.

Najua una furaha sana kwa hilo, upo kwenye karamu ya kufurahia ushindi kiasi kwamba itakuwa vigumu sana kwa lofa kama mimi kukutana na wewe hasa katika kipindi hiki ambacho unaamini kasi na viwango vyako vimedhihirika. Hata hivyo, hilo halinizuii kufikisha ujumbe wangu kwako.
Mimi si Mbunge wa Urambo Mashariki kama wewe, sikuzaliwa Desemba 18, 1942 wala sijamuoa mwanamke mwanasiasa, Magreth Sitta aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali kama wewe. Mimi ni mwananchi wa kawaida tu, lofa, hohehahe nisiye na mbele wala nyuma.
Sijawahi kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala sijawahi kujipatia umaarufu mkubwa na kupendwa na wengi kutokana na kuruhusu mijadala ya ufisadi bungeni kama ulivyo wewe. Sijawahi kuibua kashfa kubwa kama ya Richmond na kusababisha baadhi ya vigogo wang’atuke kwenye nyadhifa zao.
Sina nia wala sitegemei kuja kugombea urais wa nchi hii kama wewe, mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa. Sijawahi kujisifu kwamba mimi ni mtu wa viwango na kasi, mimi ni mlala hoi tu.
Sijawahi kuitumia nchi hii katika nyadhifa mbalimbali kuanzia nilipokuwa shule, kwa zaidi ya miaka 40 nikigusa karibu awamu zote za uongozi kama wewe, mimi si Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wala sijawahi kuota ndoto kwamba nitakuja kuwa Spika wa Bunge Maalum la Katiba! Narudia tena, mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa, hohehahe nisiye na ndoto za kuja kuwa mwanasiasa.
Hata hivyo, ningekuwa mimi ndiyo nipo kwenye nafasi yako, hakika nakuapia nisingeshiriki kwenye karamu ya wenye dhambi kama wewe. Nisingeshiriki hata kidogo kuchakachua maoni ya mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, Jaji Joseph Warioba kama wewe.
Nisingerudia kukusanya upya maoni kwa wananchi wakati nikijua fika kuwa hiyo siyo kazi yangu. Nisingebadilika ghafla kama wewe, kutoka kuwa shujaa wa kutegemewa kama ulivyokuwa kipindi ulipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuwa adui wa demokrasia kama ulivyo sasa.
Nakuhakikishia nisingeshiriki kabisa karamu ya wenye dhambi, kwa kulazimisha wajumbe wa bunge maalum la katiba, hata kwa vitisho waipigie kura ya ndiyo rasimu ya katiba inayopendekezwa huku nikijua waziwazi kwamba nimeshiriki kunyofoa vipengele vyote muhimu ambavyo wananchi walivipendekeza ili kupata katiba bora.
Nisingefikia hatua ya kuwatusi viongozi wa dini ambao walikuwa wakinionesha waziwazi kwamba nilichokuwa nakifanya kwenye bunge maalum la katiba hayakuwa matakwa ya Mungu bali ya watu wachache wenye dhambi.
Kwa kuwa najua kwamba katiba ndiyo ‘injini’ ya maendeleo ya taifa lolote, ningekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba maoni ya wananchi ndiyo yanayoingia kwenye katiba bila kuchakachuliwa. Ningethibitisha kwa vitendo kwamba mimi ni mtu wa kasi na viwango!
Nisingekubali kuongozwa na tamaa ya kuja kuwa rais wa nchi hii kiasi cha kulipua mchakato mzima wa kupata katiba kwa maslahi yangu na chama changu kwa sababu ningejua kwamba umri umeshanitupa mkono (Una miaka 71 sasa) lakini wapo wanangu, wajukuu na ndugu zangu wengi na watu wanaoniamini ambao wanaisubiri kwa hamu katiba mpya itakayowakomboa, baada ya ile ya awali kushindwa kuwatatulia kero zao kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.
Narudia tena, nisingeongozwa na tamaa ya madaraka, upendeleo kwa chama changu wala maslhai ya mtu au watu fulani, la hasha! Ningesimamia haki katika ukamilifu wake na rasimu ambayo ingepatikana, ingekuwa ni mawazo ya wananchi wote na siyo uhuni kama uliofanyika sasa kupata rasimu ya katiba inayopendekezwa.
Ningeongozwa na hofu ya Mungu na nisingewaangusha wananchi ambao kwa kipindi kirefu waliniona mpiganaji ninayesimamia maslahi yao na taifa kwa jumla na kamwe nisingeshiriki karamu ya wenye dhambi kama ilivyotokea kwenye Bunge Maalum la Katiba. 
Kwa bahati mbaya mimi nitabaki kuwa mimi na sitaweza kuwa wewe lakini kama ningekuwa mimi kwenye nafasi yako, kwa jinsi hali ilivyo sasa, narudia tena kusema bila kumung’unya maneno kwamba nisingeshiriki kwenye karamu ya wenye dhambi kama wewe, ningesimamia ukweli, haki na demokrasia bila kumpendelea wala kumkandamiza mtu yeyote.
Wasalaam!CHANZO GLOBAL PUBLISHER TANZANIA