YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday, 11 April 2013

MAMBO YA GOAL TECHNOLOGY SASA YAMEFIKA HAPA.

2
.
.
Kampuni ya Uingereza ya Hawk Eye imepewa mkataba wa kufunga na kuendesha mifumo ya teknolojia ya mstari wa goli maarufu kama Goal Line Technology kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya England.
Maamuzi hayo yamefanyika kwenye mkutano wa vilabu vya ligi hiyo ambavyo vimeridhia matumizi ya teknolojia hiyo kuwasaidia waamuzi kutambua pale goli linapofungwa.
.
.
Mara ya mwisho kampuni hiyo ambayo inatoa huduma kama hiyo kwenye michezo ya Cricket na Tenis ilishindwa na kampuni ya Goal Control ya Ujerumani ambayo imezawadiwa tenda ya kufunga mifumo ya Goal Line Technology kwenye michuano ya Kombe la mabara na tayari imeanza kufanya kazi ya majaribio ya kufunga camera kwenye uwanja wa St Mary’s wa timu ya Southampton.
Tayari chama cha soka cha England FA kimepitisha matumizi ya teknolojia hiyo kwenye uwanja wa Wembley ambapo itaanza kutumika kwenye mchezo wa ngao ya Jamii mwezi Agosti 2013.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg