YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday 17 August 2018

MJUE ALIYEKUA RAISI MASKINI ZAIDI DUNIANI

Former Uruguayan President José Mujica drives a tractor on his farm on the outskirts of Montevideo, Uruguay

Haki miliki ya picha
Image captionJosé Mujica amestaafu kutoka seneti kutumia muda kwenye shamba lake
Aliyekua rais wa Uruguay Jose Mujica, aliyejulikana kama rais maskini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu aanze kuhudumu kama seneta.
Mujica aliacha kazi ya useneta mnano Jumanne, kiti ambacho amekua akishikilia tangu muda wake wa kuhudumua kama raisi ukamilika mwaka wa 2015.
Alidai kuwa amechoka na hangeweza kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020. Muasi huyo wa zamani wa mrengo wa kushoto ana miaka 83.
Mujica aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti. Alisema ya kwamba fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni uchovu wa safari ndefu.
Hata hivyo aliongeza kua ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili yake inafanya inafanya kazi.
Mujica anayejulikana kwa matamshi yake ya kichesi aliomba msamaha kwa wenzake kwa uamuzi huo.
Mwaka 2016, alidai rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama mbuzi.
Umaarufu wake ulienea kutokana na maisha yake ya chini ya kukataa kuishi kwenye ikulu ya rais.
Former Uruguayan President Jose Mujica speaks with Barcelona"s Deputy Mayor, Argentinian Gerardo Pisarello (not pictured), in Montevideo, Uruguay, 06 August 2018Haki miliki ya picha
Image captionAlitoa mshahari wake kwa misaada na kile alichobaki nacho tu alipoingia ofisini mwaka wa 2010 ni gari aina ya Volkswagen Beetle la mwaka 1987.
Wakati akiwa rais na hata sasa, yeye pamoja na mkewe, ambaye pia alimusaidia katika vita vya msituni wamekua wakiishi katika shamba moja nje ya kidogo mwa mji wa Montevideo.
Alitoa mshahari wake kwa misaada na kile alichobaki nacho tu alipoingia ofisini mwaka wa 2010 ni gari aina ya Volkswagen Beetle la mwaka 1987.
Gari hilo lilipata umaarufu na mwaka 2014 alipewa dola milioni moja lakini akataa huku akidai kuwa atashindwa kumbeba mbwa wake mwenye miguu mitatu.
Kuacha kazi kwa Mujica hakukupokelewa na mshangao kwa sababu alikua amedokeza kufanya hivyo mnano Agosti 3 alipofika mara ya mwisho seneti.

    No comments:

    Post a Comment

    gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg