YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 21 August 2018

MKE WA RAISI TRUMP KUFIKA AFRIKA

Mke wa rais wa Marekani Melania Trump anatarajiwa kufanya ziara barani Afrika

Haki miliki ya picha
Image captionBi. Melania Trump anatarajiwa kufanya kazi za kibinadamu barani Afrika
Mke wa rais wa Marekani Melania Trump anatarajiwa kufanya ziara barani Afrika mwaka huu ingawa haijafahamika ni maeneo gani ya bara hilo ataweza kutembelea.
"Hii itakuwa safari yangu ya kwanza barani Afrika na shauku yangu kubwa ni kutoa mafunzo juu ya masuala yanayowahusu watoto na vilevile kujifunza juu ya utajiri wa utamaduni na historia ya bara hilo la Afrika" Melania alielezea.
Bi.Trump anatarajia kufanya ziara barani Afrika bila kuongozana na mume wakeHaki miliki ya picha
Image captionBi.Trump anatarajia kufanya ziara barani Afrika bila kuongozana na mume wake
Bi.Trump anatarajia kuangazia masuala ya kazi za kibinadamu na miradi ya maendeleo ambayo yaliwahi kufanywa katika mataifa mbalimbali
Rais Donald Trump ambaye aliwahi kukosolewa kwa kuzidharau baadhi ya mataifa ya Afrika licha ya kwamba alikana kuwa mbaguzi hatasafiri na mke wake kuja barani Afrika.
Rais Trump hajawahi kufanya safari ya Afrika tangu aingie ofisini mnamo januari 2016.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg