YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 2 April 2013

HUYU NDIO PROFESA ANAESEMA NI DAKTARI WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA

0
.
Profesa Easter Mwaikambo.
Post hii ni maalum kwa Profesa Easter Mwaikambo ambae anasema yeye ndio Daktari wa kwanza kabisa Tanzania kazi aliyoianza miaka 44 iliyopita.
Namkariri akisema “Mimi ni Daktari wa kwanza kabisa Mwanamke Tanzania na ndio mwanzilishi wa MEWATA mwaka 1987 na nimekiongoza kama Rais kwa karibia miaka 20″
“Mimi ni mwenyeji wa Moshi, nimeolewa Unyakyusani… mimi sio Daktari wa kwanza tu Mwanamke Tanzania, nilikua Daktari kwanza Tanzania, nimekua Mwanamke wa kwanza Profesa kwenye fani ya Medicine, nimekua Mwanamke wa kwanza kuwa Vice Chancellor wa chuo kikuu hapa Tanzania na mambo mengi sana”
Profesa Easter ambae ana umri wa miaka 72 amesema kwa sasa Madaktari wa kike Tanzania kwa sasa wanazidi elfu moja, na katika chuo anachofundisha cha Udaktari anaona idadi ya Wanawake wanaojiandikisha kusomea Udaktari inaongezeka.
Kwenye sentensi ya mwisho Profesa amesema baada ya mwaka mmoja baada ya yeye kuwa Daktari pekee wa kike Tanzania (1969) mwaka uliofata (1970) waliongezeka na Tanzania kuwa na Madaktari watatu Wanawake Tanzania ambapo idadi ya Madktari Wanawake ilianza kuongezeka kwa wingi mwaka 1979.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg