YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 2 April 2013

Maafa juu ya maafa, Dar 36 Arusha 20


Kile kilichodhaniwa kuwa kilele cha sikukuu ya pasaka, kimegeuka msiba baada ya wachimba kokoto 20 kufukiwa katika kifusi Jijini Arusha.
Hiyo ilikuwa ni kama ndimu katika kidonda kibichi, kwani ni ijumaa iliyopita tu wakati watu wakijiandaa kwa sikukuu ya Pasaka jengo la ghorofa 16 lilidondoka Jijini Dar es Salaam na kuua watu 36.
Vifo hivi vilivyotokea katika msimu wa sikukuu vimeweka idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 56 hivi, ndani ya  siku nne tu.
Watu waliofukiwa na kifusi mkoani Arusha, walikuwa wakichimba kokoto katika eneo la Moshono.
 Imeelezwa kuwa ni maiti 14 tu ndizo zilizoopolewa na watu wengine bado wanahofiwa kuwa ndani ya kifusi hicho.
 Ilikuwa ni saa tano asubuhi, juzi, gema la kokoto liliporomoka kisha kuwafunika wote waliokuwamo ndani, sababu kubwa ikielezwa kuwa ni mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha mjini Arusha.
 Vilevile magari mawili yaliyokuwa yamepaki pembeni kwa ajili ya kubeba mzigo huo yalizama ndani ya shimo hilo kubwa la kokoto.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg