YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday, 19 September 2013

Hofu ya mashahidi Kenya kuhusu ICC


Jaji anayeongoza vikao hivyo amewaonya wanablogu dhidi ya kuwatambulisha mashahidi katika kesi hiyo
Mwanamke mmoja nchini Kenya amesema kuwa anahofia maisha yake baada ya kutambuliwa visivyo kwenye mitandao ya internet kwamba yeye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
Mwanamke huyo anasema aliathirika na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008 lakini yeye si shahidi katika mahkama ya ICC.
Mama huyo Rahab Muthoni Kagiri ,mwenye umri wa miaka 27 kutoka eneo la Burnt Forest , huko Rift valley anasema yeye sii shahidi katika kesi hiyo inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto pamoja na mtangazaji wa zani Joshua arap Sang.
Akionekana mwenye wasiwasi Bi Rahab asema sie yeye aliyesimama kizimbani kama shahidi wa kwanza katika kesi hiyo kinyume na inavyodaiwa na mitandao ya kijamii nchini Kenya.
Mama huyo anadia kuwa picha hiyo alipigwa na rafiki yake kwa lengo la kuiweka katika mtandao wake wa Facebook majira ya saa tano siku ya jumanne.
Lakini alishangaa saa mbili baadaye alianza kupigiwa simu na jamaa , ndugu na marafiki wakisema wameona picha yake katika mtandao ukisema yeye ndie shahidi aliyetoa ushahidi dhidi ya naibu Rais Wiliam Ruto.
Bi Rahab anasema japo yeye pia ni muathiriwa wa machafuko yaliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1,00 waliuwawa lakini hajajitolea kutoa ushaidi katika mahakam hiyo ya ICC.
Na kutokana na madai ya ufichuzi wa mashahidi nchini Kenya , hii leo Mahakama ya ICC iliamuru shahidi wa kwanza ambaye alianza kutoa ushaidi wake siku ya jumatatu atoe ushahidi wake faraghani.
Hii nikutokana na kudaiwa kuwa na hofu nyingi

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg