YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday 23 September 2013

HUYU NDIYE MWANAMKE ADAIWA NDIO KIONGOZI WA MAGAIDI WA AL SHABAAB WALIOTEKA WESTGATE MALL KENYA

Mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi ya 175.



Tayari mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi hao walioshambulia Westgate.

Nayo akaunti ya Twitter ya American Jihad Watch ‏@watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on mall camera at Westgate Centre Shopping mall earlier yesterday may be infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.


Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo

Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.


Kwa mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.

Hata hivyo Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph, jana usiku ofisa wa shirika la kupambana na ugaidi Kenya alikanusha taarifa kuwa Samantha Lewthwaite anaweza kuhusika na shambulio la jana.

Samantha Lewthwaite aka The White Widow ni nani?

Ni mwanamke anayetafutwa kwa udi na uvumba kwa kuhusika kwake kwenye matukio mbalimbali ya kigaidi nchini Uingereza na Afrika Mashariki. Yeye ndiye aliyepanga shambulio la kigaidi jijini London la mwaka 2005 lililosababisha vifo vya watu 52 ambapo mume wake Jermaine Lindsay alijitoa muhanga.


Akitokea Aylesbury, Buckinghamshire, nchini Uingereza, The White Widow kwa sasa ni kiongozi wa juu wa mashambulio ya Al Shabaab nchini Kenya na Somalia. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa shughuli za kundi hilo la kigaidi.

Mwezi May hati ya kumkamata ilitolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani nchini Kenya kwa kesi ya kutengeneza bomu.

TAZAMA PICHA ZA DIAMOND PLATNUMZ AKILA BATA MALAYSIA


diamod6

Diamond leo tarehe 20/9 anafanya show ndani ya jiji la Kuala Lumpur huko Malaysia. Tangu jana alikuwa ameshafika na hizi ni baadhi ya picha ambazo Diamond amezipiga akiwa huko Kualar Lumpar kabla ya kufanya show leo usiku kwa mada wa huko.
diamond3
diamond5
diamond2

MSANII WA BONGO FLEVA SAM WA UKWELI AELEZEA JINSI ALIVYOMUUA MDOGO WAKE BILA KUKUSUDIA



Sam ameeleza kuwa hakuna kitu kinachomuuma sana kama siku alipomdondosha mdogo wake chini na kumsababishia kifo kutokana na kuanguka kwake,msanii huyo amesema kuwa kisa hicho kilitokea wakati mama yake akiwa shambani na kumuacha sam na mdogo wake na ilipofika mchana sam aliyekuwa kambeba mdogo wake huku akitokea ndani ndani akiwa kabeba uji wa huyo mtoto,ila kwa bahati mbaya sam alijikwaa na kudondoka chini na kumfanya yule mtoto alie sana hadi baba huyo wa kufikia wa sam alipokuja na kuanza kumfokea sam hadi mama yake alipokuja na kumnyonyesha mtoto na kulala ula usiku mtoto alianza kulia kwa staili ya kustuka ikapidi wampeleke hosptali ya mision na alipoangaliwa alionekana hana kitu ikabidi waondoke nae hadi kwa wataalamu wa jadi ila muda mfupi yule mtoto akafariki.

Sam anasema kuwa baada ya hapo baba huyo wa kufikia alisema sam kamuua mwanae maksudi na kuleta mtafaruku mzito katika familia yao jambo lililosababisha ndoa hiyo kuvunjika  na wakarudi kwa bibi yake mzaa mama  na ndipo walipokuja kushangaa baada ya  baba yao mzazi ambae waliambiwa kafa kurudi nyumbani akiwa mzima kabisa na ndio safari ya kuja dar kwa mara ya kwanza.

TAFSIRI YA KISWAILI YA MAHOJIANO YA MSEMAJI WA AL-SHABAAB JUU YA UVAMIZI NA MAUAJI YA WATU KENYA



Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda. Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.

JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?

Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya. Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu. Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.

JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?

Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo. Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya jiji. Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile Mkenya.

JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?

Msemaji:
 Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.

JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?

Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.

JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?

Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.

JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?

Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.

JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?

Msemaji:
 Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.

JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?

Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.

JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?

Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia. Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya.

HAWA NDIO WASHINDI WA TUZO ZA TANZANIAN BLOG AWARDS:


Tanzanian Blog Awards
Nashukuru sana kwa wote waliopigia kura blog yetu ya bossngasa.com na kufanya kuwa mshindi wa kwanza katika Category ya the best newcomer blog,shukrani na pongezi kwa wote walioshiriki zoezi hili:

The Best Newcomer Blog

Bonyeza hapo chini kuona matokeo yote kwa wale walioshiriki:

http://tanzanianblogawards.blogspot.com/

PICHA ZINGINE NAMNA DAMU ILIVYOMWAGIKA KENYA,TAHADHARI PICHA ZINGINE NI MBAYA SANA



Mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa akiomba msaada
September 21, ni tarehe ambayo Kenya haitoisahau kamwe. Ni baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab lilipoishambulia mall ya Westgate maarufu kwa kuwa na wateja matajiri jijini Nairobi na kuwashikilia watu mateka, kuwaua na kuwajeruhi wengine.

   Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatariFamilia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari
 article-2427892-182485E800000578-152_964x631130921145130-25-kenya-mall-restricted-horizontal-gallery130921103725-07-kenya-mall-horizontal-galleryMashuhuda wanasema watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na nguo nyeusi na vichwa vyao vikifunikwa na vilemba waliingia kwenye mall hiyo ya Westgate jana mchana. Mpaka sasa, idadi ya watu walioshikiliwa mateka ndani ya mall hiyo haijajulikana.Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatiliMama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatiliMfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyoMfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyoMtoto akikimbia kuokoa maisha yakeMtoto akikimbia kuokoa maisha yakeMtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Zaidi ya watu 40 wameripotiwa kuuawa na zaidi ya 162 wakijeruhiwa.Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo haoMtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo haoMwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askariMwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askariMwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shoppingMwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shoppingMwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwaMwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwaOfisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silahaOfisa wa usalama na wenzake wakielekezana na wenzake mahali walipo watu hao wenye silahaPolisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mallPolisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mallPolisi na wanajeshi wakipambana na magaidi haoPolisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao Mashuhuda wengine wamedai kuwa wanamgambo hao waliwaambia waislamu waondoke na wabaki waumini wa dini zingine. “Walisema na kusema: ‘Kama wewe ni muislamu, simama. Tumekuja kuwaokoa,” Elijah Lamau aliiambia BBC. Alisema waislamu waliondoka wakiwa wamenyoosha mikono juu na kisha watu hao wakawapiga risasi watu wawili.Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-ShababPolisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-ShababPolisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-ShababPolisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-ShababPolisi wakipambana na Al-shababPolisi wakipambana na Al-ShababRais wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi haoRaia wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi haoWanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-shababWanajeshi walimwaga kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaida la Al-ShababWananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silahaWananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha Gaidi mmoja alikamatwa jana na kufa kutokana na majeraha. Maafisa wa Kenya wameimbia BBC kuwa wengine wanne wamekamatwa

BAADA YA MPOKI KUJIPENDEKEZA KWA DEMU WA KIZUNGU, MZUNGU AMPIGA CHINI. TAZAMA MCHEZO MZIMA ULIVYOKUA


PICHA YA KWANZA KABISA IKIONYESHA MAGAIDI WA AL SHABAAB NDANI YA MALL YA WESTGATE KENYA



Suspected AlShabaab fighters inside #Westgate. Look how comfortably they are walking around as if they're shopping 

UPDATE: OPERESHENI YA KUWAKOMBOA MATEKA WANAOSHIKILIWA NA AL-SHABAAB HUKO NAIROBI KUKAMILIKA MUDA MCHACHE KUANZIA SASA..!!


Jeshi la Kenya limefanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate na wanaendelea vema na operesheni ya kuhakikisha wanawakomboa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa kundi la Alshabab ambao walivamia na kuteka eneo hilo jumamosi mchana.

Msemaji wa jeshi la kenya kanali Cyrus Oguna amethibitisha operesheni ya kuwakomboa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Alshabab imefikia hatua ya mwisho na inaweza kutamatika muda wowote.

Idadi ya watu waliopoteza maisha imeongezeka na kufikia 69 wakati majeruhi wakifikia 175 kwa mujibu wa serikali nchini Kenya.Misaada ya aina mbalimbali imeendelea kutolewa ikiwemo zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi ambao wengine wamefanyiwa upasuaji.

Tukio la mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Al-Shabab kwenye maduka ya westgate nchini kenya limezusha hofu miongoni mwa mataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Maziwa makuu.

Serikali za Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi zimelaani shambulio hili na kutoa pole kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na wananchi wa taifa hilo ambao wamepoteza ndugu zao.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa kenya kwasasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kiusalama hali ambayo ni lazima nchi jirani ziimarishe usalama kwenye mipaka yao.

PICHA: JEURI YA FEDHA..!! DIAMOND PLATNUMZ AVAA GRAMU 87.97 ZA GOLD SHINGONI KWAKE...!!




JAMAA MZIGO KANUNUA MALAYSIA BAADA YA SHOW YA JANA

HUYU NDIYE ELIZABERT MICHAEL (LULU)AKIWA NA VAN VICKER WA GHANA





Thursday 19 September 2013

Hofu ya mashahidi Kenya kuhusu ICC


Jaji anayeongoza vikao hivyo amewaonya wanablogu dhidi ya kuwatambulisha mashahidi katika kesi hiyo
Mwanamke mmoja nchini Kenya amesema kuwa anahofia maisha yake baada ya kutambuliwa visivyo kwenye mitandao ya internet kwamba yeye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
Mwanamke huyo anasema aliathirika na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008 lakini yeye si shahidi katika mahkama ya ICC.
Mama huyo Rahab Muthoni Kagiri ,mwenye umri wa miaka 27 kutoka eneo la Burnt Forest , huko Rift valley anasema yeye sii shahidi katika kesi hiyo inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto pamoja na mtangazaji wa zani Joshua arap Sang.
Akionekana mwenye wasiwasi Bi Rahab asema sie yeye aliyesimama kizimbani kama shahidi wa kwanza katika kesi hiyo kinyume na inavyodaiwa na mitandao ya kijamii nchini Kenya.
Mama huyo anadia kuwa picha hiyo alipigwa na rafiki yake kwa lengo la kuiweka katika mtandao wake wa Facebook majira ya saa tano siku ya jumanne.
Lakini alishangaa saa mbili baadaye alianza kupigiwa simu na jamaa , ndugu na marafiki wakisema wameona picha yake katika mtandao ukisema yeye ndie shahidi aliyetoa ushahidi dhidi ya naibu Rais Wiliam Ruto.
Bi Rahab anasema japo yeye pia ni muathiriwa wa machafuko yaliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1,00 waliuwawa lakini hajajitolea kutoa ushaidi katika mahakam hiyo ya ICC.
Na kutokana na madai ya ufichuzi wa mashahidi nchini Kenya , hii leo Mahakama ya ICC iliamuru shahidi wa kwanza ambaye alianza kutoa ushaidi wake siku ya jumatatu atoe ushahidi wake faraghani.
Hii nikutokana na kudaiwa kuwa na hofu nyingi

Tume ya Marikana - Polisi walidanganya


Wachimba migodi wa Marikana waliandamana wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi
Polisi wa Afrika Kusini wanatuhumiwa kwa kudanganya kuhusu mauaji ya Marikana yaliyotokea mwaka jana, ambapo wachimba migodi 34 waliuawa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa tume ya uchunguzi iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza mauaji hayo.
Inasemekana polisi walitoa ushahidi wa uongo au kuficha nyaraka ambazo zilitoa taarifa za uongo kuhusu matukio katika mgodi huo
Kitendo cha polisi kuwauawa kwa kuwapiga risasi wachimba migodi katika mgodi unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin kiliwashtua sana wengi nchini humo.
Polisi walisema kuwa walikuwa wanajikinga kutokana na kuvamiwa na wachimba migodi hao siku chache baada waandamanaji kudaiwa kuwanyonga polisi wawili.
Tume ihiyo iliteuliwa na Rais Jacob Zuma kuchungza mauaji hayo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kufanywa na polisi tangu kukamilika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Taarifa yake ambayo imekuja siku kumi baada ya kupata taarifa za polisi kwenye komputa zao na pia kupitia nyaraka zao.

SHAHIDI AFARIKI GHAFLA MAHAKAMANI WAKATI AKITOA USHAHIDI HUKO MKOANI MARA...!!



Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kijiji cha Lorwe Kata ya Nyahongo Shirati, wilayani Rorya, mkoani Mara, Charles Warito (38), ambaye ni shahidi wa  mlalamikaji  katika Kesi ya kudhuru mwili kwa kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa mkono na kusababisha ulemavu amefariki dunia, wakati akitoa ushahidi.

Warito alikutwa na umauti huo akiwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime mbele ya Jaji  G. Ndika anayesikiliza kesi katika Wilaya za Tarime na Rorya.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana mchana baada ya Mwanasheria wa Serikali, Mayega na Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta George Lutonja walimwita  kuingia Kizimbani tayari kutoa ushahidi.

Shahidi huyo alianza kutoa ushahidi wake na alieleza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na mtuhumiwa Kichohe Kichere ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Omoche Kata hiyo ya Nyahongo Shirati Januari 26, mwaka 2008 na kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kukatwa mkono na mwili wake ulianza kupooza na kulemaa upande wa kulia ambao mkono ulikatwa

Alipoanza kujibu maswali kutoka kwa wakili wa mtuhumiwa mara alianza kulegea na kuishiwa nguvu na kuanguka kizimbani na kuzimia  hali iliyofanya Mahakama hiyo Kusitisha Kusikiliza kesi na shahidi huyo kukimbizwa Hospitali ya Wilaya kupatiwa matibabu na alifariki kabla ya kupatiwa matibabu.

Mtuhumiwa katika kesi hiyo akiondoka haraka mahakamani hapo huku ndugu wa marehemu  aliyejitambulisha kwa jina Otieno Rada alisema: "Nimesikitishwa na kifo hiki cha ndugu yangu Charles Joseph kwani majeraha hayo aliyoyapata  ya kukatwa mkono na Kichere  yalisababisha alemae mkono na kuanza kupooza na yamechangia kifo chake."
Mwili wa marehemu Charles umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya Tarime ukisubili kuchukuliwa na ndugu zake kutoka Kijiji cha Lorwe Kata ya Nyahongo Shirati kwa maziko.

HUYU NDIYE MWANAMKE HATARI SANA KWA KUUZA MADAWA YA KULEVYA HADI OBAMA ANAMWOGOPA NA KUWA ADUI YAKE:



 
MWANAMKE raia wa Kenya, Naima Mohamed Nyakiniywa ambaye pia anatumia pasiport ya kusafiria ya Tanzania ikiwa na jina la Mwanaidi Ramadhani Mfundo maarufu kama Mama Leila, ni adui mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama kutokana na madai kwamba amebobea kwenye biashara ya madawa ya kulevya.
Obama, ambaye pia baba yake mzazi alikuwa Mkenya, mwaka 2011 alimtaja Naima katika orodha ya watu saba yeye akiwa wa 6 kuwa ni hatari kwa biashara hiyo haramu ya ‘unga’ ambapo pia aliamuru mali zake na wenzake hao zilizoko Marekani kutaifishwa, pia wasiruhusiwe kukanyaga ardhi ya taifa hilo kubwa duniani.
Septemba 16 na 17, mwaka huu, Mama Leila (na wenzake nane) alifikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa mashitaka ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin, Juni Mosi, 2011 Mbezi Beach jijini Dar.
Rekodi zinaonesha kuwa mwanamke huyo alizaliwa Septemba 2, 1962, Majengo, Nairobi, Kenya. Ingawa ni maarufu maeneo mengi ya mji huo mkuu wa nchi jirani, Pumwani, Majengo, Kariokor, Kaloleni, Biafra na Bahati, lakini katika hali ya usiri mkubwa, mwanamke huyo hafahamiki kwa majina ya Mama Leila, Naima au Nyakiniywa, isipokuwa anafahamika kama Kanyanya.
Kanyanya anayedaiwa kuwa mama wa watoto watano, katika eneo analoishi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam anajulikana ni Mtanzania kutoka kabila la Wadigo na majirani wanasema ni mtu mwema, mwenye moyo wa kusaidia walio na shida, akiwa pia ni mfanyabiashara wa magari, saluni na ‘internet cafes’.
Nchini Kenya, inadaiwa Kanyanya alikuwa mtu mwema katika eneo la Majengo huku majirani wakisema hakukuwa na njaa katika eneo lolote ambalo Naima alikuwepo na kila mtu alipata alichokihitaji.
Kutajwa kwake na Rais Obama kunadaiwa kuwashtua wakazi wengi wa Nairobi ambako kama ilivyo Mombasa na Dar es Salaam, anamiliki mali mbalimbali, yakiwemo majumba ya kifahari.
Hata hivyo, mwaka 2009, Polisi wa Kenya walidaiwa kuwakamata vijana watatu wakiwa na madawa ya kulevya na wote walimtaja Naima kama ndiye mwenye mzigo lakini ilikuwa vigumu kwao kumuunganisha kutokana na kukosa ushahidi.
Chanzo  chetu kimethibitisha kwamba wakati mmoja Naima aliwahi kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani jijini Nairobi lakini shinikizo kutoka ‘juu’ lilisababisha mwanamama huyo kuachiwa bila kufunguliwa mashitaka.
Inadaiwa kuwa hata alipokamatwa Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na biashara hiyo, kulikuwa na idadi ya simu za kutosha kutoka ofisi ‘kubwa’ jijini Nairobi zilizotaka aachiwe lakini polisi wa Bongo ‘walikomaa’ naye ili kumfahamu zaidi.
Naima anamiliki zaidi ya hati sita za kusafiria zenye majina na sura tofauti ili kufanikisha safari zake za mara kwa mara nje ya nchi na mojawapo ni ya Tanzania ambayo haifahamiki ilipatikana kutoka ofisi gani ya uhamiaji hapa nchini.
Katika orodha ya Rais Obama ya watu hao kutakiwa kufilisiwa mali zao na kutokanyaga Marekani, pia yupo mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilome, John Harun Mwau kutoka chama cha siasa cha Party of Independent Candidates of Kenya (PICK).
Wengine katika orodha hiyo ni Manuel Torres Felix wa Mexico, Gonzalo Inzunza Inzunza (Mexico) Haji Lal Jan Ishaqzai (Afghanistan), Kamchybek Asanbekovich 

AIBU!! MKE ASHIKWA UGONI NA WAKWE ZAKE AKIWA NA DEREVA WA BODABODA,MUME AANGUA KILIO....!!




WAZAZI wa mwanamme aliyejulikana kwa jina la Ally Maulidi Kambi, wakazi wa Kibada jijini Dar es Salaam wamemshika ugoni Farida Omar ambaye walidai ni mke wa Ally akiwa na dereva wa bodaboda, Risasi Mchanganyiko linakujuza mwanzo mwisho.
  Farida Omar akiwa na dereva bodaboda aitwaye Chidi baada ya kushikwa ugoni.
Tukio hilo la aibu lilijiri usiku wa Septemba 15, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kibada ambayo anaishi dereva huyo aliyejulikana kwa jina moja la Chidi.
KISA CHA UGONI
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kunaswa kwa Farida kulitokana na familia ya mumewe kutilia shaka nyendo za mwanamke huyo, hususan mumewe anapokuwa safarini.
“Wakwe zake, wakiwemo mashemeji na mawifi walishaziona nyendo za Farida kuwa si za kiuadilifu hasa mume wake anapokuwa safarini,” kilisema chanzo hicho.

 Mke akiwa chumbani kwa Chidi baada ya kunaswa na wakwe zake.
Kikaongeza kuwa mara nyingi mume akisafiri mwanamke huyo huenda kuishi na mwanamme mwingine mpaka mumewe anaporudi, hali ambayo imezua minong’ono mitaani kwa wale waliofanikiwa kujua hilo.
Maelezo ya wazi kutoka kwa vyanzo ni kwamba, chumba anachoishi Chidi kilipangwa na mwanamke mwingine na baadaye kumwachia Farida ili atanulie kiaina.

               Chumbani kwa Chidi alipokutwa Farida Omar.
WAKWE WAONGEA KWA JAZBA
Wakizungumza kwa jazba siku ya tukio, wakwe wa Farida ambao ni wazazi wa Ally walisema mwanamke huyo aliyeolewa na mtoto wao miaka mitano iliyopita, amekuwa si mwaminifu kwa mumewe hasa anapokwenda nje ya nchi, habari ambazo wao walizisikia na kuzifanyia kazi.
Waliongeza kuwa kutokana na tabia hiyo chafu, walijaribu kumuweka kikao mumewe na kumpasulia kila kitu lakini jamaa huyo hakuwa akiwaamini, alidhani ni roho mbaya zao tu.
 
SHEMEJI MTU APIGILIA MSUMARI
Wakati wazazi wakiongea hayo, shemeji mmoja wa Farida, yaani kaka wa Ally alidakia na kusema kuwa baada ya ndugu yao kwenda Kongo kikazi, Farida naye aliondoka nyumbani hapo bila kuaga na alipomtafuta kwa njia ya simu yake ya mkononi, mwanamke huyo alijibu kuwa yupo kwa mama yake mzazi, Kivule, Dar.
Msome shemeji mtu hapa: “Siku moja nikiwa katika safari zangu za usiku, nilimuona Farida akiwa na kijana anayeitwa Chidi.
“Niliamua kuwafuatilia nyendo zao kwa vile tayari tabia yake ilikuwa inajulikana. Niligundua kuwa alikuwa anaishi na kijana huyo kwenye chumba kimoja ambacho mwanamke huyo ndiye aliyekipanga. Hebu fikiria mke anapanga chumba nje ili awe anasalitia!”
Shemeji mtu huyo akaendelea kusema kuwa baada ya kukigundua chumba hicho, yeye na ndugu wengine walikwenda kwa mjumbe wa eneo hilo, Saidi Juma Mpili ambaye aliwathibitisha kuwa ni kweli Farida anaishi na Chidi japokuwa chumba kilipangishwa kwa jina la mtu mwingine.
 
MTEGO WAWEKWA
Baada ya kuthibitishiwa hivyo, familia hiyo iliwasiliana na mapaparazi kwa lengo la kuwanasa wawili hao ambao kwa muda huo walikuwa mitaani wakitanua.
Kwa ushirikiano wa familia, mapaparazi na mjumbe huyo mtego uliwekwa na baada ya muda Chidi na Farida waliwasili wakiwa kwenye pikipiki bila kujua wako ndani ya kumi na nane ya wakwe zake.
 
WABANWA LAIVU
Nje ya nyumba hiyo, wawili hao walibanwa na kuulizwa uhusiano wao ambapo Chidi alisema yeye ni kaka wa hiyari wa Farida na kukataa kwamba wanaishi pamoja, utetezi ambao uliwapandisha hasira wakwe hao na kumwomba mjumbe wapekue chumbani ili kujiridhisha kuwa hawaishi pamoja.
 
FARIDA AWAPOTOSHA WAKWE ZAKE
Farida ndiye aliyeongoza msafara wa kuingia ndani akifuatiwa na jamaa yake, lakini cha ajabu aliwapotosha ndugu wa mume kwa kuwaingiza ndani ya chumba cha mpangaji mmoja akidai ni chake, jambo ambalo lilishtukiwa na mapaparazi wetu waliokuwa wameshafanya uchunguzi wa kutosha kabla.
Farida aliambiwa chumba hicho sicho, wakamtaka aoneshe chake ndipo akaenda kuingia huko ambako zilionekana suruali aina ya ‘jeans’ za Chidi na makoti mengi ya kuendeshea bodaboda ambayo yalitoa ushahidi kuwa watu hao wanaishi pamoja humo.
 
BAADA YA UTHIBITISHO, MUME AJULISHWA KWA SIMU, ALIA
Kufuatia ushahidi huo na Farida mwenyewe kukiri, ndugu walimwendea hewani mume wa mwanamke huyo, yaani Ally na kumtumbulia siri hiyo nzito ambapo alilia kwenye simu.
 
HUENDA ILIKUWA HIVI
Katika kupashana huko, huenda kaka mtu ndiye aliyepiga simu na kusema hivi:
“Haloo dogo.”
Ally: Ee bro, shikamoo.”
“Marhaba. Nakutaarifu kuwa tumemfumania mkeo akiwa kwa kijana mwendesha bodaboda.”
Ally: Nini? Kweli bro?
Bro: Kweli dogo, hivi ninavyoongea na wewe tupo hapa, mama, mama mdogo na sista.
Ally: (kilio).
 
ALICHOKISEMA MUME
Akizungumza baada ya kupata taarifa za kubambwa  kwa mke wake na Chidi, mume wa Farida alisema akiwa nchini Kongo mkewe alimuaga anakwenda kwa mama yake Kivule na hatambui kama alikuwa amepanga chumba na kuishi na mwanaume mwingine, jambo alilosema limemshangaza sana.
Ally akaulizwa atachukua uamuzi gani baada ya tukio hilo, akajibu huku akilia na kusema atarejea Bongo kumaliza suala hilo mwenyewe kisha akakata simu huku sauti ya kilio ikimalizikia kusikika kwa mbali hali iliyowafanya ndugu zake washikwe na  huzuni.
 
FARIDA AOGOPA KUONDOKA NA WAKWE ZAKE
Baada ya tukio zima kukamilika, Farida aligoma kuondoka na wakwe zake akidai kwamba anahofia watakwenda kumpiga au kumfanyia jambo lolote baya kutokana na kitendo alichomfanyia mtoto wao, lakini akafunguka kwamba bado anampenda mumewe na hataki kupewa talaka.

AIBU:- NDOA YASAMBARATIKA KANISANI DAKIKA CHACHE KABLA YA KUIDHINISHWA



Hili  ni  tukio  la  kusikitisha, lakini  lenye  mafunzo  kibao  ndani  yake.Tukio  hilo  lilitoke  mwanzoni  mwa  mwezi wa  nane  mwaka  huu ndani  ya  kanisa  la Pentekoste  la  nchini  Kenya  ambapo  wanandoa  wawili    walikuwa  wakila  kiapo  cha  maisha  mbele  ya  mchungaji  wa  kanisa hilo.


Dakika  chache  kabla  ya  wanandoa  hao  kuapishwa  na  kuruhusiwa  kuvishana  pete, Mchungaji  wa  kanisa  hilo   aliwauliza  waumini  kama  kuna  yeyote  mwenye  pingamizi  la  kufungwa  kwa  ndoa  ya  wapenzi  hao...

Baada  ya  swali  hilo, mwanamke  mmoja  alisimama  na  kuelekea  mbele  ya  kanisa  hilo  huku  akiwa  na  vyeti  mkononi.

Alipomkaribia  mchungaji, mwanamke  huyo  alipaaza sauti  yake  na  kusema  kuwa  ndoa  hiyo  haistahili  kufungwa  kwa  sababu  yeye  na  bwana  harusi  wanamtoto  waliyemzaa  pamoja  na  kwamba  walikuwa  na  mipango  ya  kuoana....


ANGALIA VIDEO HAPA: