YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 24 September 2014

MWANAMUZIKI RAPPA MAHIRI KUTOKA NCHINI MAREKANI T.I KUSAMBAZA UPENDO NDANI YA TAMASHA LA FIESTA OKTOBA 18,2014 JIJINI DAR


 Mmoja wa Marappa mahiri kutoka nchini  Marekani atambulikae kwa jina la  Clifford Joseph Harris,'T.I' ni mmoja  wa wanamuziki watakaoangusha bonge la shoo la kusambaza upendo kwa  wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake,katika onesho la Fiesta 2014  linalotarajiwa kufanyika ndani ya
Viwanja vya Leaders Club   jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
T.I atafanya makamuzi pamoja na wasanii wengine mahiri wa hapa 
nchini,watakao pangwa kushusha bonge la burudani kwa wale  watakaobahatika kupangwa kwenye orodha ya Oktoba 18, mwaka huu jijini
Dar. 

Nguli huyo mwenye albamu nane ambazo ni I'm Serious, Trap Muzik, Urban
Legend, King, T.I. vs. T.I.P., Paper Trail, No Mercy na Trouble Man:
Heavy Is the Head ambapo nyingi kati yake zimefanya vyema katika
soko la muziki.  
T.I ameshinda tuzo tatu za Grammy tangu aanze safari yake ya muziki.  

Baadhi ya singo kali alizoachia mkali huyo na kufanya vyema ni "Bring
Em Out", "What You Know", "Big Shit Poppin' (Do It)", "Swagga Like Us"
(FT Kanye West, Jay-Z na Lil Wayne), "Dead and Gone" (FT Justin
Timberlake), "Ball" (FT Lil Wayne) na "No Mediocre" (FT Iggy Azalea).

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg