YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 4 September 2012

KAULI YA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA MWENZAO KUUAWAWA



Muda mfupi baada ya mwandishi kuuwawa.
Siku moja baada kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi wa Channel 10 kutokea kwa kulipukiwa na bomu Iringa akiwa mikononi mwa polisi waliokua wakiwatawanya wafuasi wa Chadema, waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu Tanzania wametoa kauli.
Jukwaa la wahariri Tanzania limesema limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwandishi huyo ambae alikua mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Iringa.
Jukwaa limesema tukio hilo linaiingiza Tanzania kwenye historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari kwani ni kwa mara ya kwanza inashuhudiwa mwandishi akiuwawa kazini.
Nacho chama cha waandishi wa habari Dodoma kimelaani mauaji hayo na kusema hakina tena imani na jeshi la polisi na kinahitaji tume itakayoundwa kuchunguza kifo hicho ishirikishe wanahabari, asasi za kiraia na mashirika yasiyokua ya kiserikali ili haki itendeke.
Kwenye line nyingine ni kwamba kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania kimesema kinajiandaa kulishitaki jeshi la Polisi katika Mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague Uholanzi kutokana na kuendelea kusababisha mauaji kwa raia wasio na hatia mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg