YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 4 September 2012

KILICHOMUUA DAVID MWANGOSI HIKI HAPA!!!


MAREHEMU DAVID MWANGOSI AMEUWAWA KWA BOMU LA MACHOZI

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limearifiwa kuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi ameuawa kwa bomu la machozi.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wahariri pamoja na mameneja wa vyombo vya habari yaliyoanza mkoani Morogoro jana.

Mukajanga alisema baada ya kupata taarifa za awali za kifo cha Mwangosi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa ( IPC), alilazimika kumtafuta kwa njia ya simu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.

Alisema katika mazungumzo yao, Dk Nchimbi alimfahamisha kuwa yupo nje ya nchi, Afrika Kusini kikazi na kukiri kupata taarifa za kifo hicho.

Mukajanga alinukuu mazungumzo yake na Waziri huyo kwa kusema; “Nimepata taarifa za kifo hicho na taarifa za awali zimesema ni bomu la machozi halikulipuka kitaalamu na limemuua (Mwangosi) na kuwajeruhi watu wengine wa tatu.” 

Alisema Dk Nchimbi alitoa rambirambi kwa waandishi wote wa habari nchini kutokana na kifo cha mwandishi mwenzao.

Kauli zakinzana “Hapa tunaona kauli ya Waziri inapishana na Polisi ambao wanadai amekufa kwa kupigwa na kitu kilichorushwa, wakati Waziri anadai ni bomu la machozi ambalo halikulipuka kitaalamu na kusababisha kifo na majeruhi watatu,” alisema Mukajanga.

Alisema MCT imefedheheshwa kwa kuwa mwandishi aliyeuawa, alikuwa kazini akitekeleza wajibu wake wa kukusanya habari.

Mbali ya kufedheheshwa huko, Mukajanga alisema mauaji hayo yametoa picha mbaya kwa Tanzania wakati huu ambao wajumbe wa Umoja wa Mabaraza ya Habari Duniani wapo nchini kwa ajili ya mkutano ambao Tanzania ni mwenyeji.

“Mimi ni Makamu wa Rais wa Mabaraza ya Habari Duniani, nimefedheheka sana kwa tukio hili, limefanyika wakati wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani wa mabaraza ya habari wapo hapa nchini kuhudhuria mkutano… wanakutana na vichwa vya habari kwenye magazeti na televisheni kuhusu kuuawa kwa mwandishi wa habari akiwa kazini,” alisema Mukajanga.

MCT imewataka waandishi wa habari kuchukua tahadhari ikiwemo kulindwa na Serikali wanapokuwa kazini. Alisema mauaji hayo yameandika historia mbaya na ya kwanza tangu kupata Uhuru.

“Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru mwandishi wa habari anauawa akiwa kazini kutekeleza wajibu wake ... tukio hili limetoa sura kwamba waandishi wa habari wanatakiwa kupatiwa mafunzo ya kuchukua tahadhari kwenye matukio ya hatari,“ alisema Mukajanga. HABARI NA TSN

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg