YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 2 September 2012

PRODUCER NA RAFIKI WA MR EBBO ANAETAKA KUACHIWA STUDIO YA MR EBBO.
2
Producer Jeff.
Ni zaidi ya miezi nane imepita sasa hivi toka kufariki kwa msanii Mr Ebbo ambae alifariki usiku wa kuamkia mwaka 2012 kutokana na kuugua kansa.
Jeff ambae alikua rafiki wa Ebbo kwa karibu miaka 20 pia akiwa ni Producer wake wa video kadhaa, siku chache baada ya kifo cha Ebbo ndio alikua akabidhiwe na familia ya Ebbo kuiendesha studio ya Motika iliyokua ikimilikiwa na Ebbo lakini baadae familia ikabadili huo mpango.
Baada ya hayo mabadiliko iliamuliwa kwamba studio hiyo iliyokua na makazi Tanga, sasa itahamishiwa Arusha na itasimamiwa na watu wengine.
Producer Jeff ameongea exclusive na millardayo.com na kueleza masikitiko yake kuhusu hiyo studio kutokufanya kazi mpaka sasa hivi huku bado akiwa na nia ya kuiendesha.
Hii ndio nyumba iliyokua inamilikiwa na marehemu Mr Ebbo Tanga ambapo studio iko hapohapo.
Jeff amesema hataki kulipwa wala kuchukua pesa yoyote kutokana na hiyo studio, anachotaka yeye ni kuisaidia familia ya Ebbo ambayo imebaki, wakiwemo watoto.
Namkariri akisema “kwa sasa studio imehamishiwa Arusha lakini vifaa vyote vimefungiwa stoo, mke wake Ebbo alikuja kuchukua vitu Tanga lakini hakuna kinachoendelea hata ndugu yake Ebbo aitwae Maukweli nimeongea nae anasema yule mwanamke haeleweki”
“Baba mzazi wa Mr Ebbo ndio alinikabidhi funguo za studio niisimamie kwa sababu yeye hana idea na hii kazi, nilipanga kumleta producer mkali kutoka Dar es salaam ili afanye kazi tuifufue studio… ila mpaka sasa pia niko tayari hata kama wakiamua kuileta tena kwangu, pale ambapo alikua akiishi Mr Ebbo sasa hivi pamepangwa anaishi mtu mwingine na hata chumba cha studio kimevunjwa na analala mtu sasa hivi”

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg