YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 28 July 2013

NEW MAISHA CLUB MBEYA IMETISHA, HAIJAWAHI KUTOKEA AFRICA MASHARIKI NA KATI: JIONEE HAPA: Jengo la New Club Maisha  Dar kama linavyoonekana kwa nje.
 
 Meneja mkuu wa kampuni ya Entertainment Masters LTD  Kushoto Geoffrey Ndawula. Kampuni hiyo ndio wamiliki wa Club Maisha zote Tanzania 
CONTINUE READING


  Hapa ni ramani ya picha ya wachina hao ambao wamesema kwa ndani Club hiyo itakavyoonekana.
 Sehemu ya kuchezea watu kama inavyoonekana.

 Na Livingstone Mkoi MBEYA.

 Kamapuni inayoongoza kuambukiza virusi vya burudani Tanzania ya Entertainment Masters Limited yenye makao yake makuu Jijini Dar es Salaam imeendelea kutimiza ahadi yake ya kuwafikishia watanzania burudani kila kona ya nchi baada ya kufungua Club mpya Mkoani Mbeya ambayo huenda ikafungulia msimu huu wa sikukuu ya Idd.
Mapapalazi wa Xdeejayz ambao wako kwenye ziara ya kikazi mkoani humo walijionea ujenzi wa Club hiyo mpya  inayosimamiwa na makandarasi toka nchini China na kufanikiwa kuongea na meneja mkuu wa kampuni ya burudani ya Entertainment Masters LTD Geoffrey Ndawula.
Meneja huyo aliiambia Xdeejayz kuwa" Kama tulivyoahidi kuwa azma ya kamapuni yetu ni kuwapelekea watanzania wote burudani huko huko waliko tumenza Mkoani Mtwara kwa mafanikio makubwa na sasa hivi tumetua hapa Mbeya na tutaendelea na mikoa mingine kadri Mungu atakavyotujalia" Alisema Ndawula

Aidha kiongozi huyo aliongeza kusema kwa nini wameajenga Club hiyo mkoani humo." Haya maswali mengi tunaulizwa na mashabiki wetu hasa wa mikoa mingine ambayo huduma yetu haijawafikia, lakini ni dhahili kabisa Mbeya walipaswa kujengewa club ya kisasa kwani wameteseka muda mrefu sana pia tulipokea maombi mengi sana wakihitaji Club Maisha ijengwe hapa hivyo sisi kama bodi ya ungozi wa kampuni yetu tukaamua kufanya hivyo" Alisema meneja huyo.

Hata hivyo ujenzi wa Club Misha hiyo ambao bado unandelea kwa kasi ambapo xdeejayz ilijionea wachina pamoja vibarua wakifanya kazi hiyo kwa kasi kubwa ambapo meneja huyo amesema wanajenga kwa uharaka na huenda sikukuu ya Idd wakaifungua hivyo wanambeya sasa ni zamu yao kula bata hivyo wakae kitako kwa burudani za aina yake

Meneja huyo alishindwa kutoa jengo hilo litatumia thamani ya shilingi ngapi hadi kukamilika licha ya kusema kuwa tayari hadi sasa mamilioni ya shilingi yameshatumika kwenye ujenzi huo

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg