YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 25 February 2014

BARAZA LA MTIHANI LATOA UFAFANUZI NA ALA,A NA MADARAJA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2013:




Baraza la Mitihani nchini limetoa ufafanuzi wa alama na madaraja yalivyopangwa kutokana na matokeo ya mtihani wa watahiniwa walioitimu Kidato cha Nne 2012/13 baada ya malalamiko yaliyotokana na mkanganyiko wa utaratibu huo mpya ambao haukuwepo katika miaka ya nyuma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde amesema utaratibu huo umelenga kupunguza mlundikano wa alama katika kundi moja.
Sasa katika makundi yetu haya saba, kama nilivyotangulia kusema, ni gredi D ndiyo ufaulu. Kama mtahiniwa alipata gredi D na kuendelea, atakuwa amefaulu. Mtahiniwa katika somo,
 akipata gredi D na F, atahesabiwa kuwa ameshindwa somo husika.

Sasa mtahiniwa huyu anahesabiwa vipi kufaulu kwa ujumla wake mtihani?

Amefanya masomo mbalimbali tunampangaje katika madaraja?

Madaraja ya ufaulu, yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20, kifungu kidogo 1 – 6 cha Kanuni za Mitihani, kinachoelekeza kuwa, Ufaulu katika daraja la I – III upangwe kwa kuzingatia idadi ya alama, yaani points, na ufaulu katika daraja la IV unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini alioupata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au kwa kiwango kisichokuwa chini ya gredi C katika somo moja.
Aidha Dk Msonde amesema sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi kwa kutumia mfumo huo mpya wa madaraja, utatolewa na mamlaka husika, ambapo Kamishana wa Elimu ndiye mwenye mamlaka ya kulitolea ufafanuzi.
----------------

UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013

Baraza la Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:-
1.  Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012.
Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.
Jedwali Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.
Kundi
Gredi
Alama
Idadi ya Pointi
1
A
75 - 100
1
2
B+
60 - 74
2
3
B
50 - 59
3
4
C
40 - 49
4
5
D
30 - 39
5
6
E
20 - 29
6
7
F
0 -  19
7
Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili (12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.
2.  Kwa kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.
3.  Madaraja ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu katika Daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2.

Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013

4. Kwa mujibu wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za kufeli.
5. Baraza la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
25 Februari, 2014

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg