YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 27 August 2014

AVUNJA REKODI KIJANA AUVUA NGUO KILELENI MLIMA KILIMANJARO.

KIJANA AVUA NGUO ZOTE NA KUBAKI MTUPU BAADA YA KUFIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO


 
KIJANA Ben Boleyn aliamua kuvua nguo baada ya kufika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini chenye joto la kati ya sentigrade 10 hadi 12.

Ben Boleyn akiwa kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Ben alifanya hivyo baada ya kuwekeana dau la shilingi 500 na mwenzake miongoni mwa aliopanda nao mlima huo.


Ben akivua nguo baada ya kuwekeana dau na mwenzake.

Kijana huyo mwenye miaka 18 alipanda mlima huo katika kuchangisha fedha kusaidia watoto wa kituo cha kulea watoto cha Acorns Children's Hospice kilichopo jijini Worcester nchini England.

Kwa kupanda mlima huo, Ben alikusanya pauni 600 ila baada ya kuvua nguo zake na kuweka picha yake mitandaoni alichangisha fedha nyingi zaidi.

Ben baada ya kuvua nguo. Ben ambaye hujitolea katika kituo hicho alipanda futi 19,341 za Mlima Kilimanjaro kwa siku 9 akiwa na wenzake 7.
Ben ambaye ni mwenyeji wa Kingswinford, England alisema: Kila mtu alifurahia kitendo nilichokifanya katika kilele cha Mlima Kilimanjaro na kuchukua picha zangu

Wazazi wangu walipigwa na mshangao mwanzoni, ila walipoona watu wanazidi kuchangia kwa wingi walinielewa maana nilifanya kitu tofauti.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg