YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday 6 August 2018

MH. RAISI MAGUFULI AWEZESHA MZEE KIMWELI DAFA KUSHEREHEKEA MIAKA 100 NDANI YA NDEGE YA DREAMLINER.

Mzee Kimweri Dafa na mwanawe Wakili Imam Dafa ndani ya ndege
Image captionMzee Kimweri Dafa na mwanawe Wakili Imam Dafa ndani ya ndege
Mzee wa miaka 100 amesherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa kusafiri na ndege kwa mara ya kwanza, kama zawadi aliyopewa na mtoto wake.
Akizungumza na BBC ndani ya ndege, huku jicho akilitupa dirishani mara kwa mara kupata mandhari nzuri ya anga, kwa sauti ya utulivu bila ya woga, mzee Kimweri Dafa Kivo amesema anasikia furaha kutokana na kuwa ni mara yake ya kwanza.
Isitoshe, amekuwa miongoni mwa Watanzania wa mwanzo mwanzo walioabiri ndege mpya iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na kupokelewa mwezi uliopita.
''Mwanangu namshukuru sana kwa sababu aameweza kunipandisha kwenye ndege, nimefurahi sana..'' amesisitiza mzee Kimweri.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg