YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 1 September 2012

MANENO 99 ALIYOSEMA MWIMBAJI MARLAW KUHUSU HIKI KILICHOANDIKWA NA GAZETI KWAMBA AMESHINDWA KUZAA.
5
.
Katika gazeti kubwa la burudani Tanzania la Baabkubwa lililotoka hivi karibuni ambalo husomwa na wabongo wengi wanaopenda stori za burudani kiliandikwa kichwa cha habari kwamba Marlaw ameshindwa kabisa kumpa mimba mkewe Besta ambae ni msanii pia.
Kutokana na hilo Marlaw aliomba namba kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM ili kukanusha hizo taarifa.
.
Namkariri akisema “swala la mimi kumpatia mimba mke wangu au uzao wa familia yangu ni swala langu binafsi, sidhani kama ni swala la Baabkubwa, mi sijapenda alafu na dizaini walivyoelezea yani ile interview mimi ninavyozungumza yale sio maneno yangu”
Kwenye line nyingine amesisitiza kwamba “kama walinipigia simu basi ningependa kama wangeandika kile hasa ambacho hasa mimi nimekisema, nakumbuka walishawahi kunipigia simu lakini tukazungumza lakini mazungumzo hayakua vile jinsi ilivyokuja kuandikwa, yamebadilishwa”
“sitochukua hatua yoyote nataka tu wanipigie simu waniambie samahani, mtu ataenipigia simu anipigie tu tumalize tuongee tu yaishe, kama wangependa kuandika kwenye gazeti lijalo waandike kile nilikiongea”
Baada ya hayo nilipochek na Baabkubwa walikua kwenye kikao lakini wakasema time ikifika msemaji atazungumza.
Msikilize Marlaw hapo chini akiongea…

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg