YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 1 September 2012

MOVIE ZILIZOONGOZA KWA KUTAZAMWA CINEMA DAR ES SALAAM WIKI HII


.

0
Paul White akitoa info kwa Millard Ayo.
Kama upo Dar es salaam mkoa pekee wenye kumbi nyingi za cinema kuliko mkoa wowote Tanzania, nimepata details za movie iliyoongoza kwa kutazamwa kuliko zote wiki hii.
Expendables 2 ambayo inawahusisha mastaa wa zamani wa movie za Action kama Rambo,Arnold Schwarzenegger, Dolph, Van Damme, Chuk Norris, Jet Li na wengine, ndio imeshika namba one kwa kutazamwa sana.
Expendables 2 ilifanya watu kukosa ticket kwa siku kadhaa mpaka ikabidi ihamishiwe kwenye ukumbi mkubwa zaidi kati ya kumbi za Cinema Mlimani City.
Movie ya pili ambayo imetazamwa sana pia ni Step up revolution.
Najua hii movie mpya ya Expendables 2 inaweza kuchelewa kidogo kuwafikia watu wangu wa Tandika, Mbagala, Mtoni, Ngarasero Usa river Arusha, Mabatini Mwanza, Chumbageni Tanga na sehemu nyingine Tanzania ambako huwa tunatazama movie kwenye vibanda umiza kwa kulipia shilingi 100 mpaka 200 kwa movie moja.
Sababu kubwa ya hii movie kuchelewa kufika kwenye hivyo vijiwe vyetu ni kwamba ni lazima kwanza itafsiriwe, watu wangu wa hizo area hawatakubali kuingia kuichek kama haijatafsiriwa na Dj Mac kwanza.
Kitu kingine ambacho hukifahamu, ni kwamba movie kama hii ya expendables ambayo wameact waigizaji wa zamani kama kina Arnold Schwarzenegger inakuza vipato vya watanzania wengi wanaofanya hiyo biashara ya kuonyesha movie kwa sababu bado kwenye hayo maeneo watu wanaamini kwamba waigizaji wa zamani moto wao ni mkali.
Amour ambae ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda umiza Dar es salaam anasema movie za watu wa zamani kama hizi anaweza kuzionyesha kwa zaidi ya mara hata tatu kwa siku na bado watu watajaa, hasa wale fans ambao wamekua wakifatilia movie toka kitambo.No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg