YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 10 March 2013

TAARIFA KAMILI KUHUSU WALIOKAMATWA KWA KUMTUMIA MSG ZA MATUSI SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA

0
.
Picha ya liblary.
Kutokana na ile ishu ya watu kumtukana spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda baada ya namba yake kudaiwa kutajwa hadharani na viongozi wa Chadema, watu watatu wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kuhusika.
Hao watu ni kutoka mikoa ya Dodoma, Simiyu na Kilimanjaro ambapo wanatuhumiwa kutumia lugha chafu za matusi na uchochezi dhidi ya spika.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Assah Mwambene amesema wawili walikamatwa kwa tuhuma za kumtumia spika msg za matusi, mmoja aliebaki alikamatwa na DVD yenye picha ya kuhamasisha lugha za matusi kwa spika.
.
Spika Anne Makinda bungeni.
Mwezi uliopita spika Anne Makinda alipokea msg zisizopungua 400 kwenye simu yake ya mkononi pamoja na kupokea simu mbalimbali za matusi baada ya namba yake kudaiwa kutajwa hadharani kwenye mkutano wa CHADEMA.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg