YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday, 14 March 2013

HUYU NDIO BALOZI ALIERUDISHWA NYUMBANI BAADA YA KUDAIWA KUTEMBEA BILA NGUO MWILINI.

0
.
.
Lassy Chiwayo ambae ni balozi wa Afrika Kusini nchini China, amerudishwa nyumbani baada ya mkataba wake kukatishwa kutokana na kukumbwa na kile kinachodaiwa kuwa matatizo ya kiafya.
Gazeti la Daily Teleghraph limeripoti kwamba moja kati ya sababu kubwa ni tatizo kwenye akili yake ambapo inadaiwa balozi huyo ilifikia mpaka kutembea mtaani bila nguo.
Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba balozi huyo alikua na mtindo wa kupotea nyumbani huko China alikokua anaishi, alikua anapotea kwa siku kadhaa alafu baadae anakuja kukutwa akiwa mtupu bila nguo.
Lassy mwenye umri wa miaka 44 akiwa ni mmoja wa watu wa karibu ambao waliwahi kufungwa gereza moja na rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, amekanusha taarifa zake za kuwa na matatizo ya akili pamoja na kutembea uchi, akisema hayo yote ni mambo mapya kuyasikia.
Imeripotiwa kwamba Lassy ambae ni baba wa watoto watatu amekumbwa na mfululizo wa matukio hivi karibuni ambapo la mwisho linalokumbukwa ni moto kulipuka nyumbani kwake na kuteketeza mali kama gari la kifahari la Porsche, quad bike na mali nyingine.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg