YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 9 June 2013

M2 The P – Sijui ni nini kilichotutokea

Picha ya marehemu M2 the P na Ngwair, waliyopiga usiku wa dhahama
Picha ya M2 the P na Marehem Ngwair, waliyopiga usiku wa dhahama
Msanii ‘M2 the P’ ambaye alikuwa na marehemu Albert “Ngwair” Mangweha nchini Afrika Kusini wakati rapper huyo anafariki na yeye kuzidiwa hadi kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, afunguka kuhusu yaliyowakuta yeye na marehemu Ngwea

‘M2 the P’ ambaye awali naye aliripotiwa kuwa amefariki kabla ya taarifa hizo kukanushwa, alisema jana kuwa hadi sasa hajui nini kiliwatokea.

Msanii huyo alisema kwamba hakumbuki kilichotokea hadi wakazidiwa na kukimbizwa hospitali wakiwa hawajitambui. Alisema pia bado anajisikia anaumwa hadi sasa licha ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya St. Hellen Joseph ya Afrika Kusini alikokuwa amelazwa. 

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg