YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 15 June 2013

MAMA WEMA SEPETU ATISHIA KUMCHOMA MTU KISU KISA MWANAE...
VIDEO inayomuonesha mama wa Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu akizua timbwili ‘hevi’ nyumbani kwa mwanaye huyo huku akitishia kumchoma mtu kisu imevuja, Ijumaa limeinasa.

Kwa mujibu wa video hiyo, mama Wema alitimba nyumbani kwa mwanaye huyo Kijitonyama, Dar kwa lengo la kuwasambaratisha marafiki wanafiki wa Wema ambao alidai wanamharibu mwanaye.
Pamoja na matusi yanayosikika kwenye video hiyo, mzazi huyo alikuwa akitoa vitisho kwa Maila ambaye ni mmoja wa mashosti wa karibu wa Wema.

“Nitammaliza huyu…(tusi), hana kwao, hana chochote,” sauti ya mama Wema inasikika na kuongeza:
“Nina data, mimi nilipigiwa simu, huyu sijui Maila, sijui nani kuwa alishikwa na begi lenye vipisi vya bangi Airport (uwanja wa ndege).
“Hawamshauri Wema chochote, wanamharibu ili maisha yake achanganyikiwe. Ningekuwa na kisu ningemchoma…ningekuwa na kisu leo ningemchoma visu…potelea mbali.”

Mbali na vitisho hivyo, mama Wema anaonekana akibinua vitu vya ndani kama makabati na makochi ikidaiwa kuwa alikuwa akisaka bangi aliyoletewa mwanaye na rafiki zake.

Kwa mujibu wa watu walioiona video hiyo walisema marafiki wa Wema kama Kajala Masanja, Snura Mushi, Martin Kadinda, Jamila na wengine kibao wanapaswa kuwa makini na mama huyo kwani anaonekana kuwa na hasira nao.

Baada ya kuinasa video hiyo, Ijumaa lilimsaka mama Wema ili kupata mzani wa habari hiyo lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Mwandishi Wetu alikwenda nyumbani kwa mama huyo Sinza-Mori, Dar ili kuzungumza naye ‘laivu’ lakini alipogonga tu getini alitokea binti aliyedai mama Wema hakuwepo.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg