YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 17 August 2014

KIJANA AGONGANISHA MADEMU MAARUFU. HIVI NDIVYO ILIVYOKUA

KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Yona Nathal, mkazi wa Ubungo ya River Side jijini Dar es Salaam, Jumanne iliyopita alijikuta katika timbwili zito na kundi la washereheshaji maarufu wa kike Dar ‘ma -MC’ baada ya kubainika kuwachanganya kimapenzi. 
Yona Nathal akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
 AWEKEWA MTEGO
Ilidaiwa kuwa Yona ameshawatokea baadhi ya ma-MC  hao kwa nyakati tofauti na kula nao raha kwa siri lakini siku moja wakajuana na kusambaziana taarifa.

 Inazidi kudaiwa kuwa, kwa vile habari zake zilishasambaa kwenye umoja wa ma- MC hao, hivyo waliweka azimio la kumnasa kwa sababu aliibuka tena na kumtongoza MC mmoja ambaye pia ni mke wa mtu (jina tunalo).
 MC huyo alikubaliana na Yona wakutane kwenye Hoteli ya Legho iliyopo Shekilango, Ubungo jijini Dar ambapo ma- MC wa kike na wa kiume walikusanyika kwa ajili ya kumtia mikononi kijana huyo waliyedai anawadhalilisha.
Akijitetea baada ya kunaswa.
 KIDUME ANASWA
Ilikuwa saa mbili usiku, Yona alishuka kwenye daladala akiwa ametinga suruali nyeusi ya kitambaa, shati jeupe na miguuni amevaa kandambili nyekundu aina ya bata.

Baada ya kushuka alimpigia simu MC mwenye ahadi naye ambaye naye alimwambia ameshafika Legho. Walipokutana uso kwa uso Yona  alimuomba ‘amuhagi’ MC huyo lakini cha kushangaza, akajikuta amezungukwa na kundi la ma- MC wengine ambao walianza kumzodoa wakimwambia ana tabia chafu ya kuwadhalilisha.
“Jamani naomba mnisamehe sana, mimi sina nia mbaya na hawa ma- MC ni maneno yakeYona Nathal.
 Ilikuwa mbilinge kubwa, ikabidi Yona awe mpole baada ya kutaitiwa ambapo aliomba msamaha huku akisema hakuwa na nia mbaya ila ana hisia kali za mapenzi na ma-MC wa kike hususan  wakati wakiwafunda maharusi kwenye kitchen party.
 “Jamani naomba mnisamehe sana, mimi sina nia mbaya na hawa ma- MC wa kike, hisia zangu ndizo zilizoniponza. Navutiwa nao sana,” alisema kijana huyo.
Wakati akihojiwa,  kijana huyo aliwataja ma -MC wengine zaidi ya sita maarufu hapa ambao ni wake za watu na kukiri kuwa ameshakula nao ‘mambo matamu’.

 HASIRA ZAIDI
Maneno hayo yalipandisha hasira za ma-MC hao ambapo walitaka kumpa kichapo lakini ghafla walitokea askari wa Kituo cha Polisi Urafiki-Ubungo, Dar na kumuokoa kisha kumpeleka kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Ndani ya kituo hicho cha polisi, Yona alifunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. URP/RB/6607/2014 UCHUNGUZI.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg