YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday, 17 August 2014

WASTARA APIGWA MKWARA ASIENDELEE NA SHUGHULI ZAKE ZA MUVI

Mkwara mbuzi! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya njemba mmoja ambaye hakufahamika kujitokeza na kumpiga mkwara asiendelee na shughuli za uzinduzi wa filamu yake.
Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma Wastara akizindua filamu yake ya Last Decision.
Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita wakati Wastara akizindua filamu yake ya Last Decision katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar.
Njemba iliyodai kuwa ni Afisa Mtendaji katika maeneo ya Mbagala-Zakhem, Dar akijaribu kumzuia Wastara katika uzinduzi huo.
Staa huyo alipofika maeneo ya Mbagala-Zakhem, Dar ndipo njemba huyo alipojitokeza na kumtaiti Wastara akidai yeye ni Afisa Mtendaji hivyo waondoke eneo hilo.
Hata hivyo, Wastara alionesha vibali vya kufanya shughuli hiyo ndipo njemba huyo alipotaitiwa na wananchi na kuambiwa achukue taimu.
Uzinduzi wa filamu ukiendelea kama kawaida.
“Jamani hata sielewi kibali nimeshalipia na ninacho lakini angalia huyu baba ametuharibia siku wakati mimi nimeamua kufanya uzinduzi wa tofauti mitaani na si kwenye kumbi kama wengine,” alisema Wastara.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg