YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday, 20 August 2014

BREAKING NEWS!!! TANESCO KAGERA YAKAMILISHA MIPANGO YA KUFIKISHA UMEME KWA VIJIJI 400 MKOANI HUMO.


Meneja TANESCO KAGERA mhandisi Martine Madulu akieleza jinsi mradi huo unavyokamilishwa

Transformer mpya yenye MVA15
Transformer ya zamani inayotumika sasa yenye MVA5
Mtaalamu kutoka makao makuu Tanesco Dar es salaam anayefunga Transformer hiyo Bwana AMON GAMBA, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu.
Fundi msaidizi kulia akiendelea kukunjua waya unaotumika kuweka mawasiliano ya umeme katika transformer hiyo mpya.
Mwonekano wa Transformer mpya ya kufua umeme kwa MVA15.


Meneja wa shirika hilo mkoa wa kagera mhandisi MARTINE MADULU akiongea na waandishi wa habari, amesema wananchi mkoani kagera wanatarajiwa kuondokana na kukatikakatika kwa umeme kutokana na kufungwa transfoma  mpya ya kusambaza umeme katika mkoa wa kagera.

Bwana madulu amesema kuwa serikali imeamua kufanya kuleta transfoma hiyo mpya iliyogharimu zaidi ya bilioni 1.4 kutokana na kuongezeka kwa wateja na kusababisha transfoma iliyokuwepo kushindwa kutoa huduma iliyokuwa inahitajika.

Mhandisi madulu ameongeza kuwa  taransfoma hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya elfu 22 wa mkoa wa kagera kuliko hii ambayo ilikuwepo.

Pia amewataka wananchi kuendelea jkushirikiana na tanesco katika kutoa taarifa kwa wanahoujumu miundo mbinu ya shirika hilo.
  

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg