YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday 1 September 2014

KIFO CHA BETTY NDEJEMBI NA MATUKIO YAKE.

Unyanyasaji Mtandano + Kifo cha Betty Ndejembi, nani wa kumnyooshea kidole?

posted 2 days ago by admin
Imeandikwa na Malisa Godlisten
Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakubadilishi ukweli kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani. Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi watu wamesema mengi, na yameandikwa mengi. Kila mmoja kwa namna alivyoguswa. Zitto kabwe ametweet hivi asubuhi “justice for bett”, akitoa rai haki ipatikane kwenye kifo cha Betty.
Marehemu Betty Ndejembi
Jokate Mwegelo naye ametweet kuomba msaada wa kuchunguza kifo cha Betty. Na watu wengine maarufu kila mmoja kasema neno, labda kwa sababu Betty alikuwa maarufu in one way or another. Lakini hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake, alinyanyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo chake, lakini mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha fulani. Saa chache kabla ya kifo chake Betty alitweet, “ITS ALWAYS THE PEOPLE YOU TRUST WILL DO THEOST DAMAGE TO YOU...ITS BEEN A GOOD LIFE THO”
Baada ya kutweet hakuonekana tena hadi alipookotwa mtaroni kesho yake asubuhi akiwa amefanyia vitendo vya kikatili na akiwa amepoteza fahamu.
Lakini kabla hata ya kutweet hivyo, Betty alikuwa anaandamwa sana mtandaoni huko Twitter. Kuna watu walianzisha team ya kumtukana, kumjibu hovyo na kumprovoke kwa kila alilofanya. Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu kwa Betty kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususani cha mtu maarufu. Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni.
Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki. Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa kujifanya askari jkt, kusengenya na kupost majungu…. Aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza
Kwenye hii mitandao, matusi imekuwa njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye ‘umaarufu’ huko twitter, facebook na instagram lakini ukidadisi chanzo cha ‘umaarufu’ huo, utaambiwa ‘ah huyu ana matusi si mchezo’. Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu Betty ni victim wa yote hayo.
Alitukanwa sana, na aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti.
Kuna waliomwita Di maria, superstar uchwara etc.. and I hope hao waliomuita hivyo wanajifahamu na wengine wananisoma hapa. Japo sijui chanzo cha ‘ugomvi’ wao, lakini naamini kuna watu wengi tu waliokuwa katika nafasi ya kuzima moto huo kwa vile walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za ‘ugomvi’ husika lakini kwa sababu ya unafiki wakapalilia moto maana wanafurahi watu wakigombana.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki. Watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake.
Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa kwamba ‘wakati’ muafaka wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.’ Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali. Mojawapo ya tweet za mwishomwisho za marehemu alisema hivi.
‘Thank you all for the names  I was called, luck y’all have such a perfect life.! No hard feelings.. I’m alive still.! Endeleeni kuongea.’
 Kwa tafsiri isiyo rasmi Betty alisema, ‘asanteni kwa majina yote mliyoniita. Mmebarikiwa kuwa na maisha mazuri.! Hamuumizwi na hisia kama mimi. Ila bado ninaishi, endeleeni kuongea.’
Kwa bahati mbaya hakuna aliyejali, hadi juzi asubuhi (Jumatano) Betty alipookotwa kwenye mtaro akiwa amefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na akiwa amepoteza fahamu. Kifo cha Betty ni miongoni mwa vifo vya kikatili sana kuwahi kutokea nchini. Nashauri wanaharakati ea haki za wanawake wapambane kuhakikisha haki inapatikana.
Akina Annanilea Nkya, Hellen Kijobisimba watafute haki ya binti huyu kama Zitto Kabwe alivyosema ‘justice for betty’, imagine mtu aliyekua kwenye maumivu makali ya hisia, anatekwa na genge la wahuni. Bila kujali kipindi kigumu alichokua anapitia, bila kujali hakua na wazazi, bila kujali psychological torture aliyokua nayo still wanamfanyia unyanyasaji wa kijinsia hadi anapoteza fahamu.
Betty aliokotwa mtaroni na kupelekwa hospitali. Jana (Alhamisi) aliweza kufungua macho, lakini hakuweza kuongea lolote hadi saa 3 usiku wa kuamkia leo, mauti ilipomkuta. Kwaheri betty, kwaheri classmate wangu (Majengo sec). Kwaheri rafiki, kwaheri ndugu. Umeondoka dunia bado inakuhitaji. Naumia you have gone too young, lakini naumia zaidi sababu umekufa kikatili mno.
Japo sijui nitakufaje, lakini nadiriki kusema hukustahili kifo cha aina hii. Nakumbuka sms yako ya mwisho kwangu uliniambia hivi, ‘Malisa blv me, only youths can change this country.’ Leo nilipopata taarifa ya kifo chako nimerudia kuisoma sms yako mara mbilimbili.
Sikujua kuwa sms hiyo ndo ulikua unaniaga. Umeniaga kwa kutuachia vijana wosia, kuwa vijana pekee ndio wenye uwezo wa kuibadilisha nchi hii. Nitakua nimekusaliti ikiwa sitautendea kazi wosia huu. I promise to fight and motivate other youths to liberate this country for your dedication. Umekwenda kumfuata mama yako, umemfuata baba yako. Wazazi wako walitangulia, leo wewe umewafuata. Hatimaye familia nzima mmekutana Paradiso.
Huu ni baadhi ya ujumbe uliondikwa na watu mbalimbali waliokuwa wakimfahamu Betty:
Faraja Nyalandu:
Kifo cha Betty kimetuachia mafundisho mengi. Natumai kila mmoja aliyemfahamu Betty kwa namna moja ama nyingine amepata lake la kujifunza. Gharama ya mafundisho tuliyoyapata ni kubwa sana. Maumivu. Kifo. Aliyelipa ni Betty na wanaompenda. Itafaa gharama hii isiende bure. Tuwe wakarimu. Tuwe na upendo. Tumshike mtu mkono pale alipo na uhitaji. Tumnyanyue akianguka. Lakini vyote haviwezi kuwa kama ndani yetu havipo. Huwezi kutoa ambacho huna. Tuanze ndani yetu. Betty tusamehe. Mungu atusamehe na Mungu atusaidie. Pumzika kwa amani Betty

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg