YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 2 September 2014

SAKATA LA MKE WA KAMANDA BARLOW, MAPYA YAIBUKA!Sakata la madai kuwa mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, Stella Barlow (pichani)alitimuliwa ukweni kwa mapanga limechukua sura mpya baada ya ndugu wa mumewe kuibuka na kutoa ufafanuzi.
Mjane Stell Barlow wakati wa mazishi ya aliyekuwa mume wake, Kamanda Liberatus Barlow.
 Akizungumza kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita, ndugu wa marehemu Kamanda Barlow, aliyejitambulisha kwa jina moja la Lyimo alisema si kweli hata kidogo kuwa walimkimbiza kwa mapanga shemeji yao huyo. 
“Kilichotokea ni kwamba tulimuambia huyo mama kuwa hawezi kufanya chochote kwenye kaburi la mumewe mpaka akamuone kiongozi wa ukoo. Kimila tangu wakati kaburi linachimbwa, linakuwa chini ya uangalizi wa wanaume na hata baada ya kuzika haliwezi kuwa chini ya mwanamke, hilo tulimjulisha,” alisema Lyimo.
Kamanda Barlow enzi za uhai wake.
 Alifafanua kuwa wamewahi kufanya misa ya kumuombea marehemu Barlow na ndugu wengine na mama huyo aliarifiwa lakini hakuja. “Ujumbe wetu ni kwamba muambieni huyo mama  kuwa siyo vizuri kuchafua ukoo kwa sababu hatuna ugomvi naye na hakika kama ni wa kulaumiwa ni yeye siyo sisi wana ukoo,” alisema Lyimo.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg