YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 4 September 2014

NYUMBA ZA ASKARI NA KITUO CHA POLISI VYABOMOLEWA, HUKU FFU WAKISIMAMIA ZOEZI...NYUKI WA AJABU WATIBUA ZOEZI


Ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi (OCD) pamoja na nyumba za makazi ya askari polisi vimebomolewa na kampuni inayojenga barabara hiyo China Henan International Group (CHICO) ndiyo iliyoendesha zoezi hilo la bomoabomoa chini ya usimamizi wa F.F.U baada ya maaskari polisi kudaiwa kugoma kuhama.

Katika hali ya kushangaza na iliyowaacha vinywa wazi wananchi, askari wa kutuliza ghasia F.F.U wamesimamia zoezi la kubomoa kituo cha polisi cha wilaya pamoja na nyumba wanazoishi askari polisi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kupisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 59.1 toka Kyaka wilayani Missenyi hadi Bugene wilayani Karagwe kwa kiwango cha lami.

Ni tukio lililovuta umakini wa watu wengi huku minong'ono ikitawala ya ukosoaji wa kauli ya polisi "Utii wa sheria bila shuruti", wakihoji maana yake kwani nao (polisi) wamekaidi kutii sheria hadi kuletewa F.F.U kuwashughulikia endapo wangejaribu kuleta fujo.
Meneja wa TANROADS mkoa wa Kagera John Kalupare alipopigiwa simu kuelezea tukio hilo amesema yupo safarini Dar es Salaam na asingeweza kuzungumzia suala hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe alipopigiwa simu juu ya tatizo hilo, simu yake imeita bila kupokelewa.
Mmoja wa maofisa wa TANROADS aliyekuwa anasimamia zoezi hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe, amesema kuwa wao wanaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao.

Sisi TANROADS tunaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao na kituo chao hivyo waulize wao kwanini ubomoaji unafanywa chini ya ulinzi mkali amesema.

Hata hivyo zoezi hilo limeingiwa na dosari baada ya kundi la nyuki kutokea na kuwashambulia wabomoaji, maaskari na mashuhuda wa tukio hilo huku dereva akilazimishwa na wachina kuendelea na ubomoaji licha ya kung'atwa na nyuki hao.
Ni tukio linaloshangaza na kuitia doa serikali kwa jeshi la polisi lenye dhamana ya kulinda usalama na raia ambalo daima huhubiria raia utii wa sheria bila shuruti sasa linaenda kinyume hadi kuletewa F.F.U kulisimamia.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya Karagwe hakupatikana kuzungumzia sakata hilo ambapo inadaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itaigharimu halmashauri hiyo baadhi ya ofisi zitakazobomolewa ikiwemo ofisi za wabunge wa majimbo ya Karagwe na Kyerwa.
Chanzo: Malunde1 Blog

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg