YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 4 September 2014

MCHINA ACHEZEA KICHAPO NI BAADA YA KUTAKA KULAZIMISHA PENZI KWA MWANADADA


Mchina akichezea kichapo kwa kumshika mke wa mtu maziwa mjini Iringa 
RAIA mmoja wa Kichina ambae jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayesadikika kuwa ni mmoja kati ya mafundi katika ghorofa moja mjini Iringa amejikuta akichezea kichapo kutoka kwa njemba mmoja ambae alikuwa ameongozana na mke wake baada ya mchina huyo kumshika maziwa mwanamke huyo akimtaka mapenzi mbele ya mumewe.

Tukio hilo lililofananishwa na udhalilishaji kwa wanawake lilitokea jana majira ya saa 2 usiku katika eneo la stendi ya daladala za Mkwawa kata ya Miyomboni mjini Iringa.

Kutokana na kitendo hicho cha aibu alichokifanya mchina huyo mume wa mwanamke huyo alikosa uvumilivu na bila kujali kuwa wachina ni wataalam wa kareti alimvaa mchina huyo na kumpiga mtama uliopelekea kuanguka chini na kuwafanya vijana wapiga debe eneo hilo kuanza kumshambulia kwa kichapo bora mradi wamepigana na mchina.

Vijana wakimpa kichapo mchina huyo 
Mashuhuda wa tukio hilo waliueleza mtandao huu wa matukiodaima.co.tz uliofika kwa wakati eneo la tukio kuwa mchina huyo alikuwa akitoka katika eneo la jengo wanalolijenga lililopo jirani na stendi hiyo na baaada ya kufika eneo hilo la Stendi alikuta watu wengi wakiwa wanasubiri usafiri wa daladala kwenda Mkwawa na Ilala na bila aibu mchina huyo alimsogelea mwanamke huyo ambae pembeni alikuwa na mume wake na kumshika maziwa yake mfano wa kumtaka penzi kwa nguvu jambo ambalo lilimfanya mwanamke huyo kupiga kelele huku mchina huyo akimsemesha kichina ambacho hakuna aliyejua anazungumza nini zaidi ya kutambua ishara za mikono ambazo mchina huyo alikuwa akionyesha kuashiria kumwita.


Hapa akionyesha eneo lake la kazi 
Kichapo kikali alichokipata mchina huyo ambae muda wote alikuwa akilalamika kwa kilio cha kichina ilimfanya mmoja kati ya askari anayeendesha biashara zake eneo hilo anayetambulika kwa jina moja la Rashid kufika kunusuru ugomvi huyo na baada ya kutamkiwa Polisi mchina huyo alipiga magoti na kuonyesha ishara za kutubu kosa na askari huyo alisikika akisema umefanya kosa huwezi mshika mwanamke maziwa hadharani na kuachiwa .

Hata hivyo imedaiwa kuwa ni tabia ya mchina huyo na wenzake wanaofanya kazi katika jengo hilo kunyanyasa wanawake na kuwavunjia heshima zao mbele ya hadhara kiasi cha baasi na maeneo ya pombe vidanda vya UVCCM kiasi cha kupigwa marufuku kuingia katika baadhi ya vibanda.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg