YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 10 October 2012

HUU NDIO UNYAMA ALIONIFANYIA MKE WANGU:


“Mimi ni dereva wa daladala linalofanya safari Mwenge na Temeka, Septemba 28, mwaka huu sikuweza kurudi nyumbani baada ya basi hilo kuharibika. Kutokana na tatizo hilo, nilishindwa kuliacha barabarani ndipo nilimtumia ujumbe mke wangu kumuarifu.

“Niliporudi  nyumbani asubuhi nilikumbana na maswali mengi kutoka kwa mke wangu, kisha akaingia jikoni na kunyanyua surufia iliyokuwa na uji akanimwagia usoni, ukaniunguza vibaya sana.

“Baada kufanyiwa unyama huo nilipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo wasamaria walikuja na kunipeleka Hospitali ya Temeke ambako nililazwa.

“Kabla ya tukio hilo tumekuwa tukizozana mara kwa mara na hata kutishia maisha yangu lakini nashindwa kuachana naye kwa kuwa nimezaanaye,” alilalamika Mlewa.
 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,  ACP David Misiime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mama huyo ameshakamatwa na upelelezi unaendelea.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg