YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 9 October 2012

TAARIFA ZIKUFIKIE KWAMBA HIZI NDIO PICHA 5 ZA EXCLUSIVE INTERVIEW YA CLOUDS FM/ TV CHOICE FM NA RICK ROSS DSM PAMOJA NA ALIYOYASEMA.Rick Ross.
Millard Ayo, Rozay na Vanessa Mdee.
.
.
.
Kupitia AMPLIFAYA ya Clouds Fm inayokua OnAiR kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa moja usiku, jana October 8 2012 ilisikika sehemu ya Exclusive Interview ya rapper Rick Ross kutoka kwa Obama ambae aliperform kwenye Serengeti Fiesta 2012.
Japo alisafiri safari ndefu ya masaa 25 alikua hajui atakuja kukutana na nini ila alikua na kumbukumbu tu za utotoni kuhusu Tanzania, mfano mlima Kilimanjaro na mengine ila ameenjoy na atarudi anytime.
Moja ya mambo ambayo huyafahamu, Ross alitaka kwenda kwenye mbuga za Wanyama lakini muda ulikosekana, pia anasema alifurahia kuona performance ya wasanii kadhaa wa bongo waliotangulia kuperform kabla yake japo alikua haelewi.
Kuhusu jina la album yake mpya ya God forgives, I don’t yani Mungu anasemehe, mimi sisamehe , namkariri Rozay akisema “kwa mtu ambae ananielewa tangu utotoni, na anaejua niliyoyapitia maishani anajua vizuri kabisa kwamba Rick Ross namjua Mungu na kumuamini, ila kuna vitu huwa vinafanyika maishani na huwa haviko mikononi mwako tena, nilitaka kuifanya hii album kama Cinema, maisha ya kila siku na nadhani niliitendea haki, nilitaka iwe stori midomoni mwa watu”
Unaweza kusikiliza sehemu ya interview yake hapo chini...

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg