YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 12 October 2012

WANACHUO WANNE WALIVYOUWAWA KIKATILI KIMAKOSA WAKISHUTUMIWA KWA WIZI.Wanafunzi wanne wa chuo wameuwawa kikatili kwa kupigwa na kuchomwa moto hadharani kwenye kijiji cha Aluu Nigeria kilichokaribu na chuo chao kwa tuhuma za wizi wa laptops na simu kitu ambacho inaaminika hawakukifanya.

Waliamua kuungana na kuanza kuishi kwenye kijiji hicho kutokana na kutoridhishwa na mazingira ya hostel za chuo, wakiwa marafiki wanne walimsindikiza mmoja wao kwa jamaa mmoja anaemdai aliekua anaeishi kwenye hicho kijiji ambacho kimekua kikikumbwa na matukio ya unyang’anyi na wizi wa vitu mbalimbali.

Daily post wameandika kwamba walipofika kwa mdaiwa kutokana na malumbano jirani yake ambae ni mama alianza kupiga kelele kwamba hawa wanafunzi ni wezi na ghafla ndio kikundi cha wananchi wenye hasira wakakusanyika na kuanza kuwapiga mpaka kuwachoma moto.


Taarifa nyingine kutoka mitandao mbalimbali ya Nigeria zinasema wanafunzi hawa wanne walimchukua mwenzao mmoja ambae anajulikana kwa ubabe ili wamtumie kumtisha huyu anaedaiwa atoe pesa haraka, huyu jamaa waliemuongeza akawa watano inasemekana alikua na bastola.

Wakati wa purukushani na mdaiwa aliionyesha hiyo bastola na wakati wananchi walipokusanyika baada ya kupigwa kelele za wezi jamaa mwenye bastola kwa uoga aliamua kuisalimisha ile bastola ambayo ndio wananchi walipata uthibitisho kwamba jamaa ni wezi, wakaanza kuwapiga lakini aliesalimisha bastola akafanikiwa kukimbia wkaabaki hawa wanne ambao ndio wameuwawa.
Taarifa zote nilizozisoma zinasema wanafunzi hawa hawakuwa wezi na wametoka kwenye familia zenye uwezo, hata mmoja wao miezi kadhaa iliyopita alikua nchini Marekani kwa mapumziko, ndio huyo hapo chini kwenye picha akiwa shopping Marekani.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg