YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday 24 August 2014

AMA KWELI NYEGE KWANZA AKILI BADAE... MUUZA GENGE AMBAKA MWANZAFUNZI KISHA KUMHONGA BUKU 5, MAZA ACHARUKA BAADA YA KUGUNDUA


Msala! Kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala, Dar kuna faili la kesi namba MBL/RB/ 9817/2014- KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI ambalo linamsaka kijana Juma Athumani (30), mkazi wa Charambe, Mbagala kwa kosa la ubakaji wa denti wa darasa la saba.

Add caption
Denti wa darasa la saba aliyebakwa na muuza genge anayefahamika kwa jina la Juma Athumani (30)
Habari za kiintelijensia zilidai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye ni muuza genge, alitenda kosa hilo Agosti, mwaka huu ambapo denti huyo alikuwa ametumwa na mama yake gengeni.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alimuomba denti huyo wazungumze kidogo ndipo akampeleka gesti kwa lazima.

Akizungumza na gazeti hili bora la habari za mastaa na kijamii, denti huyo alisema kuwa alipofika gesti, jamaa huyo alilipa fasta na kumvutia chumbani ambapo alianza kumshika ‘manido’ kisha akamtupia kitandani na kumwingilia kimwili bila ridhaa yake.

Mama wa mwanafunzi aliyebakwa.
Alisema kwamba, jamaa alipomaliza shida zake, alimpa buku tano (5,000/=) lakini alipokataa huku akilia ndipo mwanaume huyo akamuongezea hadi ikafika buku kumi (10,000/=).
“Niliporudi nyumbani mama aliniuliza kwa nini nimechelewa kisha akaziona hela, akaniuliza nimezipata wapi, nikamwambia amenipa Juma ndiyo tukaenda hadi gengeni kwa Juma kuuliza ndiyo mama akagundua kuwa nimebakwa.

“Baadaye mama alikwenda kuripoti polisi ndipo Juma akakamatwa na mimi nikapelekwa hospitali na kugundulika kweli nilikuwa nimebakwa,” alisema denti huyo.
Habari zilizotufikia punde kabla ya kuingia mitamboni zilidai kwamba uchunguzi wa polisi unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

NDOA YA MTANGAZAJI WA STAR TV SAUDA MWILIMA SASA NI SHIDA!


Oooh nooo! Miaka miwili baada ya kufunga pingu za maisha (ndoa) na mwanaume aitwaye Kauli Juma, imefichuka kwamba ndoa ya prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima ina shida kwani haishi na mumewe, ikidaiwa kwamba kila mmoja anaishi nchi tofauti na mwenzake.

Prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima akiwa na mume wake, Kauli Jumasiku ya harusi yao.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Sauda, kilisema kwamba baada ya wawili hao kufunga ndoa, Kauli aliondoka kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ alikokuwa akifanya shughuli zake kabla ya kufunga ndoa na hadi leo hajawahi kurudi Tanzania.
“Yaani baada ya Sauda kufunga ndoa, mumewe alikaa kwa miezi michache hapa Bongo, nasikia hata tendo la ndoa walifanya mara mbili tu.
“Hata alipojifungua na mtoto kufariki dunia kwa bahati mbaya, mumewe hakuwepo na hadi leo hajarudi, ukweli inauma sana ila Sauda ni mvumilivu kwani ndoa yake ni shida,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Sauda ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Sauda Mwilima akivishwa pete na mume wake, Kauli Juma.
“Ni kweli anaishi Sauzi. Tangu tukiwa wachumba tulielewana kwamba tukioana kila mtu ataendelea kuishi anapoishi hivyo mume wangu anafanya shughuli zake nchini Afrika Kusini na huwa anakuja mara mojamoja akiwa na nafasi au akiwa likizo.

“Mimi siyo mtu wa kujionesha kwamba eti mume wangu yupo nchini hivyo akija huwa ni kimyakimya anakaa tunaendelea na mambo ya familia yetu basi muda ukiisha anaondoka na tulikubaliana tangu tukiwa wachumba hivyo ikitokea mmoja wetu ameamua kumfuata mwenzake na kwenda kuishi naye hakuna shida,” alisema Sauda.Sauda aliongeza kwamba ndoa yake iko vizuri na hawajaachana na endapo ingekuwa haipo asingevaa pete ya ndoa.
“Ndoa yangu haijavunjika, tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake,” alisema Sauda.
Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 25/8/2014

.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

matangazaji mwenye gari la gharama, huyu hapa









“HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa
Manchester United, Wayne Rooney.
Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya magari yenye thamani kubwa kama hilo.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.



Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.

Ameinunua kwa bei gani?

“Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.

Alipolinunua

“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.

Spidi ya gari

“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.

Matumizi ya mafuta

“Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.

Usumbufu anaoupata

“Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.
“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.

“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.

“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha