YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday 27 June 2014

ANGALIA PICHA MAJAMBAZI WAWILI WALIOUAWA JANA


Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha ya bunduki aina ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya sanlg yenye namba T460 CVQ wamevamia duka la mpesa na kumuua mfanyabiashara Gosbert Kulwa(59) mkazi wa tambukaleli mjini Geita. 


Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la benki ya NMB ambapo majambazi hao walimpiga risasi ya tumboni mfanyabiashara huyo wa mpesa na kufariki dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.


Amesema mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo.


Kamanda ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia kwenye duka la mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua pesa kiasi ambacho hakijafahamika na kuchukua bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo. 


Aidha majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi 13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia makoti meusi na helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.


Jeshi la polisi lilipata taarifa muda mfupi zilizotolewa na raia wema ambapo kamanda wa polisi akiongoza kuwafuatilia majambazi hao walifanikiwa kuwakuta katika pori lililopo jirani na kijiji cha Ibambila wilayani Nyangh’hwale zaidi ya km 50 kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.


Wakiwa wanakimbizana majambazi hao walipowaona askari jambazi mmoja aliyekuwa na silaha aliruka kwenye pikipiki na kuanza kuwashambulia askari kwa risasi lakini dereva wa porisi alimfuta moja kwa moja na kumgonga kwa gari jambazi huyo na kufariki hapo hapo.


Baada ya hapo jambazi mwingine alikimbia kwa pikipiki na askari wakaanza kumfukuza wakishirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale na kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshambulia na alifariki wakati anakimbizwa kupelekwa hospitali.


Taharuki hiyo iliyokuwa imeikumba mji wa Geita kwa masaa takribani 3 kabala hawajakamatwa majira ya saa2 baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya tukio hilo huku kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha amani katika mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg