YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 25 June 2014

LUPITA SASA ANA MAHUSIANO NA RAPA HUYU.

Lupita Nyong’o athibitisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa huyu.

lupiii
Lupita amezidi kuchukua headlines za vyombo mbalimbali vya habari tangu afanikiwe kuchukua tuzo za Oscar na kutajwa kama mwanamke mrembo zaidi duniani, sasa amethibitisha kuhusu upande wake wa mahusiano kuwa ni kweli ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki K’naan kutoka Somalia.
lupita-knaan
Mara ya kwanza Lupita alikuwa akihusishwa na Michael Fassbender na Jared Leto lakini mwigizaji huyo amekita mizizi yake ya kimapenzi kwa rapa K’naan na wanafuraha na mahusiano yao.
Wapenzi hao mara kadhaa wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali wakiwa pamoja lakini hawakuwa wakiweka wazi nini kinaendelea kati yao na kufanya watu wahisi tu juu ya uhusiano wao.
lupita_nyongo_vogue_cover
Stori ni kwamba katika jarida la hivi karibuni la Vogue ambalo Lupita ametokea kwenye ukurasa wa mbele amethibitisha kweli ana uhusiano wa kimapenzi na K’naan na anampenda sana.
K’naan ni mzaliwa wa Somalia na ameingia katika umaarufu baada ya kuimba wimbo rasmi wa kombe la dunia kwa mwaka 2010 wa “Wavin’ Flag”.
Kila kinachonifikia ni halali yako kukipata mtu wangu! ili niwe nakutumia moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa twitter instagram na facebook jiunge na mimi kwa kubonyeza hapa TWITTER INSTA FB

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg