YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 25 June 2014

MWINGINE TENA ANG'ATWA NA SUAREZ

Ushahidi wa Suarez kumng’ata mchezaji mwingine – matokeo ya mechi ya Italy vs Uruguay na England vs Costa Rica

20140625-075306-28386633.jpg
Kwa mara nyingine katika kipindi cha maisha yake ya soka, Luis Suarez ameingia tena kwenye headlines kwa kumng’ata mchezaji mwenzie uwanjani.
Kwenye mchezo wa mwisho wa makundi kati ya Uruguay vs Italy, zikiwa zimebakia dakika 9 mchezo kuisha ulitokea utata mkubwa wakati Suarez na Chiellini walipokumbana katika maeneo ya penalti
20140625-081301-29581417.jpg
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati kwa refa kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Mpaka unamalizika Uruguay walikuwa washindi, na kuungana na Costa Rica kwenda hatua ya 16 ya michuano hiyo.
Wakati huo huo Italy iliungana na England iliyomaliza mechi zake za makundi kwa kutoka sare ya 0-0 na costa Rica – kufungasha virago kurudi nyumbani zikishindwa kufuzu kwenda hatua ya pili.
Uruguay sasa itacheza na Colombia wakati Costa Rica ikikutana na Ugiriki kwenye hatua ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg