YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday 4 August 2014

LAANA+AIBU KWA TAIFA: MASHOGA, WASAGAJI WAFANYA MKUTANO DAR...SHUHUDIA MWENYEWE HAPA...!




Mashoga wakiandamana kudai haki zao.Tumekwisha! Taarifa ikufikie kwamba wanaume tata ambao si riziki (mashoga) na wanawake wanaojishughulisha na mapenzi ya jinsi moja (wasagaji) kutoka nchi mbalimbali wamefanya mkutano wao mkubwa wa kimataifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina mkanda mzima.


Tukio hilo lililonaswa na gazeti hili lilifanyika kwa siku tatu mfululizo mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli maarufu iliyopo Posta jijini Dar wakitaka serikali ya Tanzania itambue na kuhalalisha mapenzi hayo ya jinsi moja na ikiwezekana hata katiba mpya inayotaka kuundwa sasa hivi viingizwe vipengele vinavyowahusu wao.



Baadhi ya Mashoga wakipata ukodaki. Bila kujua anazungumza na mwanahabari wetu, mmoja wao alipoulizwa nini kinaendelea hotelini hapo, alisema mkutano huo unawahusu mashoga na wasagaji huku akibainisha kwamba unafanywa kwa siri kubwa.




Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba. Baada ya kupata taarifa hizo, kachero wa Ijumaa Wikienda alizama ndani kimafia ambapo alinasa mazungumzo ya kikao hicho, ajenda kubwa ikiwa ni kuishinikiza serikali itambue uwepo wao hapa nchini.

Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg