YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 8 August 2014

MAN U NOMA KWELI, YAIZUNGUKA BARCA.

Man Utd ya van Gaal yaifanyia umafia FC Barcelona

posted 1 day ago by admin
Mashetani wekundu Man Utd wameuugeuza upepo wa harakati za kuiwania saini ya beki kutoka nchini Ublegiji na klabu ya Arsenal Thomas Vermaelen ikiwa ni siku moja baada ya kubainika FC Barcelona wametuma ofa ya paund million 10.
Man Utd wameonekana kuwa mstari wa mbele na huenda wakaipiku FC Barcelona katika mbio za kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 28, licha ya ada wanayotarajia kuiwasilisha Ashburton Grove kufanya siri.
Sababu kubwa zinazotajwa katika harakati za usajili wa usajili Thomas Vermaelen kuelekea Man utd, ni mikakati madhubuti inayopangwa na meneja kutoka nchini Uholanzi Aloysius Paulus Maria van Gaal *Louis van Gaal* ambaye amapania kumuona beki huyo akisalia nchini UIngereza.
Hata hivyo mchambuzi wa masuala ya soka nchini Uingereza James Olley amesema meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger hayupo tayari kukubali kumruhusu Vermaelen kujiunga na Man Utd, kutokana na kutotaka kurejea kosa alilolifanya kwa mshambuliaji Robin van Parsie.
Olley Amesema ana hakika meneja huyo kutoka nchini Ufaransa atakuwa radhi kukubali kumpeleka beki huyi FC Barcelona ili amalize mzizi wa fitna unaohofiwa kuibuka kutoka kwa mashabiki ambao siku zote wanachukizwa na hatua ya kumuona mchezaji wao akifanya vyema katika timu pinzani ya nchini Uingereza.
Umadhubuti wa mabeki Per Mertesacker pamoja na Laurent Koscielny unachukuliwa kama sababu ya pili kwa Thomas Vermaelen kuruhusiwa kuondoka Emirates Stadium katika kipindi hiki baada ya ile ya kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Thomas Vermaelen pia amesaliwa na mwaka mmoja katika mkataba wake, hivyo Arsenal wanaendelea kuwa na mashiko ya kukubalia kumuachia katika kipindi hiki na kujiunga na klabu nyingine kwa kuhofia suala la kuingia hasara ya kuondoka klabuni hapo kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg