YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 5 August 2014

ASKOFU KAKOBE: NINAUNGA MKONO UKAWA KUSUSIA BUNGE LA KATIBA




Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameongeza chumvi katika Mchakato wa Katiba kwa kueleza kuwa anaunga mkono msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutorejea kwenye awamu ya pili ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba. 

Kakobe pia alimtupia lawama Rais Jakaya Kikwete akisema hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo chanzo cha kuvuruga mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.

Kakobe ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita takriban siku tatu tangu Rais Kikwete alipotoa hotuba yake ya kila mwezi na kujivua lawama hizo alizokuwa akitupiwa na watu wa kada mbalimbali.

“Naunga mkono Ukawa si kwa asilimia 100 bali asilimia 150 kwa msimamo wao wa kususia vikao. Tena sitegemei kusikia wamerejea bungeni, wakirejea watakuwa wamelogwa. Lazima wahakikishe upungufu huo unafanyiwa kazi kabla ya kurejea kwenye awamu ya pili ya vikao hivyo vilivyopangwa kuanza Agosti 5,” alisema.

Aliongeza: “Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume. Sioni kosa langu ni kutoa maoni kuhusu baadhi ya vipengele vya rasimu kwa sababu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine,” alisema Kikwete kwenye hotuba hiyo.

Hata hivyo, jana Kakobe aliyezungumza kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Kanisa la FGBF alisema kuwa anapingana na utetezi huo kwani hauna hoja ya msingi kwani alishavuruga mchakato huo tangu awali.

“Hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo iliyoharibu mambo yote hadi sasa tumefika katika hali hii.Anafanya hivyo akiwa na dhamira ya kuvuruga mchakato huo ili usiendelee kwa kuhofia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanguka katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Mapendekezo ya wananchi, ambayo yameorodheshwa kwenye rasimu, yanakinzana na matakwa ya chama hicho hiyo ndiyo sababu,” alisema Kakobe kwa msisitizo.

Askofu huyo alisema, ikibidi Rais Kikwete angefanya uungwana kwa kurejea tena kwa wananchi kwa kuandaa hotuba nyingine ili kuwaomba radhi kwa kuvuruga mchakato huo ndiyo mambo mengine yaendelee.

“Hata kama yeye ni kiongozi, kama amekosea, anatakiwa kuomba radhi…lazima awatendee wananchi haki yao kwa kukiri kuwa yeye ndiye chanzo cha mvurugiko huo ili kuruhusu mchakato wa Katiba uendelee ili Watanzania wapate Katiba wanayoitaka,” alibainisha Askofu Kakobe na kuongeza:

“Sasa umefika wakati wa chama tawala kukubaliana na mabadiliko yanayotokea. Wananchi wa sasa siyo wale wa zamani wakuburuzwa tu. Siku hizi watu wajanja, watu wanataka kuona maoni waliyopendekeza yanafanyiwa kazi bila kuweka usiasa ndani wala si vinginevyo.”

Alisema kuwa juhudi zote za kuunda kamati kwa ajili ya kufanya vikao vya maridhiano ili kutaka Ukawa warejee bungeni zimekuwa zikigongwa mwamba kutokana na kukosa uthabiti juu ya hilo

DUNIA IMEKWISHA: MUME AFUMWA LIVE NA MKEWE AKINGONOKA NA MBWA DAR...MKE ADAI AMEMPA MIMBA MBWA HUYO..!MKASA MZIMA UPO HAPA!





Mwanamke anayejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis akiwa na mume wake(mtuhumiwa) Hamis Juma.DU! Kweli dunia sasa ni vululuvululu! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis (pichani), mkazi wa Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es Salaam amemlalamikia mumewe aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba ametembea na mbwa wao mweusi hadi kumpa mimba.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita. 

SIMULIZI YENYEWE
“Nililigundua hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala, nikamsikia mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia ili kujua sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana kumwona mume wangu yuko naye amemshikilia (asomaye na afahamu).
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema mwanamke huyo. 

MARA YA PILI
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo alisema:
“Siku iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia, nikaamka. Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.”

Akaendelea: “Hawa mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni majike na tangu walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja kwani mara nyingi tunawafungia kwenye banda lao.

 

Bw. Hamis Juma akijitetea kuhusiana na shutuma za mkewe.“Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.” 

AWAELEZA MAJIRANI
Mwanamke huyo alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua kuwaeleza majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa eneo hilo. 

MJUMBE MWENYEWE HUYU HAPA
Akizungumza na Uwazi, Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka Nyamaishwa alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo akamshauri kuyapeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.

 

Mbwa anayedaiwa kupewa mimba na Bw. Hamis Juma.MAJIRANI WAONA ANACHELEWA
Habari zaidi zinawekwa wazi kwamba, majirani nao walipoona mwanamke huyo anachelewa kwenda polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo walitoa taarifa katika Dawati la Jinsia.

Mkuu wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa hao kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3 kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea. 

SWALI LA MSINGI
Uwazi lilimuuliza swali moja mwanamke huyo, ni kwa nini anasema aliamka na kutoka nje usiku bila kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani hakuonyesha kushangaa kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”



Mbwa huyo akicheza na mwenzie.
JE, MUME ANASEMAJE?
Uwazi lilimgeukia mume wa mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu madai mazito ya mkewe ambapo alisema:
“Mimi sijawahi kufanya kitendo hicho na mbwa ila nahisi mke wangu na hawa majirani wa hapa wananitengenezea hilo tukio ili nikafungwe jela maisha, halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu kwani ndani ya ndoa yangu kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.” 


UWAZI LAMUULIZA DAKTARI WA MUHIMBILI
Uwazi lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.

Msikie: “Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
“Ila kama huyo mama anasema hivyo, mbwa akapimwe na ikibainika ni kweli basi yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia ina mambo yake.

MSALITI WA UKAWA HUYU HAPA

Wakati wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wa kususia vikao vinavyotarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, mmoja wa wajumbe wake jana aliripoti bungeni na kujiandikisha.
Mjumbe huyo, Clara Mwatuka ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa 6:30 mchana akiwa ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).
CUF ni moja ya vyama vinavyounda Ukawa, pamoja na Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wametangaza kwamba wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki vikao vya Bunge hilo.
Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Bwanausi.
Awali, alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu kuwapo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha bungeni

magazeti ya leo

Magazeti ya leo August 05 2015i

.
.
Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

BAS LA BUNDA LAPATA AJALI MBAYA MCHANA HUU...KWA TAAFA ZAIDI SOMA HAPA





 Toyota Coaster lenye namba za usajili T 399 BYC lililokuwa likitokea Musoma kwenda Bunda likiwa limepata ajali mchana huu eneo la Bitaraguru, Bunda mkoani Mara.

Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali wakisaidiwa kutoka kwenye basi hilo.

Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.

Basi hilo likiinuliwa na wananchi baada ya ajali.
BASI la abiria aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 399 BYC lililokuwa likitokea Musoma kwenda Bunda limepata ajali mchana huu na kujeruhi abiria katika eneo la Bitaraguru lililopo nje kidogo ya mji wa Bunda mkoani Mara.
Basi hilo limepata ajali baada ya kuacha njia na kupinduka. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo hakuna abiria aliyepoteza maisha.
( Whatsapp 0716909576, kama una tukio kama hili tutumie kupitia namba hiyo)

KILICHOWAKUTA YANGA HIKI HAPA

CECAFA yajibu kwa kuifuta Dar es salaam Young Africans

posted 4 hours ago by admin
Mabingwa wa soka Tanzania bara Azam FC, watashiriki michuano ya kombe la Kagame mwaka huu, wakichukua nafasi ya Dar es salaam Young Africans ambayo imetimuliwa na CECAFA kufuatia azimio la kupeleka timu ya vijana lililotangazwa na kocha mkuu wa klabu hiyo mbrazil Marcio Maximo mwishoni mwa juma lililopita.
Katibu mkuu wa baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA Nicolas Musonye, amesema wamefikia maamuzi ya kuiengua timu ya yanga kwenye michuano hiyo kutokana na maamuzi yao ya kutaka kupeleka kikosi cha vijana kuchukuliwa kama dharau.
Kufuatia maamuzi hayo Azam FC wanaingia katika kundi la kwanza la michuano hiyo ambalo lina timu za Rayon Sport ya Rwanda, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de L’Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti wakati Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
Ratiba ya michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame inaonyesha Azam FC watacheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya wenyeji Rayon Sport katika uwanja wa Amahoro Agosti 8, mwaka huu.
Mchezo mwingine kwa siku hiyo utachezwa saa nane mchana kati ya mabingwa wa visiwani Zanzibar KMKM dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini.
Mchezo wa pili Azam FC watacheza mnamo Agosti 10 dhidi ya KMKM, kabla ya kuivaa Atlabara Agosti 12, halafu itamaliza makundi dhidi ya Coffee ya Ethiopia Agosti 16.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano hayo ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawad

SAMWELI SITA JAMANIIIII.

0Aug

Karibuni tena Dodoma Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la kutunga Katiba ya nchi yetu. Sote tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu wetu kwa kuendelea kutupa uhai na afya hadi leo kutuwezesha kuwepo ndani ya ukumbi huu. Tupo humu ili tuitekeleze kazi waliyotukabidhi Watanzania wenzetu milioni arobaini na sita (46) ya kuwapatia Katiba mpya. Dhamana hii ni nzito na haistahili kufanyiwa ajizi.

Tunaendelea na shughuli zetu za Bunge Maalum kwa kuzingatia Kanuni ya 30 (1) inayosema
Akidi kwa kila kikao cha Bunge Maalum isipokuwa wakati wa kupitisha uamuzi wa Bunge Maalum itakuwa ni nusu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum“.
Nimetaarifiwa na Katibu kwamba wajumbe waliokuja Dodoma kuhudhuria ni zaidi ya robo tatu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum. Nawashukuruni nyote kwa kuja hapa Dodoma ili kutimiza wajibu wenu.
Kwa niaba yenu, nawashukuru Watanzania wenzetu wote ambao kwa mamilioni wamedhihirisha utashi mwema wa kisiasa kwa kuunga mkono hatua ya Bunge Maalum kuendelea na kazi zake hadi tuipate Katiba inayopendekezwa ambayo wataipigia kura ya maoni. Kipekee na kwa niaba yenu, nawashukuru kwa dhati viongozi wetu wa dini wa madhehebu yote wanaloliombea Taifa hili mafanikio Bunge Maalum, wakitanguliza utaifa pamoja na amani ya nchi na umoja ndani ya nchi na siyo ubinafsi na maslahi ya makundi.
 Kwa leo sikupenda sana kuzungumzia hoja mbali mbali zinazotawala magumzo ya mchakato wa Katiba mpya hapa nchini, magumzo yanayoendeshwa na makundi maalum kwa jazba na hata matusi. Hata hivyo nalazimika kutoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu upotoshaji mkubwa unaoendeshwa na baadhi ya watu kuhusu Bunge Maalum. Nikiwa Mwenyekiti wenu ninao wajibu wa kuwafafanulia wananchi kuhusu uhalali wa shughuli za Bunge Maalum linaloendelea na utaratibu wa shughuli zetu.
Ni Rasimu ya Tume au la
Wapo wanaodai kuwa eti hapa Bungeni hatujadili Rasimu ya Tume. Tuhuma hii haina ukweli hata kidogo. Msingi wa majadiliano yote tangu tumeanza ni Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Katiba. Utaratibu ni kwamba pale ambapo wajumbe wanaona panafaa kurekebishwa wanafanya hivyo. Maana ya rasimu ni andiko ambalo halijajitosheleza bila kupata ithibati ya taasisi ya juu zaidi. Anayekabidhiwa rasimu anayo haki na mamlaka ya kuirekebisha. Vinginevyo kujadili rasimu hakuna sababu. Itakuwa ni jambo la ajabu na lisilo na mantiki yoyote kuwa taasisi iliyopewa mamlaka ya kujadili Rasimu ikishaijadili iiache ibaki kama ilivyokuwa wakati ilipowasilishwa!
 Je suala ni muundo wa Muungano tu?
Maudhui ya Rasimu yanajumuisha baadhi ya masuala muhimu yafuatayo:
-      Kuimarisha Muungano wetu kwa kuleta uwiano     bora zaidi wa mamlaka ya Zanzibar na Tanzania      Bara ndani ya Muungano
-      Kuimarisha haki za binadamu ili kuwawezesha      raia wa kawaida kufaidi uhuru wa demokrasia     bila ubabe na dhuluma
-      Kuzuia wachache kufuja rasilimali za taifa bila       kujali maslahi ya wengi na ya vizazi vijavyo.
-      Kujenga uwiano sahihi na wenye haki baina ya      wanawake na wanaume katika nafasi za uongozi.
-      Kubainisha hatua zenye kuleta matumaini mapya ya maendeleo kwa makundi maalum ya vijana     wakulima wadogo, wafugaji, wafanyakazi wa ngazi   za kawaida, walemavu, wafanya biashara wadogo   na wajasiriamali wengine.
-      Kuweka msingi imara wa kutungwa kwa sheria      kakamavu za kuzuia ukandamizaji wa raia,        unyonyaji, wizi wa mali ya umma, rushwa,    hujuma dhidi ya uchumi na kuzuia mapato        haramu na fedha chafu.
-      Kutambua haki za ardhi kwa wakulima, wafugaji    na wajasiriamali wengine ili kupunguza migongano na migogoro.
-      Kuweka Misingi ya utawala bora inayozingatia        uadilifu, sifa stahiki na ufanisi.
-      Kuwezesha kutungwa kwa sheria bora zaidi     zitakazosimamia chaguzi zilizo za haki na huru    zaidi pamoja na kuwepo Tume za Uchaguzi       zilizoboreshwa.
Zaidi ya hivyo, yapo mapungufu katika Rasimu iliyopo kwa kuachwa masuala ya kuwezesha Serikali za mitaa; kutoa maelekezo kuhusu masuala ya matumizi ya ardhi na rasilimali nyingine za Taifa. Nini kinatuzuia kuiboresha Rasimu kwa kuyaongeza mambo haya ndani ya Katiba kwa faida ya Taifa?
 Yote haya ni masuala muhimu ambayo yamo ndani ya rasimu na wakati wake wa kuyaweka sawa ndiyo huu. Pamoja na umuhimu wake suala la muundo wa Muungano si suala la kutulazimisha tuyaahirishe mazuri yote yaliyomo katika Rasimu tuliyopewa.
 Uhalali wa Shughuli za Bunge Maalum
Pamoja na uhalali wa kisheria wa Bunge hili Maalum kuendelea kufanya kazi zake, linao pia uhalali wa kisiasa kutokana na sifa za uwakilishi wetu na pia maudhui yaliyomo ndani ya Rasimu. Kutofautiana maoni hakuwapi hadhi tofauti baadhi ya wajumbe kujiona wao wana uhalali zaidi mbele ya wananchi kuliko wenzao. Ndiyo maana utaratibu umewekwa wa kupiga kura na wa maridhiano. Utamaduni mpya unaoanza kujengwa na baadhi ya viongozi wa jamii wa kususia mijadala halali na kwenda nje kuelezea hoja za upande mmoja hauna nafasi katika Tanzania jamii isiyotaka fujo na utengano.
 Wajumbe wa Bunge Maalum wanaoendelea na kazi mjini Dodoma ni wateule wa Rais kwa niaba ya wananchi kwa kazi ya kutunga Katiba. Kazi hii haiwezi kusitishwa kwa sababu tu wajumbe wachache wameisusia. Tutazingatia matakwa ya sheria katika kufikia hatma ya mchakato wa Katiba.
 Mabadiliko ya Kanuni
Kama nilivyoeleza hapo mwanzo, Rasimu ina jumla ya sura kumi na saba (17) zenye mambo mengi yenye maslahi kwa Watanzania wote. Kwa muda tuliopewa wa siku sitini (60) isingewezekana kuikamilisha kazi tuliyopewa ndani ya muda. Ikumbukwe kwamba kwa Kanuni zilivyo, kila sura mbili zinahitaji siku tisa kuzifanyia kazi. Kwa njia hiyo, ingetuchukua siku takriban mia moja thelathini (130) ili kuikamilisha kazi hii! Pendekezo la msingi hapa ni kwamba Kamati zetu kumi na mbili (12) zizingatie na kuzijadili sura kumi na tano (15) za Rasimu na pia zikamilishe uandishi wa sura mbili zilizojadiliwa awali na ikibidi ziongeze sura ambazo zitadhihirika kuwa ni muhimu. Naamini mtiririko huu utatuwezesha kuwa na mpangilio bora zaidi wa sura na ibara katika Katiba mpya. Tusingependa na wala isingefaa kuomba tena muda wa ziada wa kazi ya Katiba ndio maana tunafanya mabadiliko ya Kanuni. Kamati ya Uongozi iliyoketi Dar es Salaam tarehe 28 Julai 2014 imependekeza yafanywe mabadiliko ya Kanuni za Bunge Maalum kuwezesha kazi ikamilike ndani ya muda tuliopewa. Kwa hiyo nitawaomba tuyatafakari mapendekezo ya mabadiliko ya Kanuni na hatimaye kuyapitisha ili ratiba ya kazi zetu iende sawa. Nitawaomba muikubali ratiba iliyogawanywa leo na pia mkubali kuzibadilisha Kanuni kwa lengo nililolieleza hapa.
 HITIMISHO
Pamoja na maoni ya kila namna yanayoendelezwa kujadili mchakato wa Katiba nje ya Bunge hili, ni muhimu wahusika wapunguze jazba, chuki na upotoshaji. Bunge Maalum lisaidiwe kwa mawazo chanya ili limalize kazi yake.
Sisi tuliomo humu katika Bunge Maalum tuna wajibu wa kuifanya kazi yetu kwa umakini na kwa uadilifu ili kazi yetu iwe bora. Tujadiliane kwa uungwana. Tofauti za mawazo zisitufanye tuingize chuki na maneno yasiyofaa. Katika mabadiliko ya Kanuni nashukuru sasa Kiti kimepewa mamlaka ya kushughulikia utovu wa nidhamu ndani ya wakati. Lakini ninaamini haitakuwa lazima kwangu mimi au Makamu Mwenyekiti kutumia nguvu za mamlaka yetu ila tu pale itakapobidi.
 Nawatakia nyote Mkutano wenye mafanikio kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
 MUNGU IBARIKI TANZANIA!
 Samuel Sitta – MB
MWENYEKITI BUNGE MAALUM LA KATIBA