Faida Nane za kufanya ngono
Mpenzi msomaji wa safu hii, juma lililopita tuliona na kujifunza baadhi ya dalili za mpenzi asiye na penzi la dhati kwako, hii tunajikita kujua walau faida tisa za kufanya ngono.
Ngono au tendo la ndoa lina faida kubwa katika mwili wa binadamu ambazo ni zaidi ya kustarehesha ama kustareheshwa hasa linapofanywa na watu wazima na tendo hilo ukizidisha unaweza kupata madhara kiafya .
1. Mzunguko wa Damu.
Tendo la ndoa huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini kutokana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo ambayo huboresha mzunguko huo wa damu pale unapopumua wakati wa kufanya tendo hilo.
2. Mazoezi ya mwili.
Watu wengi hawafanyi mazoezi lakini kufanya ngono ni moja ya mazoezi ya mwili ambapo unatakiwa kwa wiki moja asizidishe kufanya ngono mara tatu jambo ambalo litakusaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini pia ukifanya hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ni sawa na kukimbia maili 75 na tendo hilo huongeza karibia vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 uwanjani.
3. Maumivu
Unapofanya mapenzi homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo hupelekea kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo huwezesha kupunguza maumivu mwilini ikiwemo uvimbe, maumivu ya shingo na kichwa ambapo ukiona vitu hivyo vinakusumbua fanya mapenzi.
4. Mafuta yenye kileo
Huweka uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na mbaya na hupunguza kwa uwiano sawa kiasi cha mafuta mwilini.
5. Huondoa Maji yenye madhara
Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji yanayozalishwa kwenye prostate ambayo huwa na madhara kwa binadamu.
6. Usingizi mnono
Hakuna ubishi kwa yeyote aliyewahi kufanya ngono kuwa aliwahi kupata usingizi mnono isivyo kawaida hasa baada ya shughuli ambayo hata mnyama Simba angeingia mahala hapo pa faragha hakuna hata mmoja ambaye angeweza kuacha tendo hilo na kumkimbia Simba.
Kufanya mapenzi na kuupumzisha mwili kabla ya kuanza tena tendo hilo hasa kwa wanaume ni jambo muhimu ambapo utaupa mwili auheni ya kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini ambapo baadaye ukitaka kulala utalala swadakta…….
7. Kudumisha ujana
Homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwilini ambayo husaidia msisimko kuongezeka ambapo mwanadamu anayefanya mapenzi huongezewa ufahamu, kuimarisha mifupa, mishipa ya moyo na hata kuzuia wapinzani wa kazi za mishipa ya fahamu na hupunguza baridi na mafua na watu wanaofanya mapenzi huelezwa kuwa mara kadhaa huonekana vijana hata kama umri utakuwa umekimbia.
8. Homoni za kiume na za kike kuongezeka
Uzalishaji wa homoni za kike nausaidia kuimarisha mifupa na misuli na kwa mwanamke tendo la ndoa humwongezea homoni ambayo inatunza tissue za sehemu ya uke na humsaidia kupokea mapenzi na kuwajibika awapo mahala husika na mwenzi wake.
Mpenzi msomaji wangu bila shaka umeanza kupagawa baada ya kuona walau faida chache za kufanya mapenzi, sasa wiki lijalo kiume huongezeka mara dufu ambapo kwa mwanaume humsaidia kuimarika kwa homoni ya kiume ambayo htutaangalia dalili za mwanamke anapotaka ngono.
No comments:
Post a Comment
gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg