Headlines nyingine zilianza kuandikwa Tanzania kwenye Siasa 2015, ambapo July 28 2015 Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli alikaribishwa CHADEMA na kupewa Kadi za Uanachama yeye pamoja na mkewe, Mama Regina Lowassa.
Stori baada ya stori zikaendelea kutawala kuanzia hapo, akafika Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni Dar es Salaam kuchukua Fomu na kurudisha pia… August 04 2015 Kikao cha Chama hicho kimefanyika Ukumbi wa Mlimani City Dar, Edward Ngoyai Lowassaametambulishwa kuwa Mgombea Urais wa umoja wa Vyama vya UKAWA na Juma Duni Haji ndio Mgombea Mwenza.
Hapa ni pichaz ilivyokuwa kuanzia nje mpaka ndani ya Ukumbi.
Hii ilikuwa mwanzo kabisa kabla Kikao hakijaanza.
Rapper Prof. Jay ambae anagombea pia Ubunge Jimbo la Mikumi, Morogoro.
Aliyekaa katikati ni Mbunge wa Kawe, Halima James Mdee.
Wabunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Godbless Lema na Joshua Nassari.
Wabunge David Silinde na David Kafulila.
Baadhi ya Wanafamilia na ndugu wa Edward Lowassa.
Maaskofu Zacharia Kakobe na Josephat Gwajima.
Prof. Mwesiga Baregu (Aliyekaa katikati)
Mbunge Halima Mdee na Mama Regina Lowassa.