YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 4 August 2012

MSANII WA KIZAZI KIPYA Rhymes Of Magic Atractions aka, ROMA MKATORIKI APATA AJARI AKIWA KWENYE GARI LAKE KWENDA KWENYE SHOO MOROGORO.

Baada ya kupata ajari, Muonekano wa Gari lenyewe

Rafiki yake na ROMA, ambae waliku wote kwenye tour.

Gari lenyewe kwa mbele.



ROMA mwenyewe akiwa kwenye mawazo pamoja na mahojiano mafupi na askari wa usalama barabarani

Friday, 3 August 2012

MJANE AMUOMBA IGP MWEMA AMPE ULINZI


SIKU mbili baada ya kukamatwa mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya Onesphory Kituly, mjane wa marahemu, Mary Kituly amemwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema kumhakikishia usalama wake.

“Ombi langu kwa sasa ni moja tu, IGP anisaidie kwa hali na mali juu ya  usalama wangu. Hao watu ni hatari. Wana mtandao mkubwa,” alilalamika  Kituly huku akitokwa machozi.

Aliongeza: “Mazingira ya mauaji ya mume wangu ni ya kutisha. Niliona dalili tangu siku nyingi kwa hiyo nina kila sababu ya kuhofia usalama wangu.”

Kabla ya kuuawa, marehemu Kituly (54), alikuwa akiwashtaki mfanyabiashara huyo anayeshikiliwa polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na wafanyabiashara wengine wawili, kwa madai ya kumdhulumu nyumba ya zaidi ya Sh600milioni. 

Alidai Oktoba mwaka jana, mtu asiyejulikana alimmiminia marehemu Kituly risasi tano kifuani, tumboni na mdomoni wakati marehemu akijiandaa kuingiza gari lake katika uzio wa nyumba yake Magomeni Mapipa, Dar es Salaam.

Ndugu wa marehemu wanaamini muuaji huyo ambaye hakuchukua kitu chochote kutoka kwa marehemu alikodiwa kutekeleze mauaji hayo. 

Inadaiwa muuaji alitumia muda mwingi kuvinjari katika maeneo alipoishi marehemu na alipata mwanya wa kutekeleza mauaji pale marehemu alipotoka nje kuingiza gari. 
Muuaji alimsogelea Kituly na kuegemea mlango wa gari na kisha kummiminia risasi.
Polisi wanasema mauaji hayo yanaweza kutekelezwa na watu au mtu ambaye marehemu alimdai ili kuepusha usumbufu au yametokana na kutokuelewana kibiashara. 

Siku moja baada ya tukio, shahidi mmoja aliiambia Mwananchi kuwa alimfuatilia muuaji kutoka Magomeni hadi eneo la Shekilango karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii, lakini hakuweza kumkamata baada ya kukosa msaada wa polisi.

Alidai walimfuatilia muuaji na kupanda naye daladala Kituo cha Magomeni Mapipa na alishuka na kumuacha kwenye daladala na kukimbia kuomba msaada wa kumkamata, lakini polisi walimtaka asubiri gari. 

Polisi walipinga vikali tuhuma hizo na kuziita maneno ya mitaani yaliyohitaji uthibitisho wa kutosha.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliahidi kuzifanyia kazi taarifa hizo akisema “nia yetu ni kufanikisha kumkamata muuaji na kumleta kwenye mkono wa sheria.”


Juzi, takriban miezi kumi baaada ya mauaji, kamanda Kenyela amekaririwa na gazeti moja akisema polisi wanamshikilia mfanyabiashara maarufu Kituo cha Polisi Magomeni kuhusiana na mauaji hayo.

WALIMU WANADANI MASLAI YAO.!!!!

HAPA HATA MGOMO UKISITISHWA KWA NGUVU BILA KUTEKELEZEWA MADAI YAO INAONEKANA BADO ITAENDELEA KUA TATIZO.

Wednesday, 1 August 2012

EXCLUSIVE: NGASSA AFUNGUKA: SINA TAARIFA RASMI JUU YA KUUZWA SIMBA - AZAM WAFUATE TARATIBU

Mrisho Ngassa akiwa na Shaffi Dauda wa Clouds fm na Sports Extra.

Muda mchache uliopita tumefanikiwa kufanya mazungumzo na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa ambaye klabu yake Azam leo imethibitisha kwamba ameuzwa kwenda klabu ya Simba.

Katika mazungumzo hayo Mrisho Ngassa amesema  kwamba yeye binafsi hajapata taarifa rasmi kutoka kwa klabu yake ya Azam juu ya kuuzwa kwenda Simba. "Kiukweli hizo taarifa mie nazisikia na kusoma kwenye mitandao tofauti lakini muajiri wangu bado hajanipa taarifa rasmi juu ya hili suala. Pia huu utaratibu sidhani kama ni sahihi, wanawezaje kuniuza timu nyingine bila kunihusisha, vipi kuhusu maslahi yangu katika hiyo timu nyingine nani ameyasimamia? Kwa maana hii bado nashindwa kuamini kama Azam watakuwa wamefanya hivyo. Ilipaswa wanipe taarifa kwamba Ngassa tunakuuza kwenda timu fulani na nina haki ya kuchagua kukubali au kukataa.

Ngassa akaendelea alivyoondoka Yanga, "Mimi sitaki kuondoka Azam huku kukiwa kuna hali ya kutokuelewana kati yangu na wao pamoja na wapenzi na mshabiki wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye kipindi chote nilichokaa pale. Unaweza ukajiuliza kwanini mimi mpaka leo kwanini mashabiki wa Yanga wanaonyesha mapenzi kwangu au ninakuwa na ukaribu nao, ni kwa sababu wakati naondoka Yanga nilipewa baraka zote na klabu yangu, yaani niliondoka vizuri. Azam walikuja wakaongea na Yanga wakakubaliana na ada ya uhamisho then na mie nikapewa taarifa nikakaa chini na Azam tukakubalina mahitaji yangu binafsi sasa iweje leo wao wameshindwa kufuata utaratibu ule ule ambao waliufuata wakati wa kuninunua kutoka Yanga. Ilipaswa wao kabla ya kukubaliana na Simba ingebidi na mie nipewe taarifa ili kuweza kukubaliana mahitaji yangu binafsi na Simba then ndio niuzwe. lakini sivyo walivyofanya."

Alipoulizwa kama Simba wakimpa vile anavyovitaka atakuwa tayari kuichezea klabu hiyo, Ngassa alijibu, "Mpira ni kazi yangu, ninafanya hii kazi ili kuweza kujikimu kimaisha maisha. Kama klabu yoyote ikikubali kunipa mahitaji yangu niyatakayo na nikapendezewa nayo nitajiunga nayo. Taratibu lazima zifuatwe na kuniuza kama kiroba cha mchele, kwa hali ilivyo mpaka sasa sitoweza kujiunga na Simba"

Tuesday, 31 July 2012

MANENO YA MSG YA MH. ZITTO KWENDA KWA KATIBU MKUU WA NISHATI NA WAZIRI MHUSIKA

Katika Gazeti la leo la Majira kuna ujmbe unaodaiwa kuandikwa na Mh.ZZK kwenda kwaKatibu Mkuu wa Nishati na Waziri Mhusika wa Wizara Bw. Maswi na Prof.Muhongo. Naomba kuunukuu " Bw. Maswi alitumiwa na Bw. Zitto, unasomeka hivi; “Maswi, sijawahi gombana na wewe kwa kuwa nakuheshimu sana, tuhuma ambazo wewe na Waziri wako mnatoa dhidi yangu ni uwongo, uzushi na za kupikwa. Mwambie Waziri wako na wewe binafsi, sijawahi kushindwa vita ya kulinda credibility yangu, sipendi ujinga hata kidogo, mimi nina uhuru wa kusema ninachoamini, sina bei tupambane tu tuone nani ataumia,” ujumbe huo unasomeka hivyo

HII NDIO COPY YA BARUA YA UMOJA WA WASANII WALIOIANDIKA KWA KAMPUNI YA PUSH MOBILE

Hallow people...

MWEZI WA RAMSO BADO WATU WAJIRUSHA TU!!!

Wakuu wakikata vinywaji Mwezi Ramso..

Hwa nao wanacheza disco Mwezi Ramso...
Hallow people...

BAADA YA KUTOKA TANGA SASA NI ZAMU YA DSM, JIPANGENI SASA WAJA HAWA WATU.

Masta J kushoto, Madame Rita katikati, Salama kulia, makini kabisa kwa kuanza kazi iliowapeleka...

Monday, 30 July 2012

TUNAJIVUNIA NINI KWENYE OLYMPIC WATANZANIA?

wanamichezo wa olympic wa kitanzania huko LONDON
Hallow people...

BAADHI YA MAGAZETI KWA SIKU YA LEO july 31, 2012

















Hallow people...

KAULI ZA BAADHI YA WABUNGE KUHUSU RUSHWA BUNGENI.


Baada ya kuwepo malalamiko ya rushwa kutembea bungeni na kusababisha kuvunjwa kwa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya Wabunge wametaka majina ya wenzao wanaojihusisha na rushwa yawekwe wazi na wafukuzwe bungeni.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (CHADEMA)amesema pamoja na kwamba kamati ya nishati na madini imetajwa moja kwa moja, zipo kamati nyingine ambazo wabunge wake wanatajwa kuhusika na kuomba rushwa.
Amesema “zipo kamati kadhaa zinatuhumiwa kwa rushwa, Mh Spika nilikua naomba muongozo wako kwamba kwa nini ofisi yako isiamue kuzivuruga kamati kadhaa ambazo zinatuhumiwa kwa rushwa ikiwemo kamati ya kudumu ya bunge ya Serikali za mitaa inayoongozwa na Mh. Mrema na Kamati ya kudumu ya bunge ya Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mh. Zitto Kabwe, hii ni kwa sababu wabunge wengi wamekua wanazikimbilia zile kamati ambazo zina mikataba lakini kamati kama ya maendeleo ya jamii ya huduma za jamii ambazo zina umuhimu mkubwa kwenye nchi kwa sababu hazina mikataba zinakimbiwa”
Mbunge wa Lindi mjini Salum Khalfan na mbunge wa Nkasi kaskazini Ally keissy Mohamed wamelitaka bunge kuwafukuza bungeni wabunge wote watakaogundulika kula rushwa, wanataka watajwe kwa sababu sasa hivi wabunge wengine kila wakipita barabarani wanakosa raha kutokana na hiyo kashfa ya rushwa iliyolichafua bunge.
Baada ya hayo Naibu Spika wa bunge Job Ndugai aliomba kamati ya uongozi wenyeviti wa kamati za bunge kukutana na Spika kulizungumza ili baadae wampe maelekezo zaidi.