Thursday, 23 October 2014
CHEKI BARUA YA DIAMOND KWENDA KWA JWTZ
Hatimaye diamond Platnum aomba msamaha baada ya kua ametumia gwanda za Jeshi. Cheki barua alioiandika kwenda kwa JWTZ
YP AAGWA KWA MACHOZI MENGI!!! WASANII MBALIMBALI AKIWEMO JUMA NATURE WALIMWAGA YAO YA MOYONI!!
Y - P azikwa |
YP kabla ya kuhamia katika sanaa ya uimbaji na kuibuka na kundi la wanaume Family alikuwa akifanya sanaa ya maigizo na vichekesho akiwa kundi moja na wasanii, Masanja Mkandamizaji, Mpigapicha maarufu na Blogger Mroki Mroki, Kiwewe, Dokii enzi hizo wakiwa na kundi la Get Well Generation lililokuwa chini ya Dokii na kurusha michezo yake Star Tv
Tuesday, 21 October 2014
Monday, 20 October 2014
TAZAMA PICHA ZA KISIMA CHA AJABU KILICHOPO MJINI DODOMA..!
mbili za Wanyazaga na Wambukwa mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo Katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM]
Baadhi ya wananchi wakifurahia kutumia maji yanayopatikana kisima cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma, kisima hicho kilichovumbuliwa katikati ya miaka 1,800 kiko katika hatihati ya kufukiwa na eneo hilo lituumike kwa matumizi mengine.
Mkuu wa kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akinywa maji yaliyochotwa kisima cha Bwibwi kilichopo Kijiji cha Iyubu Manispaa ya Dodoma, Kisima hicho kinachoaminika ni cha maajabu na mtu anayetumia maji yake hupata Mafanikio ya kiafya na kimaisha
HUU MSALA NA MAJANGA SASA ,BABA ACHOMA MOTO NYUMBA NA KUFA YEYE NA MKEWE BAADA YA KUGOMBANA
Mume na mke wamejilipua namafuta ya Petrol Mkoani Mtwara baada ya kutokea kwa ugomvi baina yao wakati wa usiku.
Kamanda wa Polisi alisema vifo hivyo vilitokana na ugomvi wa kifamilia ambapo Mume huyo aliyetambulika kwa jina la Selsius Kamguna alimpiga mkewe hadi kupoteza fahamu.
Alisema baada ya kuona mke wake amepoteza fahamu aliamua kuteketeza nyumba yao kwa moto akitumia mafuta ya petroli wakiwa ndani kitendo kilichosababisha wote wawili kupoteza maisha,
HICHI NDIO KILICHOMFANYA T.I KUKERWA NA KUWATUKANA MASHABIKI WAKE...SOMA HAPA KUJUA UNDANI ZAIDI
Rapper T.I ameamua kuvunja ukimya na kutoa matusi kwa mashabiki wake waliokuwa wakimkejeli na kumtukana kwa uamuzi wake wa kuja Africa
Katika moja ya picha zake kupitia ukurasa wake wa insta aliyokuwa ameituma akiwa Tanzania, mashabiki wake kutoka marekani walimshambulia kwa kuchukua uamuzi wa kuja Africa wakati akijua wazi kuna ugonjwa wa Ebola, na hata kudiriki kusema “ndio maana ugonjwa huo unawafikia wamarekani.
Baada ya comment za aina hiyo kuongezeka kwa kasi T.I aliamua kuvunja ukimya na kumkibu mmoja wa mashabiki hao aliedai kuwa “Ebola ipo huko na bado mnasafiri???ndio maana ugonjwa huo umefika US
TAARIFA KUTOKA JENZI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)
JJESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
Aidha, kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ. Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963
Subscribe to:
Posts (Atom)