YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 5 July 2013

LOWASA AONGEA NA WAFANYA BIASHARA WA JIJIO LA MWANZA.

Hallow people...

WAZIRI MAGUFULI ATAMANI KUWA RAIS WA TANZANIA......ANADAI KWAMBA YUPO TAYARI KUGOMBEA MWAKA 2015 ENDAPO ATAKIDHI MASHARTI


 Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.
Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.


Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita  kuendelea na wadhifa huo.

“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,
” alisema Dk. Magufuli.

“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh.   3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa  ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

"GEREZANI KUMENIFANYA NIMJUE MUNGU VIZURI SANA"....HII NI INTERVIEW YA LULU MICHAEL





Kwa mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu. 

Lulu aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.
 Katia interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa, mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza.

Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age


Ninaplan kufanya uzinduzi kwaajili ya movie yangu, lengo kubwa la kufanya uzinduzi ni kwamba kwanza nitajiskia vizuri kukutana na ‘okay these are my fans’ kukutana nao sehemu moja. Kuna vitu sitaweza kuongea kwenye interview ntahitaji kuviongea mwenyewe kama mwenyewe. 



Nitahitaji watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish Age. Nitaizindua chini ya kampuni ya Proen (????) Promotions Ltd na ni kampuni ambayo ndio inanimanage kwa sasa.

Kuhusu kama ana boyfriend aliyemnunulia vitu vya thamani

Watanzania wengi tulishajiwekea ile dhana kwamba ‘ukiona mwanamke amefanya kitu basi there is a man behind, yaani ni ile dhani ipo tayari ndani yetu kwahiyo hata kama mtu atastruggle kutafuta kitu chake mwenyewe lakini hiyo itakuwa ni ukweli wako na unaujua mwenyewe . 



Kiukweli ni kwamba hakuna mwanaume yeyote ambaye amenifanyia chochote till now. Nachoshukuru tu ni menejimenti yangu, kampuni ambayo nafanya nayo kazi.


 Ni kampuni ambayo inanijali, inajali kazi zangu, inajali msanii wao kwahiyo whatever I’m having, whatever I’m doing ni mimi mwenyewe, ni kazi zangu ni biashara yangu.

Uhusiano wake na Mama Kanumba na jinsi alivyompata kufanya naye movie ‘Mapenzi ya Mungu’

Kwa sasa hivi tupo kama familia kwa hiyo it wasn’t hard mimi kumpata na nilijisikia vizuri kama ntaweza kufanya naye kazi. Kuna spirit ambayo ilinivuta zaidi nifanya kazi na Mama Kanumba kuliko labda mama mwingine.

Anachomiss kwa Kanumba

Busara zake, he was a person ambaye akikuona unaenda hivi he takes you in the right way.

Kuhusu kwanini mapenzi yake na Kanumba yalikuwa siri
Ni makubaliano tu and there was no need like to let people know yaani kumfanya kila mtu ajue nadhani haikuwa na maana kwetu.

Kuhusu kwanini alinenepa alipokuwa gerezani


Labda kwasababu nilimwachia Mungu kila kitu, nilimkabidhi Mungu kila kitu so I had this peace of mind. Niliacha kwamba yeye ni msimamizi wa kila kitu. Let me confess kwamba gerezani kumenifanya nimjue Mungu vizuri sana,. 



Kumenifanya nimjue na nimwamini na kumjua na kumwamini kumetokana kwamba kuna vitu vingi vimekuwa vinafanyika like naviona hivi kwa macho na naona kabisa kwamba hapa ingekuwa mimi kama mimi ama binadamu yeyote haiwezekani... 

So ni Mungu tu ndio ameweza kufanya hili likapita. Kwahiyo niliamua tu kumwachia yeye kila kitu nikajikuta tu nina amani.

KAJALA NA MZEE JENGUA HAWA HAPA USO KWA USO:






CONTINUE READING:









AJALI ZAENDELEA KUTUMALIZA WATANZANIA.....TUNAOMBA RADHI KWA PICHA


 Ajali hii ilitokea jana jioni  tarehe 02/07/2013, baada ya gari dogo lililokuwa linatokea maeneo ya Ubungo kwenda uelekeo wa Buguruni kumgonga mwenda kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara katika maeneo Gereji (garage)...
Damu ilimtoka kwa wingi sana mara baada ya ajali katika maeneo ya kichwani, na hapo ilipotokea ajali kuna kivuko cha waendeo kwa miguu
Darubini Leo

DENT WA MWAKA WA KWANZA AIBA SIMU AINA YA BLACKBERRY NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI:BALAA LAKE SASA SHUHUDIA MWENYEWE:


Tukio hili limetokea huko Nigeria ambapo binti anayesemekana ni wa mwaka wa kwanza alikwenda kutembea katika hostel za wenzake na alipopata mwanya akaiba simu aina ya Black Berry.

 Hata hivyo baada ya mwenye simu kushtuka binti huyo aligoma kuichukua simu hiyo na

ndipo watu
walipoamua kuipiga simu na kuanza kuita ikiwa sehemu za siri. Baada ya tukio hilo wavulana kutoka vyumba vya pembeni walikuja na kumsachi huku wakimvua nguo, hakuwa na la ziada zaidi ya kuwa mpole wakati watu wakimpiga picha hizo za aibu.

HAPA NDIPO ATAKAPOZIKWA MZEE MANDELA PINDI ATAKAPOFARIKI..



Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama wa kuamuru miili ya watoto wake watatu iliyohamishiwa Mvezo, ifukuliwe na kwenda kuzikwa tena Qunu
Pretoria.
Vita ya wapi atakapozikwa  Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela imefikia tamati na sasa ni rasmi kwamba atazikwa Qunu uamuzi ambao umeacha ufa na uhasama mkubwa katika familia ya kiongozi huyo.
CONTINUE READING
Jana, mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela ambao ni marehemu ilitarajiwa kuzikwa upya katika eneo la Qunu, yakiwa ni mazishi ya mara ya tatu tangu walipofariki dunia katika vipindi tofauti, ukiwa ni utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ya Eastern Cape.


Uamuzi huo ulimaanisha kushindwa kwa mjukuu wa Mandela, Mandla ambaye jana katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema: “Sikusudii kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama,” lakini akahusisha ugomvi katika familia ya babu yake kwamba ni vita ya fedha na mali za Mandela.
Mabaki hayo ni ya mtoto wa kwanza wa kiume wa kiongozi huyo, Makgato aliyefariki dunia 2005, binti yake wa kwanza Makaziwe (mkubwa) ambaye alifariki akiwa mchanga mwaka 1948 na mtoto wake wa pili wa kiume, Madiba Thembekile aliyefariki katika ajali ya gari 1969.
Mahakama Kuu ya Eastern Cape ilitoa uamuzi uliowapa ushindi wanafamilia 16 wa Mandela ambao walifungua madai wakiongozwa na shangazi yake Mandla, Makaziwe.
Jaji Lusindiso Pakade katika hukumu yake, mbali na kutoa amri hiyo alitaja vitendo vya Mandla kuwa ni vya aibu visivyo vya kibinadamu hivyo kutoa amri ya kufukuliwa miili hiyo na kisha kurejeshwa Qunu. Mabaki hayo yalihamishwa kutoka kijiji cha Mvezo ambako yalizikwa mara ya pili kwa kificho miaka miwili iliyopita na mjukuu mkubwa wa Mandela, Mandla ambaye pia ni kiongozi wa kimila katika kijiji hicho.
Kazi ya kufukua makaburi ya watoto wa Mandela katika eneo la Mvezo ilifanyika hadi juzi usiku chini ya ulinzi wa polisi baada ya madalali wa mahakama kutumia sururu kuvunja lango (geti) kuu la kuingia katika makazi ya Mandla.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa eneo hilo, Luteni Kanali Mzukisi Fatyela, uchimbuaji wa makaburi ulifanywa na wataalamu wa Kituo cha Afya cha Mthatha na baadaye kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo hicho juzi usiku na jana asubuhi mabaki ya marehemu hao yalifanyiwa uchunguzi wa kimaabara kabla ya kupelekwa Qunu kwa maziko.
Madaraka au fedha?
Makaziwe (60) ambaye ni binti mkubwa  wa Mandela na wenzake 15 kutoka katika familia hiyo, walifungua madai wakitaka kurejeshwa kwa mabaki ya miili hiyo Qunu wakisema Mandla aliyahamisha bila makubaliano ya familia. Mandla katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Mvezo jana alisema ugomvi uliopo ni wa kimasilahi na kwamba familia inawania fedha za babu yake.
Alisema chimbuko la kuandamwa linatokana na msimamo wake wa kukataa kuondolewa katika bodi ya ya mfuko wa Mandela baadhi ya watu wakiwamo Wakili George Bizos na Waziri wa Makazi Tokyo Sexwale. “Sasa wameamua kunilenga mimi kama mlengwa dhaifu.

DENT WA MWAKA WA KWANZA AIBA SIMU AINA YA BLACKBERRY NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI:BALAA LAKE SASA SHUHUDIA MWENYEWE:


Tukio hili limetokea huko Nigeria ambapo binti anayesemekana ni wa mwaka wa kwanza alikwenda kutembea katika hostel za wenzake na alipopata mwanya akaiba simu aina ya Black Berry.

 Hata hivyo baada ya mwenye simu kushtuka binti huyo aligoma kuichukua simu hiyo na

ndipo watu
walipoamua kuipiga simu na kuanza kuita ikiwa sehemu za siri. Baada ya tukio hilo wavulana kutoka vyumba vya pembeni walikuja na kumsachi huku wakimvua nguo, hakuwa na la ziada zaidi ya kuwa mpole wakati watu wakimpiga picha hizo za aibu.

KUNDI LA BAIKOKO TOKA TANGA NI BALAA TUPU...WAPI TUNAKWENDA?


Hizi  ni  baadhi  ya  picha  za  kundi  la  wacheza  uchi / nusu  uchi  maarufu  kwa  jina  la  Baikoko  lenye  maskani  yake Tanga....

 
 
 
 

Wednesday, 3 July 2013

Video: Psquare wamekamilisha yao tena watupia style za Michael Jackson single mpya video mpya "personally"


Psquare wamefanya yao kwa mara nyingine tena, baada ya kuachia bonge la hit "Personally" huku video yake ikiwaonyesha kutupia styles za kudance tulizoachiwa urithi na King wa Pop (Michael Jackson). cheki na video pamoja na audio hapo chini

 

Exclusive Nu joint: Bila kukunja goti / AY & FA feat J Martins


Leo hii kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm, AY ameachia single mpya akiwa na FA pamoja na J Martins kutoka Nigeria "Bila kukunja goti" , mkono ukiwa wa Producer Macochali studio za MJ.

akizungumza na Fetty pamoja na Adam mchomvu, AY alisema kuwa idea nyuma ya wimbo huo ilitoka kwa Macochali na wao kama wasanii ndio wakajazia lyrics na kuikamilisha ambapo nakupa nafasi ya kuisikiliza hapa.


Picha: Harusi ya Paul james na Wasiwasi mwabulambo


Picha za harusi ya Paul James na Beatrice, Paul James Mtangazaji wa Clouds FM Kipindi cha Power Breakfast, Harusi ilifungwa siku ya Jumamosi 22/6/2013 jijini Dar es salaam.




Harusi ya wasiwasi Mwabulambo na Janeth ilifungwa kwenye Kanisa La Kilutheri Boko Dar Es Salaam Na Baadae kwenye tafrija iliyofanyika Mbezi Beach siku ya Jumamosi 22/6/2013.Clouds Media Group intakutakia maisha mema ya ndoa na Mungu awaongoze katika kila jambo..Amen.



Video: Wema Sepetu akiporomosha matusi ya nguoni kwa mlinzi baada ya gari lake kuibiwa power window likiwa ndani kwake


Msanii nyota wa Bongo movie, Wema Sepetu, leo hii amejikuta akitoa matusi ya nguoni kwa mlinzi wake baada ya kukuta gari lake likiwa limeibiwa power window na betri la gari lake kuchomolewa.
hali hiyo imetokea nyumbani kwake Kijito nyama, pale alipokuwa akijaribu kuwasha gari lake na kuondoka.
video hii inaonyesha masjirani waliposkia kelele za matusi kutoka kwa mwanadadiva huyo waliamua kupanda sehem na kuchukua video ya kilichokuwa kikiendelea kwa kujificha.

Wema akimkimbiza mfanyakazi wake huku akiwa na beseni lenye maji
Mlinzi sa sijui alikuwa anaiwaza segerea au amechoka kwa mbio zilizokuwa zikiendelea humo ndani, au ndio zile "mungu wangu ntafanyaje mie mtoto wa watu"

 

Video: Raisi wa Marekani Barack Obama akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam



Baada ya kutua jijini Dar leo hii, Raisi Barack Obama aliongea na waandishi wa habari, Ikulu jijini Dar es salaam


Video streaming by Ustream

MACHANGUDOA"UJIO WA OBAMA HAUKUWA NA MASLAI KWETU"



Katika hali ilisiyokuwa ya kawaida,  machangudoa wameulalamikia ujio wa Rais Barack Obama kwa kile kinachodaiwa  kuwa  haukuwa na faida yoyote kwa kukosa dili za pesa. 


" Tumesikitishwa sana na ujio wa Obama kwani tulikuwa tumejipanga kupiga hela ndefu sana . 
"Bahati mbaya watu  wake tuliokuwa tunategemea kuwanasa walikuwa busy na wale  wa  mikoani  walizuiwa" Walisema akina dada hao.
 
Machungudoa hao wanadai  kuwa  kipindi cha Bush alipokuwa Rais ambaye alikaa nchini karibu wiki moja walinufaika sana ambapo wengi wao walijenga majumba kwa pesa za ziara ya Bush .

MSANII MAARUFU WA BONGO MOVIE ABAKWA!!!!!




Kuna habari mbaya ambazo zilianza kusambaa mtandaoni jana.Habari hizo zinazomhusu msanii maarufu wa bongo movie ambaye anadaiwa kubakwa (Mtungo ) na wanaume kadhaa.

Habari hizo zinadai kuwa, Msanii huyo wa kike mwenye jina kubwa hapa nchini alikutwa na balaa hilo baada ya kuwachanganya kimapenzi washikaji wawili ambao ni kama marafiki na hivyo wakaamua kulipa...

Ili kutimiza kisasi chao, habari zinadai kuwa "mpenzi mpya" alimuomba msanii huyo wakutane hotelini ili wakafaidi maisha.Wakati huo huo, "mpenzi wa zamani" alipewa taarifa kwamba watakutana hoteli flani na saa flani.

"Mpenzi wa zamani " alitinga eneo la tukio akiwa na vijana kadhaa na kisha akabana sehemu kumsubiri mhanga wa tukio....

Muda ulipofika, msanii huyo akiwa na "mpenzi wake mpya" waliingia hotelini hapo na kujimwaga katika chumba kilichokuwa kimeandaliwa na kwamba ndani yake kulikuwa na vinywaji vyakutosha.

Habari hizo zinapasha kuwa, baada ya muda flani, "Mpenzi mpya" aliaga anatoka nje kidogo..Aliporudi ndani hakufunga mlango.

Dakika chache baadaye, waliingia hao vijana wakiwa na 'mpenzi wa zamani"..Walitembeza kichapo kidogo kwa mrembo kisha wakamtia kilevi na baada ya hapo wakafaidi tunda...!!

Habari hizi hazijathibitishwa...Ni habari ambazo ziko barabarani na mitandaoni tangu jana.. Tunafanya jitihada za kuupata ukweli wa mkasa huu kwa kuwasiliana na wahusika..

Tunaahidi kulianika jina la msanii huyo baada ya UPEKUZI wetu kukamilika ikiwa ni pamoja na kujiridhisha kwa kina juu ya SAKATA hili la aibu

HUYU NDIO MTANZANIA ATAKAYE BURUDISHA KWENYE SHOW YA BIG BROTHER AFRICA JUMAPILI HII



Anajulikana kwa Jina la Wakazi ....Ni Mtanzania Ambae yuko katika harakati za Hip Hop muda mrefu japo kipindi cha nyuma alikuwa akizifanyia hizo harakati Marekani ..ila kwa sasa Yupo Tanzania ....Jumapili hii Aburudisha katika Show ya Big Brother ya Kila Jumapili.....Hongera Brooooooo
TOA MAONI YAKO HAPA

OBAMA AWAOMBA RADHI WATANZANIA: SOMA HAPA


Kana kwamba alisikia kilio cha wakazi wa Dar es Salaam waliokuwa na shauku ya kumwona lakini ikashindikana, Rais Barack Obama wa Marekani amewaomba radhi kwa hali hiyo.
Akizungumza juzi wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa ajili yake na ujumbe wake na Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Dar es Salaam, Obama alisema akirudi nchini siku zijazo, atapita mitaani akiwa katika gari la wazi.
CONTINUE READING

"Niliona wananchi walivyojitokeza kwa wingi kutupokea barabarani, nilifarijika sana lakini hawakuweza kutuona vizuri kwani tulikuwa ndani ya gari maalumu-The Beast.

"Miaka ya sitini Rais John Kennedy alipokuja hapa, alipita na gari la wazi mitaani wananchi wakamwona, naomba radhi nikija tena nitaonekana," alisema Obama. 

Watu wengi waliozungumza na vyombo vya habari walionesha dhahiri kiu ya kutaka kumwona Rais huyo wa kwanza mweusi wa Marekani, lakini wakaishia kuona gari lake ambalo hata hivyo, lilipita kwa kasi barabarani kwenda Ikulu na kurudi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Kama ilivyokuwa imezoeleka huko nyuma, Rais wa nchi ambaye amekuwa akifika nchini kwa mara ya kwanza, amekuwa akipita mitaani kwa gari la wazi sambamba na mwenyeji wake akisalimiana na wananchi, hiyo imekuwa ikifanyika pia kwa wasanii wa kigeni.

Hata hivyo, safari hii ulinzi ulionekana kuwa mkali katika ujio wa Rais Obama na kusababisha wenye kiu ya kumwona moja kwa moja kushindwa kufanya hivyo isipokuwa waliokuwa na uwezo wa kufika uwanjani na katika shughuli alizofanya maeneo kadhaa jijini.

Mapema, Rais Kikwete alimhakikishia Rais Obama kwamba kuanzia sasa Afrika itapenda kuona ongezeko la uwekezaji na uhusiano wa kibiashara baina yake na Marekani.

Kikwete alisema hayo juzi usiku katika Ikulu ya Dar es Salaam katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais Obama ambaye alimalizia ziara yake jana.


"Hii inaweza kuwa katika ngazi ya mataifa mawili au Taifa la Marekani na eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki,"alisema Kikwete.

Alimwambia uzinduzi wa Mpango wa Nishati ya Umeme kwa Afrika wenye lengo la kusaidia nchi za Kiafrika kukabiliana na upungufu wa nishati hiyo ni msaada ambao umekuja kwa wakati mwafaka.

Alisema Afrika imekuwa ikilenga kuwa na uchumi mkubwa na hatimaye kujiletea maendeleo, lakini kikwazo kikubwa kimekuwa ni tatizo la umeme wa kutosha.

"Hatua hii ya Marekani kusaidia katika eneo hilo, itakwenda sambamba na kuwezesha mataifa ya Afrika kuibua uwezo wao wa kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu wao," alisisitiza Kikwete.

Alisema hatua hiyo itaimarisha ushindani, itakuza maendeleo ya viwanda na kufanya nchi za Afrika kushiriki vizuri katika uchumi wa dunia na kuwa wabia katika biashara ya kimataifa badala ya kuwa wapokeaji wa misaada ya kigeni.

"Tunakupongeza kwa uongozi wako katika kukabiliana na changamoto za maendeleo na usalama zinazolikabili bara la Afrika. Umekuwa kishawishi kikubwa kwetu, tunaoamini katika demokrasia, uhuru wa mtu, fursa sawa, kutokuwa na ubaguzi na kuwa na Afrika isiyo na migogoro.

"Wewe ni rafiki wa kweli wa Tanzania na Afrika, siku zote tutaenzi amali hizo katika nyoyo na fikra zetu,"Kikwete alimwambia Obama.

Alieleza matumaini ya Watanzania kwamba Obama atapata fursa nyingine ya kuja nchini na kukaa angalau kwa muda mrefu kidogo ili ajionee mengi nchini; nchi ambayo ina vivutio kama Mlima Kilimanjaro, hifadhi za Serengeti na Ngorongoro na kisiwa cha marashi cha Zanzibar. 

Rais Kikwete alimshukuru Rais Obama na Serikali yake na watu wa Marekani kwa msaada wao endelevu kwa Serikali na watu wa Tanzania.

"Msaada wenu katika chakula, elimu, afya, barabara, umeme na maji umesaidia kuboresha maisha ya watu wengi nchini Tanzania.

"Naamini uendelevu wa msaada huo utamaanisha watu wengi kuondokana na umasikini. Kauli yako ya kutuhakikisha kwamba Serikali yako itaendelea kuisaidia Tanzania katika maendeleo imepokewa nasi kwa mikono miwili na unyenyekevu mkubwa," alisema Kikwete.

Akiwa Symbion, Rais Obama aliihimiza Serikali kuhakikisha miradi ambayo itaanzishwa chini ya mpango wa Power Africa utekelezaji wake uharakishwe ili kutoa fursa kwa wananchi kuona manufaa yao katika kujipunguzia umasikini.

Alisema katika mpango huo ambao Serikali yake imeahidi kutoa dola za Marekani bilioni 7, alisema sekta binafsi ambayo itahusishwa kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wake itatoa dola za Marekani bilioni 9.

Alisema kutakuwa na manufaa makubwa iwapo mpango huo utahusisha Serikali na sekta binafsi kwa upande mwingine akiongeza kuwa dhamira ya sekta binafsi katika kutoa kiasi hicho cha fedha inaonesha nia ya Marekani kuinua Afrika yenye nuru," alisema Rais Obama akionesha matumaini ya mpango huo ambavyo unaweza kunufaisha nchi nyingi za Afrika. 

Obama ambaye aliitumia hotuba hiyo kuaga Watanzania, alisema Symbion ni mfano wa miradi ambayo Marekani imedhamiria kuitekeleza Afrika ya kuongeza maradufu uzalishaji wa nishati ya umeme ambayo lengo ni kupunguza umasikini katika bara hilo. 

Alisema ili miradi hiyo iwe na manufaa kwa nchi husika kote alikopita, alitoa mwito kwa viongozi kuhakikisha utekelezaji unaharakishwa ili kunufaisha nchi na kwa watu. 

Alikemea tabia ya ucheleweshaji wa miradi katika Afrika ikiwamo ya umeme lakini akasema ana imani na uongozi wa Rais Kikwete kuwa mpango huo utatekelezwa kwa kasi. "Ni lazima tuongoze katika utekelezaji wa miradi hii na naamini chini ya Rais Kikwete hili linawezekana."

Alisema ili kufanikisha kuwa na umeme wa uhakika ni vema kupunguza urasimu katika kuhudumia wawekezaji wa sekta ya umeme ili wapate nafasi ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi.

Aliongeza kuwa ufanikishaji wa mpango huo utakuwa ni hatua ya ushindi kwa pande zote; yaani kwa Tanzania ambayo itapata umeme wa uhakika ambao utasaidia kupunguza umasikini, lakini pia kwa Marekani ambako wafanyabiashara watapata fursa ya kuwekeza nchini.

Pia alitaka sheria na taratibu zifuatwe na kuheshimiwa katika masuala yote ya uwekezaji ambao utahusisha miradi itakayoanzishwa chini ya mpango wa Power Africa.


Alipoingia ndani ya mitambo ya Symbion, Rais Obama alikabidhiwa mpira wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa gesi.

Mpira huo ambao umebuniwa na vijana wa Kimarekani, unafaa kwa matumizi vijijini kwani unaweza hata kuchaji vifaa vya umeme kama simu ambapo pia gesi hiyo ina uwezo wa kuwasha taa inayoweza kutumika kumulika ndani ya nyumba.

Rais Obama alizindua mipira hiyo ambayo itapatikana hivi karibuni nchini kwa kumpasia Rais Kikwete na kueleza matumaini yake kuwa inaweza kuwa na manufaa makubwa katika maeneo ambako hayajafikiwa na umeme.

Kampuni ya Symbion yenye makao yake makuu Washington, Marekani imeajiri Watanzania 1,000 na Rais Obama jana alitangaza kuwa ni kampuni pekee ambayo itasimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme inayofadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani.

Symbion kwa sasa inatekeleza miradi yenye uwezo wa kuzalisha umeme katika nchi za Afrika Mashariki na Magharibi ambayo imepangwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Katika miaka mitano, kampuni hiyo imepanga kuwekeza kiasi cha Sh trilioni 3 katika uzalishaji umeme na njia za kuusafirisha.

Kati ya miradi hiyo, umo wa gesi unaojengwa Mtwara wenye uwezo wa megawati 400 na unaendeshwa kwa kushirikiana na kampuni nyingine ya Marekani ya General Electric (GE) itakayotoa vifaa vya ujenzi katika mradi huo ambao unahusisha ujenzi wa njia ya umeme yenye umbali wa kilometa 650.

Nchini, kampuni hiyo kwa sasa inamiliki vituo vitatu vya kuzalishia umeme wa jumla ya megawati 217 ambavyo vipo Dar es Salaam, Dodoma na Arusha. Kituo cha Ubungo cha Symbion kinazalisha megawati 112 kwa gesi na ndiyo kampuni inayozalisha umeme mwingi unaoingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Mitambo hiyo imetengenezwa mjini Houston, Texas na inaelezwa kuwa ya kisasa zaidi yenye uwezo mkubwa wa kufua umeme kwa kasi kama ilivyo injini ya ndege. Mitambo hiyo awali ilikuwa ya Dowans ambayo iliileta nchini baada ya kupewa zabuni ya kufanya hivyo na Kampuni ya Richmond.

Awali baadhi ya wabunge walishauri inunuliwe na Serikali, lakini baadhi yao walikataa kuwa ni mitumba na sheria ya manunuzi hairuhusu. Lakini mitambo hiyo ambayo baadhi ya Watanzania waliikejeli leo ndiyo kimbilio la Serikali kutokana na vyanzo vya kufua umeme wa maji kupungua uwezo wake.


Kutokana na mapenzi mengi waliyonayo Watanzania kwa Obama, jana maelfu ya watu walikusanyikwa Ubungo ili kumwona Rais huyo mweusi wa Marekani.

Tangu saa mbili asubuhi Ubungo ilishafurika watu na hadi anawasili eneo hilo saa 5 asubuhi umati huo ulishaongezeka hali inayoonesha kuwa Rais huyo ni kipenzi cha Watanzania.


Baada ya kukagua mitambo ya Symbion, Rais Obama alisindikizwa na mwenyeji wake, Rais Kikwete hadi uwanja wa ndege na akapanda ndege yake ya Air Force One na kurejea Marekani.

WAKENYA BADO WANA HASIRA NA OBAMA, CHEKI WANAVYOMKEJERI




Akiwa nchini Senegal,Rais Obama alinukuliwa na vyombo vya habari akiyasisitiza mataifa ya afrika kuhusu kutambua uwepo wa MASHOGA na kwamba haki zao za msingi ni lazima ziheshimiwe...

Kauli hiyo imewachefua wengi hasa viongozi wa dini nchini Kenya .
Jana, kiongozi wa kiislamu alimuuliza obama swali gumu sana kwamba "Atajisikiaje endapo atabaini kuwa watoto wake wa kike Sasha na Malia ni WASAGAJI???"

Kwa mtazamo huo huo, Wakenya nao wamepaza sauti zao na kumhoji obama kwamba "Angeupataje urais wa marekani kama baba yake mzazi angalikuwa ni SHOGA wa kuliwa 0712, au 0713 au ile 0718????"..

Waafrika wengi wameanza kumuona Obama kama mtu msaliti na mbinafsi.Yeye alizaliwa baada ya wazazi wake kukutana kimwili, mama akabeba mimba na hatimaye akamzaa yeye.Mungu akambariki, leo hii ni Rais wa taifa kubwa duniani.

Iwaje yeye azunguke duniani na kutetea mambo ya USHOGA na ndoa za jinzia moja??

Huo ni ubinafsi..Sitaki niseme mengi.\

Sunday, 30 June 2013

WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI


Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka.

Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.

Kwa mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."

Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.

Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.


Miili ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.

Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.

Inafikiriwa kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.

Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
 
Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.