Huyu Ndio Henry Aliye Uawa |
Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema Akiwatuliza Wanafunzi Wa Chuo Hicho |
----
Taarifa Kutoka Chuo Cha Uhasibu Arusha zinadai kuwa Mwanafunzi Wa BEF 2 anayejulikana kwa jina la Henry ameuawa kikatili na watu wasiofahamika....
Mwanafunzi huyo Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami. Kabla Hajafika Eneo La Malazi (Hostel) alipigiwa Simu na Mwenzake amsubiri Ili Waende Wote Hostel.
Inasemekana Wakati anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo...Wakati wakiendelea kuzozana, rafiki yake naye alifika.....
Majibu Ya Wanafunzi Hao Hayakuwafurahisha Watu Hao Na Ndio Walipochomoa Kisu Na Kumchoma Mmoja wa Vijana Hao Tumboni Na Shingoni na Kupoteza Maisha Hapo Hapo....
Rafiki Aliye Kuwa Nae Inasemekana Alichomwa Kisu Cha Tumboni Na Kuachwa Akishuhudia Mwenzake Akipoteza Maisha.