YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday, 7 August 2013

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA... PICHA ZA WALIOMEZA ZANASWA


Na Mwandishi Wetu
BAADA ya hivi karibuni Taifa la Tanzania kutikiswa na tuhuma nzito ya biashara ya madawa ya kulevya, picha za watu wanaosafirisha bidhaa hiyo haramu kwa njia ya kumeza almaarufu kwa jina la punda, zimenaswa.
Utumbo wa binadamu baada ya kuchanwa ili kutoa kete zenye madawa ya kulevya.
Picha hizo zinazopatikana mtandaoni ambazo hazikujulikana mara moja ni za watu kutoka nchi gani, zinaonesha jinsi madawa hayo yanavyoweza kusafirishwa kwa njia ya kuyameza tumboni huku madhara ya kufanya hivyo yakiainishwa.

MADHARA
Madhara makubwa yaliyoanishwa ni vijana wengi kupoteza maisha kwa urahisi wakati wakihitaji utajiri wa haraka.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyoambatanishwa na picha hizo, watu wanaobeba madawa ya kulevya kwa njia hii wako katika hatari kubwa ya kuweza kuharibu utumbo na kusababisha vifo vya ghafla.
Hali hiyo huweza kutokea pindi madawa hayo yatakapokaa kwa muda mrefu tumboni na kupasuka kutokana na kuchelewa kutolewa.
Kijana mwenye dawa za kulevya akipasuliwa kutolewa madawa.
MFANO WATOLEWA
Katika maelezo ya picha hizo, inadaiwa mmoja wa watu waliokuwa wakifanya kazi hiyo ya ‘upunda’ alipasukiwa na madawa hayo tumboni na kujikuta akifariki dunia baada ya kuchelewa kuyatoa.
Mwingine ilidaiwa kuwa, aliumbuliwa na mashine zilizokuwa kwenye uwanja wa ndege (haukutajwa ni wa nchi gani) na ililazimika  kufanyiwa upasuaji kisha madawa hayo kutolewa.
...Upasuaji ukiendelea.
SAFARI ZA NDEGE HUCHANGIA
Kitu kikubwa ambacho kimekuwa kikiwasababishia vifo wabebaji wengi ni kuahirishwa au kucheleweshwa kwa safari zao za ndege zinazosafiri katika mataifa mbalimbali duniani.
Hali hii huweza kutokea wakati wowote kutokana na hali ya hewa kuchafuka au dharura nyinginezo na kuwakuta wabebaji hao wakiwa hawana ujanja wa kuweza kukwepa  vifo.
...Baada ya utumbo kutolewa.
WAFANYABISHARA, WANASIASA WATAJWA
Katika hili watu wanaotajwa kuwabebesha madawa ya kulevya vijana wa Kitanzania na kuwatuma kuyapeleka katika nchi mbalimbali duniani ni wafanyabishara wakubwa na wanasiasa.
Tuhuma hizi zimekuwepo kwa muda mrefu kwamba vigogo hao huwatumia vijana wa Kitanzania kuhatarisha maisha yao ilhali wao wakitajirika kwa kupata fedha nyingi.
Majina makubwa ya viongozi na watoto wa vigogo yamekuwa yakitajwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine na biashara hiyo haramu na wengi hawajitokezi hadharani kukanusha.
Kete zenye dawa za kulevya baada ya kutolewa kwenye utumbo.
PUNDA WAKUBWA NI WASANII
Punda wakubwa ambao wanatumika kwa ajili ya kubeba madawa ya kulevya ni wasanii wa filamu na wale wa muziki ambao mara kwa mara huonekana wakisafiri nchi mbalimbali duniani.
Inadaiwa wasanii hutumika kwa urahisi kufanya biashara hiyo kwa kuwa ni  vigumu kutiliwa shaka pindi wanapokuwa wanapita kwenye viwanja vya ndege huku wakiwa wamemeza madawa hayo.
Aidha, wasanii wanatumika kwenye biashara hiyo kwa kuwa ni watu wa kusafirisafiri sana kwa shughuli zao za kisanii na pia jamii duniani kote inawapenda, hivyo wana uwanja mpana wa kusaidiwa pindi wanapopata matatizo.
Mtego mwingine wa wasanii unaowafanya kuingia katika  biashara hiyo ni wengi wao kutaka kuishi kifahari tofauti na uwezo wao, hivyo hukubali kuwa punda ili kuweza kupata kipato zaidi  ya kile wanachokipata katika  kazi zao.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
MASOGANGE NA MWENZAKE WAWAUMIZA VIGOGO
Huku hali ikiwa ni ya sintofahamu, baadhi ya vigogo wanaodaiwa kuhusika na biashara hiyo hapa Bongo wanaumia vichwa hasa baada ya msanii, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa Edward kukamatwa nchini Afrika Kusini wakihisi wakati wowote wanaweza kuwataja.
Masogange na mwenzake huyo wanaendelea kuhudhuria mahakamani nchini huko na wakizidiwa wanaweza kuwataja watu waliowatuma kwa kuwa ni vigumu kwao kupitisha  madawa hayo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar bila ya msaada wa vigogo wenye uzoefu wa biashara hiyo.
 
Melisa Edward.
IWE FUNDISHO
Picha zinazowaonesha watu waliokufa kwa kumeza ili kusafirisha madawa ya kulevya na kupoteza maisha yao huku wengine wakiathirika kwa kiasi kikubwa, ziwe fundisho kwa vijana wa Kitanzania ambao wamekuwa wakifanya madili hayo na wale wanaotamani kufanya wajue kwamba kujiingiza huko ni kujitafutia vifo.
chanzo;globalpublisherz.info

CHEKI HII VIDEO YA UTUPU YA AGNES MWASOGANGE HUKO AFRICA KUSINI





RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAMA SALMA WAMJULIA HALI MWENYEKITI WA UDP MH. JOHN MOMOSE CHEYO ALIELAZWA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ES SALAAM


 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali mwenyekiti wa UDP Mh.John Momose Cheyo aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.Katikati ya Rais na Mama Salma ni Mjukuu wa Mheshimiwa Cheyo anayejulikana kama Gabriel Cheyo.Picha Freddy Maro-IKULU

MFANYABIASHARA MKUBWA WA MADINI JIJINI ARUSHA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA.



Pichani juu askari wakikagua mwili wa  Erasto Msuya, mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana ambaye pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kufa papo hapo.

 Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mfanya biashara huyo alifariki dunia mara baada ya majibishano ya risasi baina ya majambazi hayo na mfanya biashara huyo ambapo alizidiwa  nguvu na kupigwa risasi na kufariki dunia

Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara. 

Habari zaidi tuvute subra kidoogo, tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.

UPDATE:SABABU 2 ZILIZOMFANYA MADAM RITA AIHAMISHIE BONGO STAR SEARCH TBC1


Epiq Bongo Star Search ya mwaka 2013 haitaoneshwa tena kupitia ITV. Mwaka huu shindano hilo la kusaka vipaji vya kuimba litakuwa likioneshwa kupitia TBC1.  


Kupitia Facebook, Rita Paulsen aka Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na jaji mkuu wa shindano hilo ametoa sababu mbili za kuhamisha matangazo hayo kutoka ITV hadi TBC1.
 


“Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1. 
 


Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving’amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.”