Matukio yanayotokea Dar es Salaam usiku ni balaa, yaliyotendeka enzi za Sodoma na Gomora ni cha mtoto! Oparesheni Fichua Maovu ya Global kwa mara nyingine imenasa ufuska wa ajabu unaofanyika katika Ufukwe wa Coco, Masaki jijini Dar usiku wa saa 9:00..
Timu ya Risasi ikiwa mzigoni mwishoni mwa wiki iliyopita, usiku tajwa hapo juu na kuendelea hadi kunakucha iliwakuta watu wa kada mbalimbali wakifanya ngono hadharani katika ufukwe huo.
UFUSKA NAMBA MOJA
Katika eneo la wazi lenye mwanga hafifu mchangani, walinaswa mwanamke na mwanaume wakifanya ngono kwa kupakatana bila kujali watu waliokuwa wakikatiza usiku huo kupunga upepo wa Bahari ya Hindi.
Wawili hao walisikika wakitoa miguno ya kimapenzi hadi waliposhtushwa na mwanga wa kamera.
NGONO LAIVU KWENYE GARI
Baada ya kutibua matukio mengine ya kifuska kutokana na mwanga wa kamera, kikosi kazi kiliondoka ufukweni na kwenda kutega kwenye maegesho ya magari.
Katika eneo hilo la maegesho, mwanaume na mwanamke walishtukiwa wakifanya mapenzi bila kujali watu waliokuwa wamelizunguka gari hilo aina ya Toyota Prado, ambalo halikuwa hata na vioo vyeusi (tinted) hivyo mchezo mzima ulishuhudiwa laivu bila king’amuzi hadi polisi wa doria walipofika na kuwagongea, wakaacha ‘kubanjuka’ kwa aibu.
AWAMU YA PILI MCHANGANI
‘Patroo’ ya timu yetu ilitimba kwa awamu ya pili upande wa baharini mchangani ambapo mabinti wa chini ya umri wa miaka 18 walibambwa na ‘mijibaba’ wakiwaridhisha kimapenzi bila kujali wengine ni sawa na baba zao.
Mita chache kutoka pale mabinti hao walipokuwa wakigawa dozi ya mapenzi kwa waliowatoroka wake zao majumbani, kulikuwa na wapenzi waliokuwa ‘wakidendeka’.
FUMANIZI
Wakati hayo yakiendelea eneo hilo, kule chini wanapouza mihogo kulisikika kelele za mwanamke aliyekuwa akilalamika kumfumania mumewe lakini kabla timu yetu haijafika wote walitimua na magari yao waliyokuwa wameyaegesha barabarani.
‘KUKU WATAMU’ WA KUMWAGA
Uchunguzi wetu ulibaini kuwepo kwa mashoga ‘kuku watamu’ wengi pale Coco ambao huzurula maeneo hayo kusaka wanaume.
Wengi wa mashoga hao ni vijana watanashati wa Kiarabu ambao tayari wameshaambukiza tabia hiyo kwa vijana wa Kitanzania.
USAGAJI
Habari za uhakika ni kwamba kuna wanawake wengi ambao hukusanyika eneo hilo usiku kucha wakisaka mabinti wadogo kwa ajili ya kukidhi haja zao za kimapenzi.
Ili kuthibisha hilo, Risasi Mchanganyiko ilishuhudia mwanamke mmoja akimchezea ‘kifua’ mwenzake huku wote wakitoa miguno ya kimahaba.
UBAKAJI
Uchunguzi huo ulibainisha kuwa mara kadhaa katika eneo hilo, wanawake hubakwa na vijana ambao wapo pale muda wote kwa ajili ya kuwafundisha kuogelea.
Uchunguzi huo ulibainisha kuwa mara kadhaa katika eneo hilo, wanawake hubakwa na vijana ambao wapo pale muda wote kwa ajili ya kuwafundisha kuogelea.
Kuna kisa cha hivi karibuni cha wasichana wawili ambao walileweshwa madawa ya kulevya, wakabakwa na baadaye walitelekezwa ufukweni hapo.
Uvutaji bangi na unga ufukweni hapo si jambo jipya kwani ukifika kule mchangani, unakaribishwa na harufu ya ‘kitu cha Arusha’.
Pamoja na ulinzi kuimarishwa na jeshi la polisi bado kuna matukio mengine ya kutisha kama ukabaji, uporaji, biashara kubwa ya ngono na madawa ya kulevya.
Global publisher