YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday, 15 August 2014

NEWS ALERT: WATU NANE WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA MWL.NYERERE WAKIINGIA NCHINI KWA PASPOTI BANDIA ZA MATAIFA TOFAUTI YA ULAYA


 Idara ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere, wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la Uturuki yenye Namba TK 603,  wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa Raia wa Sweden na Belgium.

  Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.      

kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini ambapo suala  la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele. akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa. "Idara ya Uhamiaji, iko macho hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe Raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini"    .

   Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa walikotoka.  Hili ni wimbi lililoibuka hivi karibuni kwa baadhi ya Raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea Mataifa ya Ulaya.

Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo;


1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT    -  SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE    - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF   - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI    - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI      - IRAQ, PPT. NO. G 1111623 

LAANA: JAMAA ATEMBEZWA UCHI MTAANI BAADA YA KUOMBA ALAWITIWE NA MWANAUME MWENZIE, KILA KITU KIPO HAPA





Matukio ya kulawitiana yameendelea kuchukua sura mpya baada ya mkazi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa wa mtaa wa Maporomoko uliopo katika mji mdogo wa Tunduma uliopo Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya ,ametembezwa uchi wa mnyama mjini baada ya yeye mwenyewe kutaka kulawitiwa na mwanamume mwenzake ambaye naye jina tunalihifadhi. 

Tukio hilo lilitokea juzi huko mtaani na mbinu waliotumia ili kumkamata ni mmoja kati yao kukubali kitendo hicho cha ajabu cha ulawiti baada ya kushawishiwa sana bila kujua kuwa mwenzake ameshaandaa watu ili wamuumbue kwa hilo. 

Aliendelea kwa kusema kuwa mmoja huyo alianza kwa kumuandikia sms ya kusema kuwa anataka amuingize kwenye ulimwengu wa mapenzi kitu kilicho mshtua mwanaume huyo ambaye alikuwa anatongozwa na mwanaume mwenziye ili akamlawiti. 

Aidha alisema kuwa aliamua kukubali na kumchukua kwenda naye kwenye chumba chake alichopanga ili waanze kazi baadaya ya yule mwanaume kutoa nguo zote mwenzake akapiga simu kwa mwenzake ambaye alikuwa anakaa naye pale ambaye alitambulika kwa jina moja la Asifiwe ili wamuumbue. 

Asifiwe aliwaita watu wengi waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya kumshikisha adabu njemba hiyo inayotaka kulawitiwa ndipo akafumaniwa na kula kichapo cha hali ya juu na wakaamua kumtembeza uchi mtaa mzima. 

tulijaribu kumtafuta mtuhumiwa kwa bahati mbaya hatukuweza kumpata kutokana na kuzingirwa na umati wa watu ili aeleze sababu zilizo mfanya atake kufanya hivyo. 

Na kwa upande wa mashuhuda walisema kuwa labda ni masharti ambayo atakuwa amepewa na mganga wa kienyeji kutokana na mali alizokuwanazo ili zizidi kuongezeka basi afanye mchezo huo mchafu.

LOUIS VAN GAAL AMSIFU WAYNE ROONEY NA KUELEZA KWANINI AMEMPA BEJI LA UNAHODHA


1408112382707_wps_1_MANCHESTER_ENGLAND_AUGUSTKiongozi: Louis van Gaal alisema mtazamo wa Wayne Rooney ndio sababu ya kumteua kuwa nahodha.
LOUIS van Gaal amesifu mtazamo wa Wayne Rooney na kuamua kumteua kuwa nahodha wa Manchester United, lakini amemuonya kujiheshimu nje na ndani ya uwanja.
Mholanzi aliweka wazi kuwa alizungumza na Roonye kuhusu kumvalisha kitambaa cha umeneja baada ya mechi ya jumanne usiku dhidi ya Valencia kufuatia mshambuliaji huyo kujituma zaidi kuwa kiongozi.
K

FUMANIZI KUTOKA MABIBO:AFUMWA LIVE AKINGONOKA NA SHEMEJI YAKE..!!!



KABAANG! Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar, amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.Picha tofauti juu zikionesha mke wa mtu na mgoni wake katika fumanizi liliotokea. 

Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake wakipeana maraha. Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda katika shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki yake na kufanya mchezo wa kikubwa

HEADLINE ZA MAGAZETI YA UDAKU LEO





RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA WAPYA 20 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose
Migiro, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu,  Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue, Mwanasheria Mkuu Jaji  Frederick Werema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein kattanga  katika picha ya pamoja na
Majaji wa Mahakama kuu ya Tanzania baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  Majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wapya
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  Majaji wa Mahakama ya Kuu Tanzania na Majaji  wapya
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  majaji wapya 
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa na Majaji wapya 
 Rais Kikwete na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro wakiwa wa wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wanawake wapya
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa katika pic ha ya jumla na Majaji wapya na wa zamani. 

KIBANO! TRAFIKI WAMFUNGIA KAZI DEREVA JEURI WA UDA




Stori: Deogratius Mongela na gabriel ng’osha

DEREVA wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibano hevi na askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila shuruti.

Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimdhibiti dereva wa basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) aliyevunja sheria ya usalama barabarani. 
Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo kukataa kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP lililokuwa limevunja sheria ya usalama barabarani.
Dereva huyo akionyesha ubishi wa kutotii maagizo ya 'trafiki'.
Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo kimedai kuwa, kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini na kazi yao, walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva huyo sambamba na kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha chafu kitendo ambacho trafiki hao walishindwa kukivumilia.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimtoa nje dereva jeuri wa UDA.
“Waliendelea kutoa lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe walichokosea ndipo trafiki wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti, tunawapongeza trafiki hawa kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya trafiki kuwadhibiti wawili hao,  mmoja wao alishika usukani, wenzake wakakaa kwenye viti na kuliendesha basi hilo hadi  Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.
Tunashauri madereva kuwa makini na watiifu pindi wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali ambazo nyingi kati ya hizo zimekuwa zikitokana na uzembe wa madereva kwa kutotii sheria za usalama barabarani-

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 16/08/2014













ANGALIA PICHA: BILL GATES NA FAMILIA YAKE WAPO LIKIZO KWENYE BOTI WALIYOKODI KWA TSHS BILIONI 8 KWA WIKI...!!




Katika boti hiyo helikopta zinamchukua Gates kumpeleke nchi kavu kucheza golf na kumrudisha Ni tajiri namba moja duniani mwenye utajiri unaofikia dola bilioni 79.2 hivyo kutumia shilingi bilioni nane kwa wiki si kitu kinachoweza kumpunguzia chochote Bill Gates.Na ndio maana Bill Gates yupo mapumzikoni ambayo tunategemea kwa mtu tajiri zaidi duniani ayafanye. 
Tajiri huyo amekodi meli binafsi maarufu yacht ambayo analipa dola milioni 5 (zaidi ya shilingi bilioni 8) kwa wiki. 




Muonekano wa sehemu moja wapo ya ndani 

Wednesday, 13 August 2014

DEREVA WA BODABODA ASAKWA KWA KUUA.

Jeshi la polisi Mkoani Iringa linamtafuta dereva wa pikipiki kwa tuhuma ya kusababisha kifo cha mtembea kwa miguu kwa ajali ya barabarani kisha kukimbia baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema Mfaume Kilangi ambaye pia ni mwenyekitio wa kijiji cha Idodi wilaya ya Iringa Vijijini Mkoani Iringa akiwa anaendesha pikipiki ambayo haijafahamika namba zake za uasjili ilimgonga na kusababisha kifo cha Laurent Kafwela umri miaka 40.

Aidha ameongeza kuwa marehemu amefariki muda mfupi akiwa anakimbizwa katika hospitari ya Mapogoro wilaya ya Iringa Vijijini Mkoa wa Iringa na chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa kutochukua tahadhari kwenye makazi ya watu.Hata hivyo Kamanda Mungi amesema ajari hiyo imetokea katika eneo la Mapogoro katika barabara ya Idodi-Tagamenda wilaya ya Iringa Vijijini pia ametoa wito kwa wamiliki na madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajari zinazoweza kuepukika

RIHANA ASHAULIWA NA DROGBA KUINUNUA LIVERPOOL

Rihanna anataka kuinunua Liverpool FC, ashauriwa na Drogba

posted 4 hours ago by admin
Mapenzi ya Rihanna kwenye soka yameingia katika hatua nyingine na sasa hataki kuwa shabiki tu bali mmiliki halali wa timu kubwa duniani, na kwa kuanza anataka kuinunua Liverpool FC!
Kwa mujibu wa gazeti la Hispania, El Mundo Deportivo mwimbaji huyo alianza mpango huo muda mfupi baada ya kuisha kwa fainali za kombe la dunia nchini Brazil ambapo alionekana akitweet mara kwa mara kuhusu mechi zilizokuwa zinaendeelea.
Gazeti hilo limeeleza kuwa Rihanna amekuwa akipata ushauri kutoka kwa marafiki zake wa karibu akiwemo mchezaji wa Chelsea, Didier Drogba ili kufanya maamuzi sahihi katika ununuzi wa club ya mpira wa miguu.
Kwa sasa Liverpool inamilikiwa na John W. Henry na hana mpango wa kuiuza timu hiyo ya soka.
Huwezi jua, endelea kutembelea www.timesfm.co.tz kufahamu kitakachoendelea

WANAWAKE WAPINGA JESHI KUPELEKA WAUME ZAO VITANI.

Wanawake wayazuia magari ya jeshi yaliyokuwa yakiwapeleka waume zao kupigana na Boko Haram

posted 1 day ago by admin
Ripoti kutoka Nigeria zinaeleza kuwa Jumamosi iliyopita kundi kubwa la wanawake lilijitokeza na kuzuia magari ya jeshi yaliyokuwa yamewabeba wanaume wao na wake zao yakielekea katika mji wa Gwosa, sehemu ambayo inadhibitiwa na kundi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa Prime Times ya Nigeria, wanawake hao walizua geti la barracks katika mji wa Borno huku wengine wakilala barabarani kushinikiza waume zao wapewe vifaa vya kisasa na imara zaidi ndipo waende vitani kupambana na kundi hilo.
Hali hiyo imekuja baada ya kuripotiwa kuwa karibu wanajeshi 60 waliuawa Jumatano iliyopita katika eneo la Gwosa linalomilikiwa na Boko Haram na kudaiwa kuwa sababu kubwa ni zana duni walizokuwa nazo kulinganisha na zana za kisasa za kijeshi za kundi hilo.
Chanzo kimeiambia Prime Times kuwa wanawake hao walieleza kuwa hawataki kubaki wajane na yatima kama wenzao kwa sababu ya vita hiyo.
“Mwanamke mmoja alisema ‘hatutaki kuwa kundi lingine la wajane, wapeni waume zetu zana bora zaidi za kivita, silaha na magari bora zaidi la sivyo hawaendi kokote’.”
Wanajeshi wengine pia walionekana kuunga mkono madai ya wanawake hao na kusukuma lawama kwa maafisa wa serikali.
We are ever ready to tackle Boko Haram terrorists but our superior officers are the ones killing us by not giving us the right arms to execute the war. How could I go and face Boko Haram with AK47 that is charged with only three cartridges when the enemy is brandishing modern GPMG, AA, RPG and so on.”Alikaririwa mwanajeshi mmoja.
Kundi la Boko Haram bado linawashikilia mateka wanafunzi wa kike zaidi ya 200 na wanawake wengine huku likitekeleza mauji ya kutisha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 13.08.2014


.
23_45aae.jpg
2_af633.jpg

21_8f720.jpg
4_14e1c.jpg 3_f7699.jpg
22_736c8.jpg
04_6bac1.jpg
37_65b2d.jpg
5_301d6.jpg

31_cdf56.jpg6_2baf6.jpg
30_568a1.jpg
7_b2b38.jpg
38_85748.jpg
11_51f64.jpg
36_622b3.jpg
12_69ac7.jpg
35_558f6.jpg
39_48121.jpg